Kutoka 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 7 (Swahili) Exodus 7 (English)

Bwana akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruni atakuwa nabii wako. Kutoka 7:1

Yahweh said to Moses, "Behold, I have made you as God to Pharaoh; and Aaron your brother shall be your prophet.

Utanena hayo yote nikuagizayo; na ndugu yako Haruni atanena na Farao, ili awape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake. Kutoka 7:2

You shall speak all that I command you; and Aaron your brother shall speak to Pharaoh, that he let the children of Israel go out of his land.

Nami nitaufanya mgumu moyo wa Farao, nami nitazifanya kuwa nyingi ishara zangu na ajabu zangu katika nchi ya Misri. Kutoka 7:3

I will harden Pharaoh's heart, and multiply my signs and my wonders in the land of Egypt.

Lakini Farao hatawasikiza ninyi, nami nitaweka mkono wangu juu ya Misri, na kuyatoa majeshi yangu, watu wangu, hao wana wa Israeli, watoke nchi ya Misri kwa hukumu zilizo kuu. Kutoka 7:4

But Pharaoh will not listen to you, and I will lay my hand on Egypt, and bring forth my hosts, my people the children of Israel, out of the land of Egypt by great judgments.

Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, hapo nitakapounyosha mkono wangu juu ya Misri na kuwatoa wana wa Israeli watoke kati yao. Kutoka 7:5

The Egyptians shall know that I am Yahweh, when I stretch forth my hand on Egypt, and bring out the children of Israel from among them."

Musa na Haruni wakafanya vivyo; kama Bwana alivyowaambia, ndivyo walivyofanya. Kutoka 7:6

Moses and Aaron did so. As Yahweh commanded them, so they did.

Huyo Musa alikuwa ni mtu wa miaka themanini umri wake, na Haruni alikuwa ni mtu wa miaka themanini na mitatu, hapo waliponena na Farao. Kutoka 7:7

Moses was eighty years old, and Aaron eighty-three years old, when they spoke to Pharaoh.

Bwana akanena na Musa na Haruni, akawaambia, Kutoka 7:8

Yahweh spoke to Moses and to Aaron, saying,

Farao atakaponena nanyi, na kuwaambia, Jifanyieni miujiza; ndipo utakapomwambia Haruni, Shika fimbo yako, uibwage chini mbele ya Farao, ili iwe nyoka. Kutoka 7:9

"When Pharaoh speaks to you, saying, 'Perform a miracle!' then you shall tell Aaron, 'Take your rod, and cast it down before Pharaoh, that it become a serpent.'"

Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama Bwana alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka. Kutoka 7:10

Moses and Aaron went in to Pharaoh, and they did so, as Yahweh had commanded: and Aaron cast down his rod before Pharaoh and before his servants, and it became a serpent.

Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao. Kutoka 7:11

Then Pharaoh also called for the wise men and the sorcerers. They also, the magicians of Egypt, did in like manner with their enchantments.

Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao. Kutoka 7:12

For they cast down every man his rod, and they became serpents: but Aaron's rod swallowed up their rods.

Moyo wa Farao ukawa ni mgumu asiwasikize; kama Bwana alivyonena. Kutoka 7:13

Pharaoh's heart was hardened, and he didn't listen to them; as Yahweh had spoken.

Bwana akamwambia Musa, Moyo wa Farao ni mzito, anakataa kuwapa watu ruhusa waende zao. Kutoka 7:14

Yahweh said to Moses, "Pharaoh's heart is stubborn. He refuses to let the people go.

Mwendee Farao asubuhi; tazama, atoka kwenda majini; nawe simama karibu na ufuo wa mto ili upate kuonana naye; na ile fimbo iliyogeuzwa kuwa nyoka utaichukua mkononi mwako. Kutoka 7:15

Go to Pharaoh in the morning. Behold, he goes out to the water; and you shall stand by the river's bank to meet him; and the rod which was turned to a serpent you shall take in your hand.

Nawe umwambie, Bwana, Mungu wa Waebrania, amenituma nije kwako, kusema, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate kunitumikia jangwani; nawe, tazama! Hujasikia hata sasa. Kutoka 7:16

You shall tell him, 'Yahweh, the God of the Hebrews, has sent me to you, saying, "Let my people go, that they may serve me in the wilderness:" and, behold, until now you haven't listened.

Bwana asema, Katika jambo hili utanijua ya kuwa mimi ndimi Bwana; tazama, nitayapiga haya maji yaliyo mtoni kwa fimbo hii niliyo nayo mkononi mwangu, nayo yatageuzwa kuwa damu. Kutoka 7:17

Thus says Yahweh, "In this you shall know that I am Yahweh. Behold, I will strike with the rod that is in my hand on the waters which are in the river, and they shall be turned to blood.

Na hao samaki walio mtoni watakufa, na huo mto utatoa uvundo; nao Wamisri watachukizwa kuyanywa maji ya mtoni. Kutoka 7:18

The fish that are in the river shall die, and the river shall become foul; and the Egyptians shall loathe to drink water from the river."'"

Bwana akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Shika fimbo yako, kaunyoshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya mito yao, juu ya vijito vyao, na juu ya maziwa ya maji yao, na juu ya visima vyao vyote vya maji, ili yageuke kuwa damu, nako kutakuwa na damu katika nchi yote ya Misri, katika vyombo vya mti, na katika vyombo vya jiwe. Kutoka 7:19

Yahweh said to Moses, "Tell Aaron, 'Take your rod, and stretch out your hand over the waters of Egypt, over their rivers, over their streams, and over their pools, and over all their ponds of water, that they may become blood; and there shall be blood throughout all the land of Egypt, both in vessels of wood and in vessels of stone.'"

Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama Bwana alivyowaambia; naye akaiinua ile fimbo, na kuyapiga maji yaliyokuwa mtoni, mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake; na hayo maji yote yaliyokuwa katika mto yakageuzwa kuwa damu. Kutoka 7:20

Moses and Aaron did so, as Yahweh commanded; and he lifted up the rod, and struck the waters that were in the river, in the sight of Pharaoh, and in the sight of his servants; and all the waters that were in the river were turned to blood.

Hao samaki waliokuwa mtoni nao wakafa; na ule mto ukatoa uvundo, Wamisri wasipate kunywa maji ya mtoni; na ile damu ilikuwa katika nchi yote na Misri. Kutoka 7:21

The fish that were in the river died; and the river became foul, and the Egyptians couldn't drink water from the river; and the blood was throughout all the land of Egypt.

Lakini waganga wa Misri wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao; na moyo wake Farao ukawa mgumu, wala hakuwasikiza, kama Bwana alivyonena. Kutoka 7:22

The magicians of Egypt did in like manner with their enchantments; and Pharaoh's heart was hardened, and he didn't listen to them; as Yahweh had spoken.

Farao akazunguka na kuingia nyumbani mwake, wala hata hilo hakuliweka moyoni. Kutoka 7:23

Pharaoh turned and went into his house, neither did he lay even this to heart.

Wamisri wote wakachimba-chimba kando ya mto ili wapate maji ya kunywa; maana, hawakuweza kuyanywa yale maji ya mtoni. Kutoka 7:24

All the Egyptians dug round about the river for water to drink; for they couldn't drink of the water of the river.

Zikatimia siku saba, baada ya Bwana kuupiga ule mto.

Kutoka 7:25

Seven days were fulfilled, after Yahweh had struck the river.