Kutoka 32 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 32 (Swahili) Exodus 32 (English)

Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata. Kutoka 32:1

When the people saw that Moses delayed to come down from the mountain, the people gathered themselves together to Aaron, and said to him, "Come, make us gods, which shall go before us; for as for this Moses, the man who brought us up out of the land of Egypt, we don't know what has become of him."

Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee. Kutoka 32:2

Aaron said to them, "Take off the golden rings, which are in the ears of your wives, of your sons, and of your daughters, and bring them to me."

Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni. Kutoka 32:3

All the people took off the golden rings which were in their ears, and brought them to Aaron.

Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. Kutoka 32:4

He received what they handed him, and fashioned it with an engraving tool, and made it a molten calf; and they said, "These are your gods, Israel, which brought you up out of the land of Egypt."

Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa Bwana. Kutoka 32:5

When Aaron saw this, he built an altar before it; and Aaron made a proclamation, and said, "Tomorrow shall be a feast to Yahweh."

Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze. Kutoka 32:6

They rose up early on the next day, and offered burnt offerings, and brought peace-offerings; and the people sat down to eat and to drink, and rose up to play.

Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, Kutoka 32:7

Yahweh spoke to Moses, "Go, get down; for your people, who you brought up out of the land of Egypt, have corrupted themselves!

wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. Kutoka 32:8

They have turned aside quickly out of the way which I commanded them. They have made themselves a molten calf, and have worshiped it, and have sacrificed to it, and said, 'These are your gods, Israel, which brought you up out of the land of Egypt.'"

Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu Kutoka 32:9

Yahweh said to Moses, "I have seen these people, and, behold, they are a stiff-necked people.

basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu. Kutoka 32:10

Now therefore leave me alone, that my wrath may burn hot against them, and that I may consume them; and I will make of you a great nation."

Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu? Kutoka 32:11

Moses begged Yahweh his God, and said, "Yahweh, why does your wrath burn hot against your people, that you have brought forth out of the land of Egypt with great power and with a mighty hand?

Kwa nini Wamisri kunena, wakisema, Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi? Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako. Kutoka 32:12

Why should the Egyptians speak, saying, 'He brought them forth for evil, to kill them in the mountains, and to consume them from the surface of the earth?' Turn from your fierce wrath, and repent of this evil against your people.

Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele. Kutoka 32:13

Remember Abraham, Isaac, and Israel, your servants, to whom you swore by your own self, and said to them, 'I will multiply your seed as the stars of the sky, and all this land that I have spoken of I will give to your seed, and they shall inherit it forever.'"

Na Bwana akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake. Kutoka 32:14

Yahweh repented of the evil which he said he would do to his people.

Basi, Musa akageuka akashuka katika mlima, na zile mbao mbili za mawe mikononi mwake; mbao zilizoandikwa pande zote mbili, upande huu na upande huu ziliandikwa. Kutoka 32:15

Moses turned, and went down from the mountain, with the two tablets of the testimony in his hand; tablets that were written on both their sides; on the one side and on the other they were written.

Na zile mbao zilikuwa kazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa katika zile mbao. Kutoka 32:16

The tablets were the work of God, and the writing was the writing of God, engraved on the tables.

Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, Kuna kelele ya vita maragoni. Kutoka 32:17

When Joshua heard the noise of the people as they shouted, he said to Moses, "There is the noise of war in the camp."

Akasema, Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa; bali kelele za watu waimbao ndizo ninazozisikia mimi. Kutoka 32:18

He said, "It isn't the voice of those who shout for victory, neither is it the voice of those who cry for being overcome; but the noise of those who sing that I hear."

Hata alipoyakaribia marago akaiona ile ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima. Kutoka 32:19

It happened, as soon as he came near to the camp, that he saw the calf and the dancing: and Moses' anger grew hot, and he threw the tablets out of his hands, and broke them beneath the mountain.

Akaitwaa ile ndama waliyoifanya, akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza juu ya maji, akawanywesha wana wa Israeli. Kutoka 32:20

He took the calf which they had made, and burnt it with fire, ground it to powder, and scattered it on the water, and made the children of Israel drink of it.

Musa akamwambia Haruni Watu hawa wamekufanyani hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao? Kutoka 32:21

Moses said to Aaron, "What did these people do to you, that you have brought a great sin on them?"

Haruni akasema, Hasira ya bwana wangu isiwake, wewe unawajua watu hawa, ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya. Kutoka 32:22

Aaron said, "Don't let the anger of my lord grow hot. You know the people, that they are set on evil.

Maana waliniambia, Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu, kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata. Kutoka 32:23

For they said to me, 'Make us gods, which shall go before us; for as for this Moses, the man who brought us up out of the land of Egypt, we don't know what has become of him.'

Nikawaambia, Mtu ye yote aliye na dhahabu na aivunje; basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu. Kutoka 32:24

I said to them, 'Whoever has any gold, let them take it off:' so they gave it me; and I threw it into the fire, and out came this calf."

Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, ili wawe dhihaka kati ya adui zao, Kutoka 32:25

When Moses saw that the people had broken loose, (for Aaron had let them loose for a derision among their enemies),

ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago, akasema, Mtu awaye yote aliye upande wa Bwana, na aje kwangu. Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia Kutoka 32:26

then Moses stood in the gate of the camp, and said, "Whoever is on Yahweh's side, come to me!" All the sons of Levi gathered themselves together to him.

Akawaambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake. Kutoka 32:27

He said to them, "Thus says Yahweh, the God of Israel, 'Every man put his sword on his thigh, and go back and forth from gate to gate throughout the camp, and every man kill his brother, and every man his companion, and every man his neighbor."

Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu. Kutoka 32:28

The sons of Levi did according to the word of Moses: and there fell of the people that day about three thousand men.

Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa Bwana leo, naam, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili awape baraka leo. Kutoka 32:29

Moses said, "Consecrate yourselves today to Yahweh, yes, every man against his son, and against his brother; that he may bestow on you a blessing this day."

Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu, Mmetenda dhambi kuu; na sasa nitakwenda juu kwa Bwana, labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu. Kutoka 32:30

It happened on the next day, that Moses said to the people, "You have sinned a great sin. Now I will go up to Yahweh. Perhaps I shall make atonement for your sin."

Musa akarejea kwa Bwana akasema, Aa! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu. Kutoka 32:31

Moses returned to Yahweh, and said, "Oh, this people have sinned a great sin, and have made themselves gods of gold.

Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao -- na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika. Kutoka 32:32

Yet now, if you will, forgive their sin-- and if not, please blot me out of your book which you have written."

Bwana akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu. Kutoka 32:33

Yahweh said to Moses, "Whoever has sinned against me, him will I blot out of my book.

Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao. Kutoka 32:34

Now go, lead the people to the place of which I have spoken to you. Behold, my angel shall go before you. Nevertheless in the day when I punish, I will punish them for their sin."

Bwana akawapiga hao watu, kwa walivyoifanya ile ndama, ambayo Haruni aliifanya.

Kutoka 32:35

Yahweh struck the people, because they made the calf, which Aaron made.