Mama ni Mama Lyrics - Bony Mwaitege
Bony Mwaitege swahili
Chorus:
Mama mama mama, uwezo wa kukulipa sina
Kwa taabu ulininyonyesha
Namwomba Mungu akupe baraka mama
ooh Mama, mama aah
Mama ni Mama Video
Mama ni Mama Lyrics
Mama mama mama, uwezo wa kukulipa sina
Kwa taabu ulininyonyesha
Namwomba Mungu akupe baraka ooh Mama
Imeandikwa waheshimu wazazi wako
siku zako zipate ongezeka
Imeandikwa waheshimu baba na mama
vijana wengi waheshimu baba peke yake
Kwa kuwa mama ni mpole wengi wanamdharau
Unatenda dhambi ukimdharau mama ni mama huyo
Ni mama yako usimpigie Ngumi
Ni mama yako huyo usimtukane
Ni mama yako usimnyoshe kidole
Mama ni mama hata kama huna msingi elimu ni mama huyo x2
Mama mama mama, uwezo wa kukulipa sina
Kwa taabu ulininyonyesha
Namwomba Mungu akupe baraka mama
ooh Mama, mama aah
Mama yako alinusurika kufa wakati unazaliwa wewe dada
Aliweka roho mkononi wakati wa kuzaliwa kwako kaka
Mama yako alinusurika kufa wakati unazaliwa wewe baba
Aliweka roho mkononi wakati wa kuzaliwa kwako dada
Ni mama yako usimpigie Ngumi
Ni mama yako huyo usimtukane
Ni mama yako usimnyoshe kidole
Mama ni mama hata kama huna msingi elimu ni mama huyo
Mama mama mama, uwezo wa kukulipa sina
Kwa taabu ulininyonyesha
Namwomba Mungu akupe baraka mama
ooh Mama, mama aah
Unapata wapi ujasiri wa kumtukana mama
Unapata wapi ujasiri wa kumpunja mama
Unapata wapi ujasiri wa kumpiga mama
Unapata ujasiri pepo ni pepo hiyo
Uponywe kwa jina la Yesu
Mama mama mama, uwezo wa kukulipa sina
Kwa taabu ulininyonyesha
Namwomba Mungu akupe baraka mama
ooh Mama, mama aah
Mungu alimuamini mama akakuweka tumboni miezi tisa
Mama yako alikuwa mwaminifu kwa Mungu, akakutunza tumboni miezi tisa
Kumbuka baba yako naye anayo tumbo, jiulize kwa nini hukuwekwa kwa baba yako
Ooh mama
Mama mama mama, uwezo wa kukulipa sina
Kwa taabu ulininyonyesha
Namwomba Mungu akupe baraka mama
ooh Mama, mama aah