Mtoto Wa Mwenzio Lyrics - Bony Mwaitege

Bony Mwaitege swahili

Mtoto Wa Mwenzio Lyrics

Yesu alisema wacheni watoto waje kwangu
Maana ufalme wa mbinguni ni wao msiwazuie
Alionyesha upendo kwa watoto

Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Endesha gari polepole usije kugonga mtoto
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Endesha pikipiki polepole hapo mbele kuna watoto
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Aah Mtoto wa mwenzio ni wako
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako

Mwanza wa Sukuma wanasema ---
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Uluya wanasema ---
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Wajaka wanasema ---
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Iringa wanasema ---
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Wasafa wanasema ---
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako

Pengine akikua atakuwa doctor akutibu nawewe
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Pengine akikua atakuwa mwanajeshi atulinde wote
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Pengine akikuwa atakuwa raisi atulinde wote
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Huenda ta rais wa sasa ni mtoto wa mwenzako
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Mtoto wa mwenzio mthamini kama wa wako

Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Endesha gari polepole usije kugonga mtoto
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Endesha pikipiki polepole hapo mbele kuna watoto
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
Aah Mtoto wa mwenzio ni wako
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto kwako

Mtoto wa mwenzio mheshimu usimtamkie maneno mabaya
Mtoto wa mwenzio ametoka shule usimchanganye
Mtoto wa mwenzio mtie moyo aweze kusoma
Mtoto wa mwenzio usimchanganye na chipsi nyama choma
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto kwako


Mtoto Wa Mwenzio Video