Kutoka 31 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 31 (Swahili) Exodus 31 (English)

Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Kutoka 31:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; Kutoka 31:2

"Behold, I have called by name Bezalel the son of Uri, the son of Hur, of the tribe of Judah:

nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, Kutoka 31:3

and I have filled him with the Spirit of God, in wisdom, and in understanding, and in knowledge, and in all manner of workmanship,

ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, Kutoka 31:4

to devise skillful works, to work in gold, and in silver, and in brass,

na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote. Kutoka 31:5

and in cutting of stones for setting, and in carving of wood, to work in all manner of workmanship.

Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza; Kutoka 31:6

I, behold, I have appointed with him Oholiab, the son of Ahisamach, of the tribe of Dan; and in the heart of all who are wise-hearted I have put wisdom, that they may make all that I have commanded you:

yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema; Kutoka 31:7

the tent of meeting, the ark of the testimony, the mercy seat that is on it, all the furniture of the Tent,

na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba; Kutoka 31:8

the table and its vessels, the pure lampstand with all its vessels, the altar of incense,

na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake; Kutoka 31:9

the altar of burnt offering with all its vessels, the basin and its base,

na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani; Kutoka 31:10

the finely worked garments--the holy garments for Aaron the priest--the garments of his sons to minister in the priest's office,

na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao. Kutoka 31:11

the anointing oil, and the incense of sweet spices for the holy place: according to all that I have commanded you they shall do."

Bwana akasema na Musa, na kumwambia, Kutoka 31:12

Yahweh spoke to Moses, saying,

Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi. Kutoka 31:13

"Speak also to the children of Israel, saying, 'Most assuredly you shall keep my Sabbaths: for it is a sign between me and you throughout your generations; that you may know that I am Yahweh who sanctifies you.

Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake. Kutoka 31:14

You shall keep the Sabbath therefore; for it is holy to you. Everyone who profanes it shall surely be put to death; for whoever does any work therein, that soul shall be cut off from among his people.

Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa Bwana; kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake atauawa. Kutoka 31:15

Six days shall work be done, but on the seventh day is a Sabbath of solemn rest, holy to Yahweh. Whoever does any work on the Sabbath day shall surely be put to death.

Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. Kutoka 31:16

Therefore the children of Israel shall keep the Sabbath, to observe the Sabbath throughout their generations, for a perpetual covenant.

Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika. Kutoka 31:17

It is a sign between me and the children of Israel forever; for in six days Yahweh made heaven and earth, and on the seventh day he rested, and was refreshed.'"

Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu. Kutoka 31:18

He gave to Moses, when he finished speaking with him on Mount Sinai, the two tablets of the testimony, stone tablets, written with God's finger.