Kutoka 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 21 (Swahili) Exodus 21 (English)

Basi hukumu utakazoziweka mbele ya watu ni hizi Kutoka 21:1

"Now these are the ordinances which you shall set before them.

Ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia muda wa miaka sita; mwaka wa saba atatoka kwako huru bure. Kutoka 21:2

If you buy a Hebrew servant, he shall serve six years and in the seventh he shall go out free without paying anything.

Kwamba aliingia kwako peke yake tu, atatoka hivyo peke yake; kwamba ameoa, mkewe atatoka aende pamoja naye. Kutoka 21:3

If he comes in by himself, he shall go out by himself. If he is married, then his wife shall go out with him.

Kwamba ni bwana wake aliyempa huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake. Kutoka 21:4

If his master gives him a wife and she bears him sons or daughters, the wife and her children shall be her master's, and he shall go out by himself.

Lakini huyo mtumwa akisema waziwazi, Mimi nampenda bwana wangu, na mke wangu na watoto wangu; sitaki mimi kutoka niwe huru; Kutoka 21:5

But if the servant shall plainly say, 'I love my master, my wife, and my children. I will not go out free;'

ndipo hapo huyo bwana wake atamleta mbele ya Mungu na kumleta mlangoni, au penye mwimo wa mlango; na bwana wake atalitoboa sikio lake kwa uma; ndipo atamtumikia sikuzote. Kutoka 21:6

then his master shall bring him to God, and shall bring him to the door or to the door-post, and his master shall bore his ear through with an awl, and he shall serve him for ever.

Mtu akimwuza binti yake awe kijakazi, hatatoka yeye kama watumwa wa kiume watokavyo. Kutoka 21:7

"If a man sells his daughter to be a maid-servant, she shall not go out as the men-servants do.

Kwamba bwana wake hakupendezewa naye, akiwa amemposa, ndipo atakubali akombolewe; hana amri yeye kumwuza aende kwa watu wageni maana amemtenda kwa udanganyifu. Kutoka 21:8

If she doesn't please her master, who has married her to himself, then he shall let her be redeemed. He shall have no right to sell her to a foreign people, seeing he has dealt deceitfully with her.

Kwamba amposa mwanawe, atamtendea kama desturi zipasazo binti zake. Kutoka 21:9

If he marries her to his son, he shall deal with her after the manner of daughters.

Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia. Kutoka 21:10

If he takes another wife to himself, he shall not diminish her food, her clothing, and her marital rights.

Kwamba hamfanyii mambo haya matatu, ndipo atatoka aende bure, pasipo kutolewa mali. Kutoka 21:11

If he doesn't do these three things for her, she may go free without paying any money.

Mtu awaye yote ampigaye mtu, hata akafa, hana budi atauawa huyo. Kutoka 21:12

"One who strikes a man so that he dies shall surely be put to death,

Lakini kama hakumvizia, ila Mungu amemtia mkononi mwake; basi nitakuonyesha mahali atakapopakimbilia. Kutoka 21:13

but not if it is unintentional, but God allows it to happen: then I will appoint you a place where he shall flee.

Lakini, mtu akimwendea mwenziwe kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata madhabahuni pangu, auawe. Kutoka 21:14

If a man schemes and comes presumptuously on his neighbor to kill him, you shall take him from my altar, that he may die.

Ampigaye baba yake au mama yake, sharti atauawa. Kutoka 21:15

"Anyone who attacks his father or his mother shall be surely put to death.

Yeye amwibaye mtu, na kumwuza, au akipatikana mkononi mwake, sharti atauawa huyo Kutoka 21:16

"Anyone who kidnaps someone and sells him, or if he is found in his hand, he shall surely be put to death.

Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa. Kutoka 21:17

"Anyone who curses his father or his mother shall surely be put to death.

Watu wakigombana, na mmoja akimpiga mwenziwe kwa jiwe, au kwa konde, asife, lakini yualazwa kitandani mwake; Kutoka 21:18

"If men quarrel and one strikes the other with a stone, or with his fist, and he doesn't die, but is confined to bed;

atakapoinuka tena na kuenenda nje kwa kutegemea fimbo, ndipo hapo yule aliyempiga ataachwa; ila atamlipa kwa ajili ya hayo majira yake yaliyompotea, naye atamwuguza hata apone kabisa. Kutoka 21:19

if he rises again and walks around with his staff, then he who struck him shall be cleared: only he shall pay for the loss of his time, and shall provide for his healing until he is thoroughly healed.

Mtu akimpiga mtumwa wake, au kijakazi chake, kwa fimbo, naye akifa mkononi mwake, hana budi ataadhibiwa. Kutoka 21:20

"If a man strikes his servant or his maid with a rod, and he dies under his hand, he shall surely be punished.

Lakini akipona siku moja au mbili hataadhibiwa; maana, ni mali yake. Kutoka 21:21

Notwithstanding, if he gets up after a day or two, he shall not be punished, for he is his property.

Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema. Kutoka 21:22

"If men fight and hurt a pregnant woman so that she gives birth prematurely, and yet no harm follows, he shall be surely fined as much as the woman's husband demands and the judges allow.

Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai, Kutoka 21:23

But if any harm follows, then you must take life for life,

jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, Kutoka 21:24

eye for eye, tooth for tooth, hand for hand, foot for foot,

kuteketeza kwa kuteketeza, jeraha kwa jeraha, chubuko kwa ajili ya chubuko. Kutoka 21:25

burning for burning, wound for wound, and bruise for bruise.

Mtu akimpiga mtumwa wake jicho, au jicho la kijakazi chake, na kuliharibu; atamwacha huru kwa ajili ya jicho lake. Kutoka 21:26

"If a man strikes his servant's eye, or his maid's eye, and destroys it, he shall let him go free for his eye's sake.

Au akimpiga mtumwa wake jino likang'oka, au jino la kijakazi chake, atamwacha huru kwa ajili ya jino lake. Kutoka 21:27

If he strikes out his man-servant's tooth, or his maid-servant's tooth, he shall let him go free for his tooth's sake.

Ng'ombe akipiga pembe mtu mume au mtu mke, nao wakafa, huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, nyama yake isiliwe; lakini mwenye huyo ng'ombe ataachiliwa. Kutoka 21:28

"If a bull gores a man or a woman to death, the bull shall surely be stoned, and its flesh shall not be eaten; but the owner of the bull shall not be held responsible.

Lakini kwamba huyo ng'ombe alizoea kupiga watu tangu hapo, naye mwenyewe ameonyeshwa jambo hilo, wala asimzuie, naye amemwua mtu mume au mwanamke; huyo ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe, na huyo mwenyewe naye atauawa. Kutoka 21:29

But if the bull had a habit of goring in the past, and it has been testified to its owner, and he has not kept it in, but it has killed a man or a woman, the bull shall be stoned, and its owner shall also be put to death.

Lakini akiandikiwa ukombozi, ndipo atakapotoa kwa ajili ya uhai wake hicho atakachoandikiwa. Kutoka 21:30

If a ransom is laid on him, then he shall give for the redemption of his life whatever is laid on him.

Akiwa ng'ombe amempiga pembe mtoto wa kiume na kumtumbua, au akiwa amempiga mtoto wa kike, atatendwa kama hukumu hiyo. Kutoka 21:31

Whether it has gored a son or has gored a daughter, according to this judgment it shall be done to him.

Ng'ombe akimtumbua mtumwa mume au kijakazi; mwenye ng'ombe atampa bwana wao shekeli thelathini za fedha, naye ng'ombe atauawa kwa kupigwa kwa mawe. Kutoka 21:32

If the bull gores a man-servant or a maid-servant, thirty shekels of silver shall be given to their master, and the ox shall be stoned.

Kwamba mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng'ombe au punda kutumbukia humo, Kutoka 21:33

"If a man opens a pit, or if a man digs a pit and doesn't cover it, and a bull or a donkey falls into it,

mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake. Kutoka 21:34

the owner of the pit shall make it good. He shall give money to its owner, and the dead animal shall be his.

Ng'ombe wa mtu akimwumiza ng'ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng'ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng'ombe aliyekufa pia watamgawanya. Kutoka 21:35

"If one man's bull injures another's, so that it dies, then they shall sell the live bull, and divide its price; and they shall also divide the dead animal.

Au kwamba ilijulikana ya kuwa ng'ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng'ombe kwa ng'ombe, na huyo ng'ombe aliyekufa atakuwa ni wake.

Kutoka 21:36

Or if it is known that the bull was in the habit of goring in the past, and its owner has not kept it in, he shall surely pay bull for bull, and the dead animal shall be his own.