Mwanzo 38 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 38 (Swahili) Genesis 38 (English)

Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira. Mwanzo 38:1

It happened at that time, that Judah went down from his brothers, and visited a certain Adullamite, whose name was Hirah.

Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake. Mwanzo 38:2

Judah saw there a daughter of a certain Canaanite whose name was Shua. He took her, and went in to her.

Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri. Mwanzo 38:3

She conceived, and bore a son; and he named him Er.

Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani. Mwanzo 38:4

She conceived again, and bore a son; and she named him Onan.

Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa. Mwanzo 38:5

She yet again bore a son, and named him Shelah: and he was at Chezib, when she bore him.

Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari. Mwanzo 38:6

Judah took a wife for Er, his firstborn, and her name was Tamar.

Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana; na Bwana akamwua. Mwanzo 38:7

Er, Judah's firstborn, was wicked in the sight of Yahweh. Yahweh killed him.

Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao. Mwanzo 38:8

Judah said to Onan, "Go in to your brother's wife, and perform the duty of a husband's brother to her, and raise up seed to your brother."

Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao. Mwanzo 38:9

Onan knew that the seed wouldn't be his; and it happened, when he went in to his brother's wife, that he spilled it on the ground, lest he should give seed to his brother.

Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye. Mwanzo 38:10

The thing which he did was evil in the sight of Yahweh, and he killed him also.

Yuda akamwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata Shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, Asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye. Mwanzo 38:11

Then Judah said to Tamar, his daughter-in-law, "Remain a widow in your father's house, until Shelah, my son, is grown up;" for he said, "Lest he also die, like his brothers." Tamar went and lived in her father's house.

Siku nyingi zikapita, akafa binti Shua, mkewe Yuda. Yuda akafarijika, akaenda kwa watu wake wawakatao manyoya kondoo huko Timna, yeye na mwenzake Hira, Mwadulami. Mwanzo 38:12

After many days, Shua's daughter, the wife of Judah, died. Judah was comforted, and went up to his sheep-shearers to Timnah, he and his friend Hirah, the Adullamite.

Huyo Tamari akapewa habari, kusema, Mkweo anakwenda Timna, akate manyoya ya kondoo zake. Mwanzo 38:13

It was told Tamar, saying, "Behold, your father-in-law is going up to Timnah to shear his sheep."

Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, wala hakuozwa awe mkewe. Mwanzo 38:14

She took off of her the garments of her widowhood, and covered herself with her veil, and wrapped herself, and sat in the gate of Enaim, which is by the way to Timnah; for she saw that Shelah was grown up, and she wasn't given to him as a wife.

Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso. Mwanzo 38:15

When Judah saw her, he thought that she was a prostitute, for she had covered her face.

Akamgeukia kando ya njia, akasema, Niruhusu niingie kwako. Maana hakujua ya kuwa ni mkwewe. Akamwuliza, Utanipa nini, ukiingia kwangu? Mwanzo 38:16

He turned to her by the way, and said, "Please come, let me come in to you:" for he didn't know that she was his daughter-in-law. She said, "What will you give me, that you may come in to me?"

Akasema, Nitakuletea mwana-mbuzi wa kundini. Naye akamwuliza, Je! Utanipa rehani hata utakapomleta? Mwanzo 38:17

He said, "I will send you a kid of the goats from the flock." She said, "Will you give me a pledge, until you send it?"

Akasema, Nikupe rehani gani? Akamjibu, Pete yako ya muhuri, na kamba yake, na fimbo yako iliyo mkononi mwako. Basi akampa, akaingia kwake, naye akapata mimba. Mwanzo 38:18

He said, "What pledge will I give you?" She said, "Your signet and your cord, and your staff that is in your hand." He gave them to her, and came in to her, and she conceived by him.

Akaondoka, akaenda zake, akavua utaji wake, na kuvaa mavazi ya ujane wake. Mwanzo 38:19

She arose, and went away, and put off her veil from her, and put on the garments of her widowhood.

Yuda akapeleka yule mwana-mbuzi kwa mkono wa rafiki yake Mwadulami, ili aipate rehani mkononi mwa huyo mwanamke lakini hakumkuta. Mwanzo 38:20

Judah sent the kid of the goats by the hand of his friend, the Adullamite, to receive the pledge from the woman's hand, but he didn't find her.

Akauliza watu wa mahali pale, akisema, Yuko wapi yule kahaba aliyekuwapo Enaimu kando ya njia? Wakasema, Hakuwako hapa kahaba. Mwanzo 38:21

Then he asked the men of her place, saying, "Where is the prostitute, that was at Enaim by the road?" They said, "There has been no prostitute here."

Akamrudia Yuda akasema, Sikumwona; hata na watu wa mahali hapo walisema, Hakuwako kahaba. Mwanzo 38:22

He returned to Judah, and said, "I haven't found her; and also the men of the place said, 'There has been no prostitute here.'"

Yuda akasema, Na aichukue yeye, tusije tukatiwa aibu; tazama, nimempelekea mbuzi huyu, wala hukumkuta. Mwanzo 38:23

Judah said, "Let her keep it, lest we be shamed. Behold, I sent this kid, and you haven't found her."

Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari, amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Yuda akasema, Mtoeni ateketezwe. Mwanzo 38:24

It happened about three months later, that it was told Judah, saying, "Tamar, your daughter-in-law, has played the prostitute; and moreover, behold, she is with child by prostitution." Judah said, "Bring her forth, and let her be burnt."

Alipotolewa, alipeleka watu kwa mkwewe, akisema, Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu hivi. Akasema, Tambua basi, vitu hivi ni vya nani, pete hii, na kamba hii, na fimbo hii. Mwanzo 38:25

When she was brought forth, she sent to her father-in-law, saying, "By the man, whose these are, I am with child." She also said, "Please discern whose are these-- the signet, and the cords, and the staff."

Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo. Mwanzo 38:26

Judah acknowledged them, and said, "She is more righteous than I, because I didn't give her to Shelah, my son." He knew her again no more.

Ikawa, wakati wake wa kuzaa walikuwapo mapacha tumboni mwake. Mwanzo 38:27

It happened in the time of her travail, that behold, twins were in her womb.

Ikawa alipokuwa akizaa, mtoto mmoja akatoa mkono, mzalisha akautwaa uzi mwekundu akaufunga mkononi mwake, huku akisema, Huyu ametoka kwanza. Mwanzo 38:28

It happened, when she travailed, that one put out a hand: and the midwife took and tied a scarlet thread on his hand, saying, "This came out first."

Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka. Akasema, Mbona umepita kwa nguvu wewe? Mambo ya nguvu na yakuandame. Kwa hiyo jina lake likaitwa Peresi. Mwanzo 38:29

It happened, as he drew back his hand, that behold, his brother came out, and she said, "Why have you made a breach for yourself?" Therefore his name was called Perez.{Perez means "breaking out."}

Akatoka ndugu yake baadaye, ana uzi mwekundu mkononi mwake; naye akaitwa jina lake Zera.

Mwanzo 38:30

Afterward his brother came out, that had the scarlet thread on his hand, and his name was called Zerah.{Zerah means "scarlet" or "brightness."}