Kutoka 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 19 (Swahili) Exodus 19 (English)

Mwezi wa tatu baada ya kutoka Waisraeli katika nchi ya Misri, siku iyo hiyo wakafika jangwa la Sinai. Kutoka 19:1

In the third month after the children of Israel had gone forth out of the land of Egypt, on that same day they came into the wilderness of Sinai.

Nao walipokuwa wameondoka Refidimu na kufika jangwa la Sinai, wakatua katika lile jangwa; Israeli wakapiga kambi huko wakiukabili mlima. Kutoka 19:2

When they had departed from Rephidim, and had come to the wilderness of Sinai, they encamped in the wilderness; and there Israel encamped before the mountain.

Musa akapanda kwa Mungu, na Bwana akamwita toka mlima ule, akisema, Utawaambia nyumba ya Yakobo, na kuwaarifu wana wa Israeli, maneno haya; Kutoka 19:3

Moses went up to God, and Yahweh called to him out of the mountain, saying, "This is what you shall tell the house of Jacob, and tell the children of Israel:

Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. Kutoka 19:4

'You have seen what I did to the Egyptians, and how I bore you on eagles' wings, and brought you to myself.

Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, Kutoka 19:5

Now therefore, if you will indeed obey my voice, and keep my covenant, then you shall be my own possession from among all peoples; for all the earth is mine;

nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli. Kutoka 19:6

and you shall be to me a kingdom of priests, and a holy nation.' These are the words which you shall speak to the children of Israel."

Musa akaenda akawaita wazee wa watu, akawafunulia maneno hayo yote, Bwana aliyokuwa amemwagiza. Kutoka 19:7

Moses came and called for the elders of the people, and set before them all these words which Yahweh commanded him.

Watu wote wakaitika pamoja wakisema, Hayo yote aliyoyasema Bwana tutayatenda. Naye Musa akamwambia Bwana maneno ya hao watu. Kutoka 19:8

All the people answered together, and said, "All that Yahweh has spoken we will do." Moses reported the words of the people to Yahweh.

Bwana akamwambia Musa, Tazama, mimi naja kwako katika wingu zito ili watu hawa wasikie nitakaposema nawe, nao wapate kukuamini wewe nawe hata milele. Musa akamwambia Bwana hayo maneno ya watu. Kutoka 19:9

Yahweh said to Moses, "Behold, I come to you in a thick cloud, that the people may hear when I speak with you, and may also believe you forever." Moses told the words of the people to Yahweh.

Bwana akamwambia Musa, Enenda kwa watu hawa, ukawatakase leo na kesho, wakazifue nguo zao, Kutoka 19:10

Yahweh said to Moses, "Go to the people, and sanctify them today and tomorrow, and let them wash their garments,

wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu Bwana atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote. Kutoka 19:11

and be ready against the third day; for on the third day Yahweh will come down in the sight of all the people on Mount Sinai.

Nawe utawawekea mipaka watu hawa pande zote, ukisema, Jihadharini, msipande mlima huu, wala msiuguse, hata mapambizo yake; kila mtu atakayeugusa mlima huu, bila shaka atauawa. Kutoka 19:12

You shall set bounds to the people round about, saying, 'Be careful that you don't go up onto the mountain, or touch its border. Whoever touches the mountain shall be surely put to death.

Mkono wa mtu awaye yote usimguse mtu huyo, ila hakika yake atapigwa kwa mawe, au kupigwa kwa mkuki; kwamba ni mnyama au kwamba ni mwanadamu, hataishi. Hapo panda itakapotoa sauti kwa kufuliza ndipo watakapoukaribia mlima. Kutoka 19:13

No hand shall touch him, but he shall surely be stoned or shot through; whether it is animal or man, he shall not live.' When the trumpet sounds long, they shall come up to the mountain."

Musa akatelemka mlimani akawaendea watu akawatakasa, nao wakafua nguo zao. Kutoka 19:14

Moses went down from the mountain to the people, and sanctified the people; and they washed their clothes.

Akawaambia watu; Mwe tayari siku ya tatu; msimkaribie mwanamke. Kutoka 19:15

He said to the people, "Be ready by the third day. Don't have sexual relations with a woman."

Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka. Kutoka 19:16

It happened on the third day, when it was morning, that there were thunders and lightnings, and a thick cloud on the mountain, and the sound of an exceedingly loud trumpet; and all the people who were in the camp trembled.

Musa akawatoa hao watu katika kituo, akawaleta ili waonane na Mungu; wakasimama pande za chini za kile kilima. Kutoka 19:17

Moses led the people out of the camp to meet God; and they stood at the lower part of the mountain.

Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu Bwana alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuu, mlima wote ukatetemeka sana. Kutoka 19:18

Mount Sinai, the whole of it, smoked, because Yahweh descended on it in fire; and its smoke ascended like the smoke of a furnace, and the whole mountain quaked greatly.

Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti. Kutoka 19:19

When the sound of the trumpet grew louder and louder, Moses spoke, and God answered him by a voice.

Bwana akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu. Kutoka 19:20

Yahweh came down on Mount Sinai, to the top of the mountain. Yahweh called Moses to the top of the mountain, and Moses went up.

Ndipo Bwana akamwambia Musa, Shuka chini, uwaonye watu wasije wakapasua njia waje kwa Bwana kutazama, kisha wengi miongoni mwao wakaangamia. Kutoka 19:21

Yahweh said to Moses, "Go down, charge the people, lest they break through to Yahweh to gaze, and many of them perish.

Makuhani nao, wamkaribiao Bwana, na wajitakase, Bwana asije akawafurikia. Kutoka 19:22

Let the priests also, who come near to Yahweh, sanctify themselves, lest Yahweh break forth on them."

Musa akamwambia Bwana, Watu hawa hawawezi kuukaribia mlima wa Sinai; kwa kuwa wewe ulituusia, ukisema, Wekeni mipaka kando-kando ya mlima, na kuutenga. Kutoka 19:23

Moses said to Yahweh, "The people can't come up to Mount Sinai, for you charged us, saying, 'Set bounds around the mountain, and sanctify it.'"

Bwana akamwambia, Nenda, ushuke wewe; nawe utakwea, wewe, na Haruni pamoja nawe; lakini wale makuhani na watu wasipenye kumkaribia Bwana, asije yeye akawafurikia juu yao. Kutoka 19:24

Yahweh said to him, "Go down and you shall bring Aaron up with you, but don't let the priests and the people break through to come up to Yahweh, lest he break forth on them."

Basi Musa akawatelemkia hao watu na kuwaambia hayo.

Kutoka 19:25

So Moses went down to the people, and told them.