Sifa Lyrics

Unastahili Kuabudiwa by Upendo Nkone cover art

Upendo Nkone - Unastahili Kuabudiwa Lyrics

Artist:
Upendo Nkone

Lyrics

Spoken Intro
Oh, Haleluya
Tunakusifu Mungu wetu
Wewe umeumba mbingu na nchi
Vile vinavyoonekana na visivyoonekana
Mito, ndege, wanyama na vitu vingi
Ukatuumba wanadamu
Kwa mfano wako wewe Mungu
Umetupa akili na katika hayo
Tunakusifu na kukuinua
Na ndio maana na mimi leo
Ninasema, unastahili eh Bwana
Haleluya.




Verse 1
Mungu wetu tunakusifu
Mungu wetu twakuinua
Yale uyatendayo ni makuu mno
Fadhili zako za milele
Haufananishwi na chochote
Ndiwe uliye mwanzo tena ni mwisho


(Repeated)
Mungu wetu tunakusifu
Mungu wetu twakuinua
Yale uyatendayo ni makuu mno
Fadhili zako za milele
Haufananishwi na chochote
Ndiwe uliye mwanzo tena ni mwisho




Verse 2
Nikiziangalia mbingu
Ni kazi ya mikono yako
Vinavyoonekana na visivyoonekana
Nani kama wewe Mungu wetu
Hatuna wakufanana na wewe
Milele na milele na utadumu




Chorus
Unastahili Yesu kuabudiwa
Unastahili Yesu kuinuliwa
Unastahili Yesu kusujudiwa
Aah-aaaaah, unastahili


(Repeated)
Unastahili Yesu kuabudiwa
Unastahili Yesu kuinuliwa
Unastahili Yesu kusujudiwa
Aah-aaaaah, unastahili




Verse 3
Wewe ni Mungu wa maajabu
Unayetenda mambo makuu
Uwezo wako Mungu ni mkuu sana
Hakuna mwingine kama wewe
Ulitengeneza njia jangwani
Ukawavusha wana wa Israeli
Wewe una nguvu kuliko chochote




Chorus & Outro (with Ad-libs)
Unastahili Yesu kuabudiwa
Unastahili Yesu kuinuliwa
Unastahili Yesu kusujudiwa
Aah-aaaaah, unastahili


(The chorus continues to loop in the background while the lead vocals deliver ad-libbed prayers of worship)


(Ad-libs):
Kule mbinguni...
Maserafi...
Wanakuabudu...
Makerubi wanakuinamia Mungu wetu...
Hakika Mungu wetu utukufu wako...
Hatustahili hata kugusa sehemu ya utukufu huo...
Ndio maana ninasema unastahili sifa Yesu...
Unastahili kuinamiwa Mwokozi...
Unastahili kuadhimishwa milele yote Bwana...
Ni wajibu wangu kukutukuza Mwokozi wangu...
Kwa sababu wewe umeketi mahali pa sifa...
Nani mwingine wa kuabudiwa? Hakuna...
Mbinguni na duniani ni wewe tu Bwana wangu...
Nakupenda Yesu...
Moyo wangu unakuadhimisha Mwokozi wangu...
Haleluya.


Video