Sifa Lyrics

Mkono wa Bwana by Zabron Singers cover art

Zabron Singers - Mkono wa Bwana Lyrics

Artist:
Zabron Singers

Lyrics

Intro


Tumeuona mkono wake Bwana


Verse 1


Mengi mazuri tumeyaona, Mungu umetenda
Ni kweli we muweza
Ulitamka vitu vikawa
Neno tu latosha
Ukisema umetenda
Bahari shamu Isiraeli
Ah uliwavusha
Kawatoa utumwani
Watumishi wako umewapa
Yote waombayo
Ikiwa umependezwa


Pre-Chorus


Uamulo hakuna wa kulipinga
Hakika we ni Mungu, wa vyote
Unatawala dunia na vilivyomo
Makuu umeyatenda, Jehova


Chorus


Refrain:
Tumeuona, mkono wako Bwana
Matendo yako Bwana ni makuu mno
Umetutoa mbali, ukatushika mkono
Mahali uliona pekee hatuwezi
Chini hata juu, watu unawainua
Sifa na utukufu ni zako milele
Twasifu jina lako, milele tutakusifu
Daima we u mwema tutaishi kwako


Tumeuona, mkono wako Bwana
Matendo yako Bwana ni makuu mno
Umetutoa mbali, ukatushika mkono
Mahali uliona pekee hatuwezi
Chini hata juu, watu unawainua
Sifa na utukufu ni zako milele
Twasifu jina lako, milele tutakusifu
Daima we u mwema tutaishi kwako


Verse 2


Ona ona ona ona
Msalabani ulitufia, hm ulitupenda
Dhambi zetu ukabeba
Baraka zako tuliziomba kweli tumeona
Hakika unabariki
Hata vipaji we ndo hutoa umetuwezesha
Tunaimba na kusifu
Walio haki hutowaacha, uliwaahidi
Hata mwisho wa dahari


Bridge


Hm watu wako umewapa mamlaka
kwa jina lako Yesu
Waponye
Na huna ubaguzi
Wote ni sawa kwako
Umetuita Yesu, tupone


Outro


(Refrain)


Ona ona ona
Daima we umwema tutaishi kwako
(Repeat)


Video

Meaning & Inspiration

“Mkono wa Bwana” by Zabron Singers is a praise song focused on recognizing God’s help, guidance, and power. The recording moves from testimony into communal thanksgiving, with a recurring refrain that gives it a celebratory, worshipful character.