Zabron Singers - Nitasubiri Lyrics

Nitasubiri Lyrics

Ya nini Mungu kujificha wakati wa shida?
Wakati mwingine kama kweli huoni
Wajua yote yalonikuta hasimliki
Nimelia na kujinyamazisha pekee yangu


Moyoni nikataabika, furaha ikaenda
Sikumwona wa kumwelezea shida
Rafiki pekee namwamini, ni Yesu mfariji
Ndio maana sijamwambia mtu shida zangu


Nitasubiri na kusubiri sitachoka
Nimeshamezana na wewe kwa maombi
Usipojibu, au ujibu nitaelewa
Nashukuru, hata kwa majaribu
Mungu unasababu mimi kuishi maisha kama haya


Nitasubiri na kusubiri sitachoka
Nimeshamezana na wewe kwa maombi
Usipojibu, au ujibu nitaelewa
Nashukuru, hata kwa majaribu
Mungu unasababu mimi kuishi maisha kama haya


Kwa nini sasa umesimama mbali nami Bwana?
Muda mwingi mi najihisi mi ni mpweke
Jidhihirishe mi nikuone, nakuhitaji Bwana
Nibariki sasa ukijibu maombi, yangu


Najua mengi nimekuudhi, nimetenda dhambi
Ndio maana ukasimama mbali nami
Nisamehe yote yote bure, kwa damu ya Yesu
Nifanye mi niwe mtoto wako siku, zote


Nitasubiri na kusubiri sitachoka
Nimeshamezana na wewe kwa maombi
Usipojibu, au ujibu nitaelewa
Nashukuru, hata kwa majaribu
Mungu unasababu mimi kuishi maisha kama haya


Nitasubiri na kusubiri sitachoka
Nimeshamezana na wewe kwa maombi
Usipojibu, au ujibu nitaelewa
Nashukuru, hata kwa majaribu
Mungu unasababu mimi kuishi maisha kama haya


Nitasubiri Video

Zabron Singers Songs

Related Songs