Kutoka 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Kutoka 2 (Swahili) Exodus 2 (English)

Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaondoka akaoa binti mmoja wa Lawi. Kutoka 2:1

A man of the house of Levi went and took a daughter of Levi as his wife.

Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu. Kutoka 2:2

The woman conceived, and bore a son. When she saw that he was a fine child, she hid him three months.

Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akampatia kisafina cha manyasi akakipaka sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka katika majani kando ya mto. Kutoka 2:3

When she could no longer hide him, she took a papyrus basket for him, and coated it with tar and with pitch. She put the child in it, and laid it in the reeds by the river's bank.

Umbu lake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata. Kutoka 2:4

His sister stood far off, to see what would be done to him.

Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kisafina katika majani, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta. Kutoka 2:5

Pharaoh's daughter came down to bathe at the river. Her maidens walked along by the riverside. She saw the basket among the reeds, and sent her handmaid to get it.

Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania. Kutoka 2:6

She opened it, and saw the child, and, behold, the baby cried. She had compassion on him, and said, "This is one of the Hebrews' children."

Basi umbu lake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu? Kutoka 2:7

Then his sister said to Pharaoh's daughter, "Should I go and call a nurse for you from the Hebrew women, that she may nurse the child for you?"

Binti Farao akamwambia, Haya! Enenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto. Kutoka 2:8

Pharaoh's daughter said to her, "Go." The maiden went and called the child's mother.

Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha. Kutoka 2:9

Pharaoh's daughter said to her, "Take this child away, and nurse him for me, and I will give you your wages." The woman took the child, and nursed it.

Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa, akasema, Ni kwa sababu nalimtoa majini. Kutoka 2:10

The child grew, and she brought him to Pharaoh's daughter, and he became her son. She named him Moses,{"Moses" sounds like the Hebrew for "draw out".} and said, "Because I drew him out of the water."

Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake. Kutoka 2:11

It happened in those days, when Moses had grown up, that he went out to his brothers, and looked at their burdens. He saw an Egyptian striking a Hebrew, one of his brothers.

Basi akatazama huko na huko, na alipoona ya kuwa hapana mtu, akampiga Mmisri yule, akamficha ndani ya mchanga. Kutoka 2:12

He looked this way and that way, and when he saw that there was no one, he killed the Egyptian, and hid him in the sand.

Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, Mbona unampiga mwenzako? Kutoka 2:13

He went out the second day, and, behold, two men of the Hebrews were fighting with each other. He said to him who did the wrong, "Why do you strike your fellow?"

Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana. Kutoka 2:14

He said, "Who made you a prince and a judge over us? Do you plan to kill me, as you killed the Egyptian?" Moses was afraid, and said, "Surely this thing is known."

Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima. Kutoka 2:15

Now when Pharaoh heard this thing, he sought to kill Moses. But Moses fled from the face of Pharaoh, and lived in the land of Midian, and he sat down by a well.

Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao. Kutoka 2:16

Now the priest of Midian had seven daughters. They came and drew water, and filled the troughs to water their father's flock.

Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao. Kutoka 2:17

The shepherds came and drove them away; but Moses stood up and helped them, and watered their flock.

Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo? Kutoka 2:18

When they came to Reuel, their father, he said, "How is it that you have returned so early today?"

Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi. Kutoka 2:19

They said, "An Egyptian delivered us out of the hand of the shepherds, and moreover he drew water for us, and watered the flock."

Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula. Kutoka 2:20

He said to his daughters, "Where is he? Why is it that you have left the man? Call him, that he may eat bread."

Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora. Kutoka 2:21

Moses was content to dwell with the man. He gave Moses Zipporah, his daughter.

Huyo akamzalia mwana, akamwita jina lake Gershomu, maana alisema, Nimekuwa mgeni katika nchi ya ugeni. Kutoka 2:22

She bore a son, and he named him Gershom,{"Gershom" sounds like the Hebrew for "an alien there."} for he said, "I have lived as a foreigner in a foreign land."

Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. Kutoka 2:23

It happened in the course of those many days, that the king of Egypt died, and the children of Israel sighed because of the bondage, and they cried, and their cry came up to God because of the bondage.

Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. Kutoka 2:24

God heard their groaning, and God remembered his covenant with Abraham, with Isaac, and with Jacob.

Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.

Kutoka 2:25

God saw the children of Israel, and God was concerned about them.