Yeremia 46 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 46 (Swahili) Jeremiah 46 (English)

Neno la Bwana lililomjia Yeremia, nabii, katika habari za mataifa. Yeremia 46:1

The word of Yahweh which came to Jeremiah the prophet concerning the nations.

Katika habari za Misri; habari za jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri, lililokuwa karibu na mto Frati katika Karkemishi, ambalo Nebukadreza, mfalme wa Babeli, alilipiga katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Yeremia 46:2

Of Egypt: concerning the army of Pharaoh Necoh king of Egypt, which was by the river Euphrates in Carchemish, which Nebuchadrezzar king of Babylon struck in the fourth year of Jehoiakim the son of Josiah, king of Judah.

Tengenezeni kigao na ngao, mkakaribie ili kupigana. Yeremia 46:3

Prepare you the buckler and shield, and draw near to battle.

Watandikeni farasi; pandeni, enyi mpandao farasi; simameni na chapeo zenu, isugueni mikuki; zivaeni dirii. Yeremia 46:4

Harness the horses, and get up, you horsemen, and stand forth with your helmets; furbish the spears, put on the coats of mail.

Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjika-vunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu ziko pande zote; asema Bwana. Yeremia 46:5

Why have I seen it? they are dismayed and are turned backward; and their mighty ones are beaten down, and have fled apace, and don't look back: terror is on every side, says Yahweh.

Mtu mwepesi asikimbie, wala shujaa asiokoke; pande za kaskazini karibu na mto Frati wamejikwaa na kuanguka. Yeremia 46:6

Don't let the swift flee away, nor the mighty man escape; in the north by the river Euphrates have they stumbled and fallen.

Nani huyu ajiinuaye kama mto Nile, Ambaye maji yake yanajirusha kama mito? Yeremia 46:7

Who is this who rises up like the Nile, whose waters toss themselves like the rivers?

Misri anajiinua kama mto Nile, Na maji yake yanajirusha kama mito; Asema, Nitajiinua, nitaifunikiza nchi; Nitauharibu mji na hao wakaao ndani yake. Yeremia 46:8

Egypt rises up like the Nile, and his waters toss themselves like the rivers: and he says, I will rise up, I will cover the earth; I will destroy cities and the inhabitants of it.

Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupeta. Yeremia 46:9

Go up, you horses; and rage, you chariots; and let the mighty men go forth: Cush and Put, who handle the shield; and the Ludim, who handle and bend the bow.

Maana hiyo ni siku ya Bwana, Bwana wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, Bwana wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati. Yeremia 46:10

For that day is [a day] of the Lord, Yahweh of Hosts, a day of vengeance, that he may avenge him of his adversaries: and the sword shall devour and be satiate, and shall drink its fill of their blood; for the Lord, Yahweh of hosts, has a sacrifice in the north country by the river Euphrates.

Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe. Yeremia 46:11

Go up into Gilead, and take balm, virgin daughter of Egypt: in vain do you use many medicines; there is no healing for you.

Mataifa wamesikia habari za aibu yako, nayo dunia imejaa kilio chako; maana shujaa amejikwaa juu ya shujaa mwenzake, wameanguka wote wawili pamoja. Yeremia 46:12

The nations have heard of your shame, and the earth is full of your cry; for the mighty man has stumbled against the mighty, they are fallen both of them together.

Neno hili ndilo ambalo Bwana alimwambia Yeremia, nabii, kueleza jinsi Nebukadreza, mfalme wa Babeli, atakavyokuja na kuipiga nchi ya Misri. Yeremia 46:13

The word that Yahweh spoke to Jeremiah the prophet, how that Nebuchadrezzar king of Babylon should come and strike the land of Egypt.

Tangazeni habari hii katika Misri, mkaihubiri katika Migdoli, na kuihubiri katika Nofu, na Tahpanesi; semeni, Simama, ujifanye tayari kwa maana upanga umekula pande zako zote. Yeremia 46:14

Declare you in Egypt, and publish in Migdol, and publish in Memphis and in Tahpanhes: say you, Stand forth, and prepare you; for the sword has devoured round about you.

Mbona mashujaa wako wamechukuliwa mbali? Hawakusimama kwa sababu Bwana aliwafukuza. Yeremia 46:15

Why are your strong ones swept away? they didn't stand, because Yahweh did drive them.

Aliwakwaza wengi, naam, wakaangukiana wao kwa wao; wakasema, Haya! Na tuondoke, tukarudi kwa watu wetu wenyewe, hata nchi tuliyozaliwa, tuukimbie upanga unaotuonea. Yeremia 46:16

He made many to stumble, yes, they fell one on another: and they said, Arise, and let us go again to our own people, and to the land of our birth, from the oppressing sword.

Wakalia huko, Farao, mfalme wa Misri, ni kishindo tu; muhula alioandikiwa ameuacha upite. Yeremia 46:17

They cried there, Pharaoh king of Egypt is but a noise; he has let the appointed time pass by.

Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja. Yeremia 46:18

As I live, says the King, whose name is Yahweh of Hosts, surely like Tabor among the mountains, and like Carmel by the sea, so shall he come.

Ee binti ukaaye katika Misri, Ujiweke tayari kwenda zako hali ya kufungwa; Kwa maana Nofu utakuwa ukiwa, Utateketezwa, usikaliwe na watu. Yeremia 46:19

You daughter who dwell in Egypt, furnish yourself to go into captivity; for Memphis shall become a desolation, and shall be burnt up, without inhabitant.

Misri ni mtamba mzuri sana, lakini uharibifu umekuja, Umekuja utokao pande za kaskazini. Yeremia 46:20

Egypt is a very beautiful heifer; [but] destruction out of the north is come, it is come.

Na watu wake waliojiwa, walio kati yake, Ni kama ndama waliowanda malishoni; Maana wao nao wamerudi nyuma, Wamekimbia wote pamoja, wasisimame; Maana siku ya msiba wao imewafikilia, Wakati wa kujiliwa kwao. Yeremia 46:21

Also her hired men in the midst of her are like calves of the stall; for they also are turned back, they are fled away together, they didn't stand: for the day of their calamity is come on them, the time of their visitation.

Sauti yake ni kama nyoka, wajapo kwa nguvu, Watamjia na mashoka, kama wachanja kuni. Yeremia 46:22

The sound of it shall go like the serpent; for they shall march with an army, and come against her with axes, as wood cutters.

Wataukata msitu wake, asema Bwana, ingawa haupenyeki; Kwa maana ni wengi kuliko nzige, hawahesabiki. Yeremia 46:23

They shall cut down her forest, says Yahweh, though it can't be searched; because they are more than the locusts, and are innumerable.

Binti ya Misri ataaibishwa; Atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini. Yeremia 46:24

The daughter of Egypt shall be disappointed; she shall be delivered into the hand of the people of the north.

Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitamwadhibu Amoni wa No, na Farao, na Misri, pamoja na miungu yake, na wafalme wake, naam, Farao, na hao wanaomtumainia; Yeremia 46:25

Yahweh of Hosts, the God of Israel, says: Behold, I will punish Amon of No, and Pharaoh, and Egypt, with her gods, and her kings; even Pharaoh, and those who trust in him:

nami nitawatia katika mikono ya hao wanaowatafuta roho zao, na katika mikono ya Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya watumishi wake; na baada ya hayo itakaliwa na watu, kama katika siku za kale, asema Bwana. Yeremia 46:26

and I will deliver them into the hand of those who seek their lives, and into the hand of Nebuchadrezzar king of Babylon, and into the hand of his servants; and afterwards it shall be inhabited, as in the days of old, says Yahweh.

Lakini usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu. Yeremia 46:27

But don't be afraid you, Jacob my servant, neither be dismayed, Israel: for, behold, I will save you from afar, and your seed from the land of their captivity; and Jacob shall return, and shall be quiet and at ease, and none shall make him afraid.

Usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema Bwana; kwa maana mimi ni pamoja nawe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokufukuza, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu. Yeremia 46:28

Don't be afraid you, O Jacob my servant, says Yahweh; for I am with you: for I will make a full end of all the nations where I have driven you; but I will not make a full end of you, but I will correct you in measure, and will in no way leave you unpunished.