Lyrics
Chorus
Usifurahi juu yangu eeeh adui yangu,
niangukapo mimi nitasimama tena.
Kumbuka niwapo gizani bwana nuru yangu,
hawezi kuniacha bwana mimi niangamie.
Verse 1
Si vyema kunisema vibaya nipatapo tatizo,
shetani wampa nafasi ndani ya moyo wako
Kumbuka kwa maombi yako nitasimama tena,
na utapata baraka kutoka kwake Mungu
Verse 2
Maana heri mtu yule ambaye kinywa chake,
huwabariki wenzake na kuwaombea.
Maana maneno mabaya huuchafua moyo.
kukuweka mbali na Mungu ni vema uwe safi.
Verse 3
Ukiona nipo kwenye shida (niombee),
Ndoa yangu imevunjika wewe niombee,
Nikifukuzwa kazini ndugu niombee,
Magonjwa yananiandama niombee,
Biashara haina faida niombee,
Nikikawia kupata mtoto nimbee,
Nimekuwa mtoto yatima niombee,
Hata nijapokuwa mjane niombee,
Refrain
Ujue kwa maombi yako mimi nitasimama tena,
Ujue kwa maombi yako nitabarikiwa,
(x2)
Credits & Song Information
Video
Meaning & Inspiration
“Usifurahi Juu Yangu” is a song of resilience in adversity. The singer answers an enemy’s celebration with confidence that, after falling or passing through darkness, she will rise again through the Lord’s help and prayer.