Yeremia 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 9 (Swahili) Jeremiah 9 (English)

Laiti kichwa changu kingekuwa maji, na macho yangu kuwa chemchemi ya machozi, ili nipate kulia mchana na usiku kwa ajili yao waliouawa wa binti ya watu wangu! Yeremia 9:1

Oh that my head were waters, and my eyes a spring of tears, that I might weep day and night for the slain of the daughter of my people!

Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana. Yeremia 9:2

Oh that I had in the wilderness a lodging-place of wayfaring men; that I might leave my people, and go from them! for they are all adulterers, an assembly of treacherous men.

Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema Bwana. Yeremia 9:3

They bend their tongue, [as it were] their bow, for falsehood; and they are grown strong in the land, but not for truth: for they proceed from evil to evil, and they don't know me, says Yahweh.

Jihadharini, kila mtu na jirani yake, wala msimtumaini ndugu awaye yote; maana kila ndugu atachongea, na kila jirani atakwenda huko na huko na kusingizia. Yeremia 9:4

Take you heed everyone of his neighbor, and don't you trust in any brother; for every brother will utterly supplant, and every neighbor will go about with slanders.

Nao watadanganya kila mtu jirani yake, wala hawatasema kweli; wameuzoeza ulimi wao kusema uongo; hujidhoofisha ili kutenda uovu. Yeremia 9:5

They will deceive everyone his neighbor, and will not speak the truth: they have taught their tongue to speak lies; they weary themselves to commit iniquity.

Makao yako ya katikati ya hadaa; kwa hadaa wanakataa kunijua mimi, asema Bwana. Yeremia 9:6

Your habitation is in the midst of deceit; through deceit they refuse to know me, says Yahweh.

Basi, kwa hiyo Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu; maana nisipotenda hivi, nitende nini kwa ajili ya binti ya watu wangu? Yeremia 9:7

Therefore thus says Yahweh of Hosts, Behold, I will melt them, and try them; for how [else] should I do, because of the daughter of my people?

Ulimi wao ni mshale ufishao; husema maneno ya hadaa; mtu mmoja husema maneno ya amani na mwenzake kwa kinywa chake, lakini moyoni mwake humwotea. Yeremia 9:8

Their tongue is a deadly arrow; it speaks deceit: one speaks peaceably to his neighbor with his mouth, but in his heart he lays wait for him.

Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii? Yeremia 9:9

Shall I not visit them for these things? says Yahweh; shall not my soul be avenged on such a nation as this?

Kwa milima nitalia na kulalama, Na kwa malisho ya nyikani nitafanya maombolezo; Kwa sababu yameteketea, hata hapana apitaye, Wala hapana awezaye kusikia sauti ya ng'ombe; Ndege wa angani, na wanyama wa mwituni, Wamekimbia, wamekwenda zao. Yeremia 9:10

For the mountains will I take up a weeping and wailing, and for the pastures of the wilderness a lamentation, because they are burned up, so that none passes through; neither can men hear the voice of the cattle; both the birds of the sky and the animals are fled, they are gone.

Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu, Makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, Isikaliwe na mtu awaye yote. Yeremia 9:11

I will make Jerusalem heaps, a dwelling-place of jackals; and I will make the cities of Judah a desolation, without inhabitant.

Ni nani aliye na hekima, apate kuelewa na haya? Tena ni nani ambaye kinywa cha Bwana kimesema naye, apate kuyatangaza? Nayo ni nini maana yake nchi hii kuharibika, na kuteketea kama nyika, asipite mtu? Yeremia 9:12

Who is the wise man, that may understand this? and [who is] he to whom the mouth of Yahweh has spoken, that he may declare it? why is the land perished and burned up like a wilderness, so that none passes through?

Naye Bwana asema, Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu niliyoweka mbele yao, wala hawakuitii sauti yangu, wala kuenenda katika hiyo; Yeremia 9:13

Yahweh says, Because they have forsaken my law which I set before them, and have not obeyed my voice, neither walked therein,

bali wameenenda katika ushupavu wa mioyo yao wenyewe, na kuandamana na Mabaali, kama walivyofundishwa na baba zao. Yeremia 9:14

but have walked after the stubbornness of their own heart, and after the Baals, which their fathers taught them;

Basi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitawalisha pakanga, naam, watu hawa, nami nitawapa maji ya uchungu wayanywe. Yeremia 9:15

therefore thus says Yahweh of Hosts, the God of Israel, Behold, I will feed them, even this people, with wormwood, and give them water of gall to drink.

Nami nitawatawanya kati ya mataifa, ambao wao hawakuwajua; wala baba zao, nami nitatuma upanga nyuma yao, hata nitakapowaangamiza kabisa. Yeremia 9:16

I will scatter them also among the nations, whom neither they nor their fathers have known; and I will send the sword after them, until I have consumed them.

Bwana wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje; Yeremia 9:17

Thus says Yahweh of Hosts, Consider you, and call for the mourning women, that they may come; and send for the skillful women, that they may come:

na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji. Yeremia 9:18

and let them make haste, and take up a wailing for us, that our eyes may run down with tears, and our eyelids gush out with waters.

Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu. Yeremia 9:19

For a voice of wailing is heard out of Zion, How are we ruined! we are greatly confounded, because we have forsaken the land, because they have cast down our dwellings.

Lakini lisikieni neno la Bwana, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia. Yeremia 9:20

Yet hear the word of Yahweh, you women, and let your ear receive the word of his mouth; and teach your daughters wailing, and everyone her neighbor lamentation.

Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu. Yeremia 9:21

For death is come up into our windows, it is entered into our palaces; to cut off the children from outside, [and] the young men from the streets.

Nena, Bwana asema hivi, Mizoga ya watu itaanguka kama samadi juu ya mashamba, Na kama konzi ya ngano nyuma yake avunaye, wala hapana mtu atakayeikusanya. Yeremia 9:22

Speak, Thus says Yahweh, The dead bodies of men shall fall as dung on the open field, and as the handful after the harvester; and none shall gather [them].

Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; Yeremia 9:23

Thus says Yahweh, Don't let the wise man glory in his wisdom, neither let the mighty man glory in his might, don't let the rich man glory in his riches;

bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana, Yeremia 9:24

but let him who glories glory in this, that he has understanding, and knows me, that I am Yahweh who exercises loving kindness, justice, and righteousness, in the earth: for in these things I delight, says Yahweh.

Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapowaadhibu wote waliotahiriwa katika hali yao ya kutokutahiriwa; Yeremia 9:25

Behold, the days come, says Yahweh, that I will punish all those who are circumcised in [their] uncircumcision:

Misri, na Yuda, na Edomu, na wana wa Amoni, na Moabu, na wote wenye kunyoa denge, wakaao nyikani; maana mataifa hayo yote hawana tohara, wala nyumba yote ya Israeli hawakutahiriwa mioyo yao. Yeremia 9:26

Egypt, and Judah, and Edom, and the children of Ammon, and Moab, and all that have the corners [of their hair] cut off, who dwell in the wilderness; for all the nations are uncircumcised, and all the house of Israel are uncircumcised in heart.