Yeremia 26 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 26 (Swahili) Jeremiah 26 (English)

Mwanzo wa kumiliki kwake Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hili lilitoka kwa Bwana, kusema, Yeremia 26:1

In the beginning of the reign of Jehoiakim the son of Josiah, king of Judah, came this word from Yahweh, saying,

Bwana asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya Bwana, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya Bwana; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja. Yeremia 26:2

Thus says Yahweh: Stand in the court of Yahweh's house, and speak to all the cities of Judah, which come to worship in Yahweh's house, all the words that I command you to speak to them; don't diminish a word.

Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu njia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya uovu wa matendo yao. Yeremia 26:3

It may be they will listen, and turn every man from his evil way; that I may repent me of the evil which I purpose to do to them because of the evil of their doings.

Nawe utawaambia, Bwana asema hivi, Kama hamtaki kunisikia, kwenda katika sheria yangu, niliyoiweka mbele yenu, Yeremia 26:4

You shall tell them, Thus says Yahweh: If you will not listen to me, to walk in my law, which I have set before you,

kuyasikiliza maneno ya watumishi wangu, manabii, ninaowatuma kwenu, naam, nikiondoka mapema na kuwatuma; lakini ninyi hamkuwasikiliza; Yeremia 26:5

to listen to the words of my servants the prophets, whom I send to you, even rising up early and sending them, but you have not listened;

basi, nitafanya nyumba hii kuwa kama Shilo, na mji huu nitaufanya kuwa laana kwa taifa zote za dunia. Yeremia 26:6

then will I make this house like Shiloh, and will make this city a curse to all the nations of the earth.

Na makuhani, na manabii, na watu wote, wakamsikia Yeremia, hapo aliposema maneno haya katika nyumba ya Bwana. Yeremia 26:7

The priests and the prophets and all the people heard Jeremiah speaking these words in the house of Yahweh.

Ikawa, Yeremia alipokuwa amekwisha kusema maneno yote Bwana aliyomwamuru kuwaambia watu wote, ndipo hao makuhani, na manabii, na watu wote, wakamkamata, wakisema, Bila shaka utakufa. Yeremia 26:8

It happened, when Jeremiah had made an end of speaking all that Yahweh had commanded him to speak to all the people, that the priests and the prophets and all the people laid hold on him, saying, You shall surely die.

Kwa nini umetabiri kwa jina la Bwana, ukisema, Nyumba hii itakuwa kama Shilo, na mji huu utakuwa ukiwa, hautakaliwa na mtu? Watu wote wakamkusanyikia Yeremia katika nyumba ya Bwana. Yeremia 26:9

Why have you prophesied in the name of Yahweh, saying, This house shall be like Shiloh, and this city shall be desolate, without inhabitant? All the people were gathered to Jeremiah in the house of Yahweh.

Na wakuu wa Yuda waliposikia habari za mambo haya, wakatoka katika nyumba ya mfalme, wakapanda juu mpaka nyumbani kwa Bwana; wakaketi, hapo watu waingiapo katika lango jipya la nyumba ya Bwana. Yeremia 26:10

When the princes of Judah heard these things, they came up from the king's house to the house of Yahweh; and they sat in the entry of the new gate of Yahweh's [house].

Ndipo hapo makuhani, na manabii, wakawaambia wakuu na watu wote, wakisema, Mtu huyu amestahili kufa, kwa sababu ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu. Yeremia 26:11

Then spoke the priests and the prophets to the princes and to all the people, saying, This man is worthy of death; for he has prophesied against this city, as you have heard with your ears.

Ndipo Yeremia akawaambia wakuu wote na watu wote, akisema, Bwana ndiye aliyenituma kutabiri juu ya nyumba hii, na juu ya mji huu, maneno hayo yote mliyoyasikia. Yeremia 26:12

Then spoke Jeremiah to all the princes and to all the people, saying, Yahweh sent me to prophesy against this house and against this city all the words that you have heard.

Basi sasa, tengenezeni njia zenu, na matendo yenu, mkaisikilize sauti ya Bwana, Mungu wenu; naye Bwana atayaghairi mabaya aliyoyanena juu yenu. Yeremia 26:13

Now therefore amend your ways and your doings, and obey the voice of Yahweh your God; and Yahweh will repent him of the evil that he has pronounced against you.

Lakini kwangu mimi, tazama, mimi nipo hapa mikononi mwenu; nitendeni myaonayo kuwa mema na haki mbele ya macho yenu. Yeremia 26:14

But as for me, behold, I am in your hand: do with me as is good and right in your eyes.

Lakini jueni yakini ya kuwa, mkiniua, mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake; kwa maana ni kweli Bwana amenituma kwenu, kuwaambieni yote mliyoyasikia. Yeremia 26:15

Only know for certain that, if you put me to death, you will bring innocent blood on yourselves, and on this city, and on the inhabitants of it; for of a truth Yahweh has sent me to you to speak all these words in your ears.

Ndipo wakuu na watu wote wakawaambia makuhani, na manabii, wakisema, Mtu huyu hastahili kuuawa; kwa maana amesema nasi katika jina la Bwana Mungu wetu. Yeremia 26:16

Then said the princes and all the people to the priests and to the prophets: This man is not worthy of death; for he has spoken to us in the name of Yahweh our God.

Ndipo watu kadha wa kadha miongoni mwa wazee wa nchi wakaondoka, wakanena na mkutano wa watu, wakisema, Yeremia 26:17

Then rose up certain of the elders of the land, and spoke to all the assembly of the people, saying,

Mikaya Mmorashti, alitabiri katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda; akasema na watu wote wa Yuda, ya kwamba, Bwana wa majeshi asema hivi, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu, na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni. Yeremia 26:18

Micah the Morashtite prophesied in the days of Hezekiah king of Judah; and he spoke to all the people of Judah, saying, Thus says Yahweh of Hosts: Zion shall be plowed as a field, and Jerusalem shall become heaps, and the mountain of the house as the high places of a forest.

Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! Hakumcha Bwana, na kumwomba Bwana awafadhili; naye Bwana akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Na sisi tungetenda mabaya makuu juu ya roho zetu. Yeremia 26:19

Did Hezekiah king of Judah and all Judah put him to death? Didn't he fear Yahweh, and entreat the favor of Yahweh, and Yahweh repented him of the evil which he had pronounced against them? Thus should we commit great evil against our own souls.

Tena, kulikuwa na mtu aliyetabiri katika jina la Bwana, Uria, mwana wa Shemaya, wa Kiriath-Yearimu; yeye naye alitabiri juu ya mji huu, na juu ya nchi hii, sawasawa na maneno yote ya Yeremia; Yeremia 26:20

There was also a man who prophesied in the name of Yahweh, Uriah the son of Shemaiah of Kiriath Jearim; and he prophesied against this city and against this land according to all the words of Jeremiah:

na Yehoyakimu, mfalme, na mashujaa wake wote, na wakuu wake wote, waliposikia maneno yake, mfalme akataka kumwua; lakini Uria alipopata habari, aliogopa, akakimbia akaenda Misri. Yeremia 26:21

and when Jehoiakim the king, with all his mighty-men, and all the princes, heard his words, the king sought to put him to death; but when Uriah heard it, he was afraid, and fled, and went into Egypt:

Basi, mfalme Yehoyakimu akatuma watu waende Misri, Elnathani, mwana wa Akbori, na watu wengine pamoja naye, kwenda Misri; Yeremia 26:22

and Jehoiakim the king sent men into Egypt, [namely], Elnathan the son of Achbor, and certain men with him, into Egypt;

wakamtoa Uria katika Misri, wakamleta kwa Yehoyakimu, mfalme; naye akamwua kwa upanga, akamtupa yule maiti katika makaburi ya watu wasio na cheo. Yeremia 26:23

and they fetched forth Uriah out of Egypt, and brought him to Jehoiakim the king, who killed him with the sword, and cast his dead body into the graves of the common people.

Lakini mkono wa Ahikamu, mwana wa Shafani, alikuwa pamoja na Yeremia, wasimtie katika mikono ya watu auawe. Yeremia 26:24

But the hand of Ahikam the son of Shaphan was with Jeremiah, that they should not give him into the hand of the people to put him to death.