Ambwene Mwasongwe - Wamechoma Moto Lyrics
Lyrics
Nilikuta mtu amelala kakauka Anafuka moshi, wamemchoma moto Kila nikikumbuka thamani ya mtu bado moyo wanhu wauma Waliozunguka ule mwili wengi, walitema mate na kushangilia Nikasikia maneno amekoma, wanatusumbua sana Nikawaza angekuwa mwanangu Nikawaza, angekuwa ndugu yangu Nikawaza, ningekuwa mungu wake Maumivu yangekuwaje? Nikatamani nimnon’oneze Nimuulize, nini kimemkuta? Bahati mbaya hawezi sikiaaaa, amekufa kwahuzuni Nikamkumbuka mama yake nyumbani Kapokeaje taarifa hizi mbaya Bahati mbaya, liliumaje kuletewa maiti ya mwanawe Nikamkumbuka mungu amejisikiaje Mwanadamu aliyeumbwa kwa ajabu na kutisha Ndipo, nikamchukia shetani Anavyitafuna maisha ya watu eeeh eeeeh Bwana yakumbuke maneno, yale ya mwisho Waliolia wakijuta, wanapokufa Kumbuka ile hali ya kupoteza Maisha ukarehemu ukawasikie
Wakiita aaah uwasikieeee Ukakumbuke wema wa kwako mwenyewe Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe Wakiita aaah uwasikieeee Ukakumbuke wema wa kwako mwenyewe Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe
Wananyongwa kwa ubaya Wananyongwa kwa aibu Wanamezwa na dunia wanapotea aaah Magonjwa laana shida mateso Vinawatafuna hawaelewi Wanahitaji msaada wako Wanahitaji huruma ya kwako Maana ni ya kwako uliwaumba uliwafanya aaah Shetani kawadhulumu maisha Wakiitaji msaada, bwana ukawajibu Katazame machozi na damu walizomwaga ukawakumbuke Kama hautawahurumia wao basi Hurumia wanaowategemea eeeh Hurumia wanaoumizlzwa na matendo yao Bwana ukawarehemu Kama ukiwatupa wewe unamtupia nani Kama ukiwageuzia kisogo waende kwa nani Maana kwako ndiko kuna wema Wewe ni mungu wa kusamehe Bwana ninawaombea watu
Wakiita aaah uwasikieeee Ukakumbuke wema wa kwako mwenyewe Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe Wakiita aaah uwasikieeee Ukakumbuke wema wa kwako mwenyewe Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe Wakiita aaah uwasikieeee Ukakumbuke wema wa kwako mwenyewe Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe Wakiita aaah uwasikieeee Ukakumbuke wema wa kwako mwenyewe Wakilia, wanapoumia ukawajibu maana ni wako mwenyewe
Video
AMBWENE MWASONGWE_WAMECHOMA MOTO LYRICS