Tumekuja Kukuchukua

Tumekuja Kukuchukua Lyrics

ieyee yaah hayaa yeeh
Tumekuja kukuchukua 
ieyee yaah hayaa yeeh
Tumekuja kukuchukua  .

Bibi harusi (Tumekuja kukuchukua) 
Bibi harusi twende mama (Tumekuja kukuchukua) 
Bibi harusi (Tumekuja kukuchukua) 
Wazazi wako tumeelewana nao (Tumekuja kukuchukua) 
Wameturuhusu tuondoke nawe (Tumekuja kukuchukua)  .

Tusingeweza kukuchukua bila ruhusa ya wazazi wako 
Ndio maana tulisafiri kwenda kuwaomba wazazi wako 
Ili turuhusiwe, zawadi mbali mbali tuliwapelekea 
Tunashukuru Mungu walizipokea 
Tulipowaomba tukuchukue 
Kuna taratibu tuliambiwa tuzifuate 
Taratibu zote tulizifwata,
Hapo ndipo tuliporuhusiwa 
Tumepewa baraka zote wewe uwe mke wa kijana wetu 
Bibi arusi wewe 
Tumepewa baraka zote wewe uingie kwenye ukoo wetu 
Bibi arusi wee .

Tunamshukuru Jehovah (Tumekuja kukuchukua) 
Maombi yetu ameyasikia (Tumekuja kukuchukua) 
Tumeomba muda mrefu sana (Tumekuja kukuchukua) 
Kijana wetu apate mke (Tumekuja kukuchukua) 
Maombi yetu yamejibiwa (Tumekuja kukuchukua) 
Wewe ndiye jibu la maombi yetu (Tumekuja kukuchukua) 
Sisi unaotuona (Tumekuja kukuchukua) 
Ni ndugu wa Bwana arusi (Tumekuja kukuchukua) 
Tumesindikiza ndugu yetu (Tumekuja kukuchukua) 
Tumekuja kukuchukua wewe (Tumekuja kukuchukua) 
Tunawashukuru ndugu zako (Tumekuja kukuchukua) 
Wametupokea vizuri sana (Tumekuja kukuchukua) 
Bibi arusi twende wee (Tumekuja kukuchukua) 
Twende kwetu mama   .

Tunatimiza maandiko (Tumekuja kukuchukua) 
Kama ilivyoandikwa (Tumekuja kukuchukua wewe) 
Mtu ataacha wazazi wake (Tumekuja kukuchukua) 
Ataambatana na mumewe (Tumekuja kukuchukua) 
Bibi arusi twende wee (Tumekuja kukuchukua) 
Malkia wetu twende (Tumekuja kukuchukua) 
Usiogope twende (Tumekuja kukuchukua) 
Yanatimizwa maandiko (Tumekuja kukuchukua) .


Share:

Write a review/comment of Tumekuja Kukuchukua :

0 Comments/Reviews


Bony Mwaitege

@bony-mwaitege

Bio

View all songs, albums & biography of Bony Mwaitege

View Profile

Bible Verses for Tumekuja Kukuchukua

Ephesians 5 : 31

For this cause will a man go away from his father and mother and be joined to his wife, and the two will become one flesh.

Mp3 Songs & Download from iTunes

  • listen on Itunes Music