Bony Mwaitege - Utanitambuaje - Tazama Matendo Lyrics

Lyrics

Utanitambuaje kama nimeokoka? Utanitambuaje kama namweshimu Mungu? Nasema, utajuaje kama tuko pamoja Katika safari ndefu ya kwenda mbiguni eeh? Utanitambuaje ndugu yangu nakuuliza niambie aiyee

Huwezi kunitambua kama nimeokoka, kwa kunitazama sura yangu Huwezi kunitambua kama nimeokoka kwa kunitazama maumbile yangu Bwana asifiwe isiwe sababu kukufanya uamini kuwa nimeokoka Japo mali yangu naweza kutamka Bwana asifiwe kumbe sijaokoka Utanitambuaje niambie aiyee

Ukitaka kutambua kama nimeokoka Hakuna haja ya kupata shida Ukitaka kutambua kama nimeokoka
Hakuna haja ya kuumiza kichwa Bwana wetu Yesu alishasema Utawatambua kwa matendo Matendo tazama matendo utanitambua eeh

Matendo yangu, tazama matendo Matendo tazama matendo Kama kweli ninamcha Mungu utanitambuaje

Usinitazame umbile tazama matendo Matendo tazama matendo Matendo tazama matendo Kama kweli ninamcha Mungu utanitambuaje Hata kama nimebatizwa tazama matendo Matendo tazama matendo Matendo Kama kweli ninamcha Mungu utanitambuaje

Mtume Petro aliulizwa wewe ni mwanafunzi wa Yesu. Mtume Petro kwa kuogopa wayahudi akakataa mimi simjui Yesu Wakamwambia mbona hata kusema kwako Kunaonyesha wewe mwanafunzi wa Yesu Mtume Petro akaamua kuondoka Hata hivyo wakamtambua mwendo wake Wakamwambia mbona hata kutembea kwako Kunaonyesha wewe mwanafunzi wa Yesu Kuongea na kutembea kwake Petro Kulionyesha yeye mwanafunzi wa Yesu Matendo yangu matendo tazameni matendo utanitambua eeh

Matendo tazama matendo Matendo tazama matendo Matendo, Kama kweli ninamcha Mungu utanitambuaje

Ukitaka kutambua kama nimeokoka Usitazame jinsi ninavojisifia Naweza kujisifu mimi ni mpole sana Lakini matendo yangu yakakataa Naweza kujisifu mimi nawajali sana yatima Lakini matendo yangu yakakataa Naweza kujisifu mimi nawajali sana wajane Lakini matendo yangu yakakataa Matendo yangu matendo Kama kweli ninamcha Mungu utanitambua aiyee

Video

Utanitambuaje By Bony Mwaitege

Thumbnail for Utanitambuaje - Tazama Matendo  video
Loading...
In Queue
View Lyrics