Zabron Singers - Unaendeleaje Lyrics

Unaendeleaje Lyrics

Verse1
Unakumbuka jinsi ulikua mtu mzuri, Unaendeleaje..?
(Do you remember how you were a good person, how are you doing?)
Tukakuita Church boy tena mtu wa Mungu, Unaendeleaje..?
(We called you a Church boy, a man of God, how are you doing?)
Unakumbuka jinsi ulikua mtu wa wema, Unaendeleaje..?
(Do you remember how you were a person of goodness, how are you doing?)
Tukakuita Church girl tena mtu wa Mungu, Unaendeleaje..?
(We called you a Church girl, a woman of God, how are you doing?)

Mtu wa watu, mwenye kujali, mwenye upendo mwingi
(A person of the people, caring, full of love)
Ulifurahisha wanadamu na Mungu wa mbinguni.
(You made people and the God of heaven happy.)
Nawaza naumia, Safari ni ya wote,
(I think and hurt, the journey is for everyone,)
Unaendeleaje..?
(How are you doing?)

Furaha yangu mimi, nione tupo wote,
(My joy, let me see we are all together,)
Safari ni pamoja.
(The journey is together.)

Unaendeleaje na maombi yako kwa Mungu, Unaendeleaje..?
(How are you doing with your prayers to God, how are you doing?)
Unaendeleaje na ibada yako kwa Mungu, Unaendeleaje..?
(How are you doing with your worship to God, how are you doing?)
Unaendeleaje na sadaka zako kwa Mungu, Unaendeleaje..?
(How are you doing with your offerings to God, how are you doing?)
Unaendeleaje na imani yako kwa Mungu, Unaendeleaje..?
(How are you doing with your faith in God, how are you doing?)
Unaendeleaje..? Unaendeleaje... eh?
(How are you doing..? How are you doing... eh?)
Unaendeleaje.. eee? Unaendeleaje... eh?
(How are you doing..? eee? How are you doing... eh?)



Verse 2
Unakumbuka enzi ulikua shemasi wetu, Unaendeleaje... eh?
(Do you remember the time you were our deacon, how are you doing... eh?)
Mzee wa kanisa, mchungaji, bawabu wetu, Unaendeleaje... eh?
(You were the elder of the church, the pastor, our usher, how are you doing... eh?)
Je wakumbuka jinsi ulipenda neno la Mungu, Unaendeleaje... eh?
(Do you remember how you loved the Word of God, how are you doing... eh?)
Kwenye makambi kanisani kote tulikuona, Unaendeleaje... eh?
(At all the church camps, we saw you, how are you doing... eh?)

Waendeleaje na ndoa ya ujana wa siku zako,
(How is your youthful marriage from your days,)
Ulitutia na moyo tutumike kwa ujasiri,
(You encouraged us with your heart to serve with courage,)
Nawaza naumia, Safari ni ya wote,
(I think and hurt, the journey is for everyone,)
Unaendeleaje..?
(How are you doing?)

Furaha yangu mimi, nione tupo wote,
(My joy, let me see we are all together,)
Safari ni pamoja.
(The journey is together.)

Unaendeleaje..? Unaendeleaje ee?
(How are you doing..? How are you doing... eee..?)
Unaendeleaje na maombi yako kwa Mungu, Unaendeleaje..?
(How are you doing with your prayers to God, how are you doing?)
Unaendeleaje na ibada yako kwa Mungu, Unaendeleaje..?
(How are you doing with your worship to God, how are you doing?)
Unaendeleaje na sadaka zako kwa Mungu, Unaendeleaje..?
(How are you doing with your offerings to God, how are you doing?)
Unaendeleaje na imani yako kwa Mungu, unaendeleaje..?
(How are you doing with your faith in God, how are you doing?)
Unaendeleaje..? Unaendeleaje... eh?
(How are you doing..? How are you doing... eh?)
Unaendeleaje.. eee? Unaendeleaje... eh?
(How are you doing.. eee? How are you doing... eh?)

Unaendeleaje, Unaendeleaje, Mchungaji wangu!
(How are you doing, How are you doing, my Pastor!)
Unaendeleaje, Unaendeleaje, Rafiki yangu!
(How are you doing, How are you doing, my friend!)
Unaendeleaje, Unaendeleaje, mshiriki mwenzangu!
(How are you doing, How are you doing, my fellow member!)
Unaendeleaje, Unaendeleaje, Kiongozi mwenzangu!
(How are you doing, How are you doing, my fellow leader!)

Unaendeleaje ee? Unaendeleaje ee?
(How are you doing... eee!? How are you doing... eh!?)


Zabron Singers - Unaendeleaje(Official video)

Zabron Singers Songs

Related Songs