Zabron Singers - Nawapenda (I Love U) Lyrics

Nawapenda (I Love U) Lyrics

Ninaye rafiki kipenzi, kipenzi namwita mama
Ana pacha wake yeye ninamwita daddy
Hawa ni wazazi wa mimi, na leo nina wimbo wao
Tuseme mazuri mengi walotufanyia


Nikianza na mama we ndo wangu superwoman (Superwoman)
Unajua mengi juu ya mi mwanao mama
Kwanza nilikusumbua, utoto ni vita vita
Na vistick nilichezea, lengo unifunze tabia njema


Mama haa, tumboni ulinibeba
Na uvumilivu mimi ukanilea 
Miezi tisa tumboni mwa mama
Shida mateso yote nilivumilia


Nilipozaliwa mimi ulinivisha na kuninywesha
Nilipokuwa mdogo ulihakikisha niko salama
Nakupenda mama, haaa
Asante mama, heee


Hata siku ya birthday yako ikifika
Nitakuimbia, happy birthday mummy
Happy birthday mummy I love you mama 


Namzungumzia mama, mama 
Mama yetu mama
Mi mwanao nakupenda, mama nani kama mama


I love you mummy
I pray for you mummy, wangu mummy
Nakupenda mama, mama
I pray for you mama


Baba ulihangaika baba
Upate chochote wanao tule
Na nguo tuvae, na shule twende baba 
Tusome twende


Nakumbuka na ule usia, kusali kuomba tushike
Niwe mtu mwema kwa Mungu na watu niwe mtu wa watu
I love, I love you
I love you daddy


Namzungumzia baba, baba
Baba yetu baba
Mi mwanao nakupenda
Baba, baba yetu baba


I love you daddy
I pray for you daddy
I love you daddy
I pray for you daddy, daddy


Nitakuja nyumbani nichukue baraka
Maisha yangu yapendeze mama 
Umwambie na baba, nampendaga sana
Anipe neno la baraka pia


Kuna muda namuomba Mungu awazidishie
Uzima maisha mazuri nije niwatunze
Muone matunda ya mi mwanenu
Muone  na niwafurahishe, I love you


I love you daddy (Baba)
I pray for you daddy (Wangu baba)
Nakupenda wangu baba, baba
I pray for you baba, wangu baba


Amri ya tano na ya Mungu
Waheshimu baba na mama yako
Na siku zako zije kuwa nyingi
Zipate kuwa nyingi, zipate kuwa nyingi


Asanteni wazazi nawapenda
Hakika nyinyi ndio kila kitu kwangu
Hata baraka zangu chanzo ninyi
Nawaombea mema, nawaombea mema


I love you, I love you
I love you mummy
Daddy, daddy daddy
Mummy, mummy mummy
Daddy mi mwanenu nawaombea kwa Mola


Nawapenda (I Love U) Video

Zabron Singers Songs

Related Songs