Zabron Singers - Imeniuma Sana Lyrics

Imeniuma Sana Lyrics

Hili limeniliza sana  
Hili limeniumiza sana  
Awamu hii nimeumia sana  
Mungu wangu nisaidie eeh  
Mbona umeniacha sana  
Katika hili nimeumia sana aaah  
Nakiri nakuhitaji sana  
Mungu wangu nisaidie eeeh  

Ungeniuliza nisingekubali mimi  
Mpendwa wangu nimeache aende eeh  
Rafiki yangu kipenzi aende  
Mungu hapana kwangu si sawa aah  
Ile mipango imezima  
Kwako ni sawa ila nabaki peke yangu  
Nitafanyaje nimeachwa peke yangu  
Mungu hapana, kwangu si sawa aah  
Ila naelewa Mungu uuh  
Kazi yako haina kosa aaah  
Nakushukuru kwa yote  
Mapenzi yako yatimizwe eeeh  

Hili limeniliza sana  
Hili limeniumiza sana  
Awamu hii nimeumia sana  
Mungu wangu nisaidie eeh  
Mbona umeniacha sana  
Katika hili nimeumia sana aaah  
Nakiri nakuhitaji sana  
Mungu wangu nisaidie eeeh  

Japo nawaza nafarijika bwana  
Kwamba kunayo siku tutakutana nae  
Ile asubuhi njema uloiweka pale  
Kwa watu wanao kuamini yesu  
Nitie nguvu baba nimechoka  
Moyo unauma nimechoka aaah  
Nisaidie baba nimechoka  
Peke yangu mimi siwezi  

Tufundishe Mungu wetu  
Kuhesabu siku zetu  
Japo dhoruba na shida  
Tusichoke kukutumikia  

Hili limeniliza sana  
Hili limeniumiza sana  
Awamu hii nimeumia sana  
Mungu wangu nisaidie eeh  
Mbona umeniacha sana  
Katika hili nimeumia sana aaah  
Nakiri nakuhitaji sana  
Mungu wangu nisaidie eeeh  

Mtu wa watu huyu  
Mwenye upendo huyu  
Mpatanishi huyu  
Kaenda vipi tena aah  
Mtu wa watu huyu  
Mwenye upendo huyu  
Mpatanishi huyu  
Kaenda vipi tena aah  



IMENIUMA SANA by Zabron Singers (Official Video)

Zabron Singers Songs

Related Songs