Yeremia 38 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yeremia 38 (Swahili) Jeremiah 38 (English)

Na Shefatia, mwana wa Matani, na Gedalia, mwana wa Pashuri, na Yukali, mwana wa Shelemia, na Pashuri, mwana wa Malkiya, wakayasikia maneno ambayo Yeremia aliwaambia watu wote, kusema, Yeremia 38:1

Shephatiah the son of Mattan, and Gedaliah the son of Pashhur, and Jucal the son of Shelemiah, and Pashhur the son of Malchijah, heard the words that Jeremiah spoke to all the people, saying,

Bwana asema hivi, Akaaye ndani ya mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atokaye kwenda kwa Wakaldayo ataishi, naye atapewa maisha yake yawe kama nyara, naye ataishi. Yeremia 38:2

Thus says Yahweh, He who remains in this city shall die by the sword, by the famine, and by the pestilence; but he who goes forth to the Chaldeans shall live, and his life shall be to him for a prey, and he shall live.

Bwana asema hivi, Bila shaka mji huu utatiwa katika mikono ya jeshi la mfalme wa Babeli, naye atautwaa. Yeremia 38:3

Thus says Yahweh, This city shall surely be given into the hand of the army of the king of Babylon, and he shall take it.

Ndipo wakuu wakamwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu, na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno kama hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri, bali shari. Yeremia 38:4

Then the princes said to the king, Let this man, we pray you, be put to death; because he weakens the hands of the men of war who remain in this city, and the hands of all the people, in speaking such words to them: for this man doesn't seek the welfare of this people, but the hurt.

Naye mfalme Sedekia akasema, Tazama, yu mikononi mwenu; maana mfalme siye awezaye kufanya neno lo lote kinyume chenu. Yeremia 38:5

Zedekiah the king said, Behold, he is in your hand; for the king is not he who can do anything against you.

Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo. Yeremia 38:6

Then took they Jeremiah, and cast him into the dungeon of Malchijah the king's son, that was in the court of the guard: and they let down Jeremiah with cords. In the dungeon there was no water, but mire; and Jeremiah sank in the mire.

Basi, Ebedmeleki, Mkushi, towashi, aliyekuwa katika nyumba ya mfalme, aliposikia kama wamemtia Yeremia shimoni; na wakati huo mfalme alikuwa amekaa katika lango la Benyamini; Yeremia 38:7

Now when Ebedmelech the Ethiopian, a eunuch, who was in the king's house, heard that they had put Jeremiah in the dungeon (the king then sitting in the gate of Benjamin),

Ebedmeleki akatoka nyumbani mwa mfalme, akamwambia mfalme, akisema, Yeremia 38:8

Ebedmelech went forth out of the king's house, and spoke to the king, saying,

Ee bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hapana mkate kabisa katika mji. Yeremia 38:9

My lord the king, these men have done evil in all that they have done to Jeremiah the prophet, whom they have cast into the dungeon; and he is likely to die in the place where he is, because of the famine; for there is no more bread in the city.

Ndipo mfalme akamwamuru Ebedmeleki, Mkushi, akisema, Chukua pamoja nawe watu thelathini toka hapa, ukamtoe Yeremia shimoni, kabla hajafa. Yeremia 38:10

Then the king commanded Ebedmelech the Ethiopian, saying, Take from hence thirty men with you, and take up Jeremiah the prophet out of the dungeon, before he die.

Basi Ebedmeleki akawachukua watu hao pamoja naye, akaingia ndani ya nyumba ya mfalme chini ya ghala, akatoa mle nguo zilizotupwa, na vitambaa vikuukuu, akamtelemshia Yeremia shimoni kwa kamba. Yeremia 38:11

So Ebedmelech took the men with him, and went into the house of the king under the treasury, and took there rags and worn-out garments, and let them down by cords into the dungeon to Jeremiah.

Naye Ebedmeleki, Mkushi, akamwambia Yeremia, Tia nguo hizi zilizotupwa, na vitambaa hivi vikuukuu, chini ya kamba kwapani. Naye Yeremia akafanya hivyo. Yeremia 38:12

Ebedmelech the Ethiopian said to Jeremiah, Put now these rags and worn-out garments under your armholes under the cords. Jeremiah did so.

Basi wakamwinua Yeremia kwa kamba hizo, wakamtoa shimoni; naye Yeremia akakaa katika uwanda wa walinzi. Yeremia 38:13

So they drew up Jeremiah with the cords, and took him up out of the dungeon: and Jeremiah remained in the court of the guard.

Kisha mfalme Sedekia akatuma watu, akamleta nabii Yeremia kwake, ndani ya maingilio ya tatu ya nyumba ya Bwana; mfalme akamwambia Yeremia, Nataka kukuuliza neno, nawe usinifiche neno lo lote. Yeremia 38:14

Then Zedekiah the king sent, and took Jeremiah the prophet to him into the third entry that is in the house of Yahweh: and the king said to Jeremiah, I will ask you a thing; hide nothing from me.

Basi Yeremia akamwambia Sedekia, Kama nikikufunulia neno hilo, je! Hutaniua wewe? Tena, mimi nikikupa shauri wewe hutanisikiliza. Yeremia 38:15

Then Jeremiah said to Zedekiah, If I declare it to you, will you not surely put me to death? and if I give you counsel, you will not listen to me.

Basi Sedekia mfalme akamwapia Yeremia kwa siri, akisema, Kama Bwana aishivyo, yeye aliyetufanyia roho zetu, sitakuua, wala sitakutia katika mikono ya watu hao wanaokutafuta wakuue. Yeremia 38:16

So Zedekiah the king swore secretly to Jeremiah, saying, As Yahweh lives, who made us this soul, I will not put you to death, neither will I give you into the hand of these men who seek your life.

Ndipo Yeremia akamwambia Sedekia, Bwana, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama ukitoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi nafsi yako utaishi, wala mji huu hautateketezwa; nawe utaishi na nyumba yako; Yeremia 38:17

Then said Jeremiah to Zedekiah, Thus says Yahweh, the God of hosts, the God of Israel: If you will go forth to the king of Babylon's princes, then your soul shall live, and this city shall not be burned with fire; and you shall live, and your house.

bali ukikataa kutoka kwenda kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, basi, mji huu utatiwa katika mikono ya Wakaldayo nao watauteketeza, hata na wewe hutajiepusha na mikono yao. Yeremia 38:18

But if you will not go forth to the king of Babylon's princes, then shall this city be given into the hand of the Chaldeans, and they shall burn it with fire, and you shall not escape out of their hand.

Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia, Nawaogopa Wayahudi waliowakimbilia Wakaldayo, wasije wakanitia katika mikono yao, nao wakanidhihaki. Yeremia 38:19

Zedekiah the king said to Jeremiah, I am afraid of the Jews who are fallen away to the Chaldeans, lest they deliver me into their hand, and they mock me.

Lakini Yeremia akasema, La! Hawatakutoa. Nakusihi, uitii sauti ya Bwana katika hayo ninayokuambia; ndivyo itakavyokufaa, na nafsi yako utaishi. Yeremia 38:20

But Jeremiah said, They shall not deliver you. Obey, I beg you, the voice of Yahweh, in that which I speak to you: so it shall be well with you, and your soul shall live.

Lakini kama ukikataa kutoka, hili ndilo neno ambalo Bwana amenionyesha; Yeremia 38:21

But if you refuse to go forth, this is the word that Yahweh has shown me:

Tazama, wanawake wote, walioachwa ndani ya nyumba ya mfalme wa Yuda, watatolewa na kuchukuliwa kwa wakuu wa mfalme wa Babeli, na wanawake hao watasema, Rafiki zako walio karibu wamekudanganya, nao wamekushinda; na kwa kuwa miguu yako imezama matopeni sasa, wamegeuka na kurudi nyuma. Yeremia 38:22

behold, all the women who are left in the king of Judah's house shall be brought forth to the king of Babylon's princes, and those women shall say, Your familiar friends have set you on, and have prevailed over you: [now that] your feet are sunk in the mire, they are turned away back.

Na watawatoa wake zako, na watoto wako wote, na kuwachukua kwa Wakaldayo; wala wewe hutapona na mikono yao, bali utakamatwa kwa mkono wa mfalme wa Babeli, nawe utakuwa sababu ya kuteketezwa mji huu. Yeremia 38:23

They shall bring out all your wives and your children to the Chaldeans; and you shall not escape out of their hand, but shall be taken by the hand of the king of Babylon: and you shall cause this city to be burned with fire.

Ndipo Sedekia akamwambia Yeremia, Mtu ye yote asipate habari ya maneno haya, nawe hutakufa. Yeremia 38:24

Then said Zedekiah to Jeremiah, Let no man know of these words, and you shall not die.

Lakini kama wakuu wakisikia ya kuwa nimenena nawe, nao wakija kwako, na kukuambia, Tufunulie sasa uliyomwambia mfalme; usimfiche, nasi hatutakuua; na pia uliyoambiwa na mfalme; Yeremia 38:25

But if the princes hear that I have talked with you, and they come to you, and tell you, Declare to us now what you have said to the king; don't hide it from us, and we will not put you to death; also what the king said to you:

basi, utawaambia, Nalimwomba mfalme asinirudishe nyumbani kwa Yonathani, nisije nikafa humo. Yeremia 38:26

then you shall tell them, I presented my supplication before the king, that he would not cause me to return to Jonathan's house, to die there.

Ndipo wakuu wakamwendea Yeremia, wakamwuliza; naye akawaambia sawasawa na maneno aliyoamriwa na mfalme. Basi wakaacha kunena naye; maana neno lile halikujulikana. Yeremia 38:27

Then came all the princes to Jeremiah, and asked him; and he told them according to all these words that the king had commanded. So they left off speaking with him; for the matter was not perceived.

Basi Yeremia akakaa katika uwanda wa walinzi hata siku ile Yerusalemu ulipotwaliwa. Yeremia 38:28

So Jeremiah abode in the court of the guard until the day that Jerusalem was taken.