Ambwene Mwasongwe ni msanii ambae nyimbo zake zimebeba ujumbe murua, ambao unawavutia watu wa aina mbalimbali walio wakristo na hatata watu wa dini zingine kusikiliza.
Mwasongwe amekuwa na uimbaji wa tofauti na wasanii wengine Afrika ya mashariki na barani Afrika , hasa katika utunzi wa nyimbo zake ambazo zinakuwa zimebeba ujumbe mzito ambao mtu yeyote akisikiliza zinamfanya atafakari zaidi
Moja kati ya nyimbo zake ambazo watu wengi wamekuwa wakipenda kusikiliza ni MAJARIBU NI MTAJI, MISULI YA IMANI na UPENDO WAKWELI hizi ni baadhi ya nyimbo za Mwasongwe ambazo zinasikilizwa kwa kiasi kikubwa.
Msanii huyu amezaliwa mwaka 1985, ambapo alianza kuimba nyimbo za injili akiwa na umri wa miaka 16 na kutoa albamu yake ya kwanza inyoitwa Majaribu ni mtaji, akiwa na miaka 19, ikiwa mpaka sasa ametoa albamu tatu yapili ikiitwa Heshima ya mrefu ni mfupi maarufu kama mzee wa siku, na ya tatu ni Misuli ya imani.
Pia mwasongwe amekuwa akitamani sana nyimbo zake zifuke ulimwenguni kote, na sio Tanzania tu ili kuwatia moyo watu wanaopita kwenye mazingira tofauti tofauti na magumu ili wazidi kusonga mbele.