Mwanzo 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 12 (Swahili) Genesis 12 (English)

Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; Mwanzo 12:1

Now Yahweh said to Abram, "Get out of your country, and from your relatives, and from your father's house, to the land that I will show you.

nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; Mwanzo 12:2

I will make of you a great nation. I will bless you, and make your name great. You will be a blessing.

nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. Mwanzo 12:3

I will bless those who bless you, and I will curse him who curses you. In you will all of the families of the earth be blessed."

Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani. Mwanzo 12:4

So Abram went, as Yahweh had spoken to him. Lot went with him. Abram was seventy-five years old when he departed out of Haran.

Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani. Mwanzo 12:5

Abram took Sarai his wife, Lot his brother's son, all their substance that they had gathered, and the souls who they had gotten in Haran; and they went forth to go into the land of Canaan. Into the land of Canaan they came.

Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo. Mwanzo 12:6

Abram passed through the land to the place of Shechem, to the oak of Moreh. The Canaanite was then in the land.

Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea. Mwanzo 12:7

Yahweh appeared to Abram, and said, "I will give this land to your seed{or, offspring}." He built an altar there to Yahweh, who appeared to him.

Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Mwanzo 12:8

He left from there to the mountain on the east of Bethel, and pitched his tent, having Bethel on the west, and Ai on the east. There he built an altar to Yahweh, and called on the name of Yahweh.

Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pande za kusini. Mwanzo 12:9

Abram traveled, going on still toward the South.

Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi. Mwanzo 12:10

There was a famine in the land. Abram went down into Egypt to live as a foreigner there, for the famine was sore in the land.

Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso; Mwanzo 12:11

It happened, when he was come near to enter into Egypt, that he said to Sarai his wife, "See now, I know that you are a beautiful woman to look on.

basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai. Mwanzo 12:12

It will happen, when the Egyptians will see you, that they will say, 'This is his wife.' They will kill me, but they will save you alive.

Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako. Mwanzo 12:13

Please say that you are my sister, that it may be well with me for your sake, and that my soul may live because of you."

Basi ikawa Abramu alipofika Misri, Wamisri wakamwona huyo mwanamke ya kwamba yeye ni mzuri sana. Mwanzo 12:14

It happened that when Abram had come into Egypt, the Egyptians saw that the woman was very beautiful.

Wakuu wa Farao wakamwona, nao wakamsifu kwa Farao; basi yule mwanamke akachukuliwa nyumbani mwa Farao. Mwanzo 12:15

The princes of Pharaoh saw her, and praised her to Pharaoh; and the woman was taken into Pharaoh's house.

Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng'ombe, na punda waume, na watumwa, na wajakazi, na punda wake, na ngamia. Mwanzo 12:16

He dealt well with Abram for her sake. He had sheep, and oxen, and male donkeys, and men-servants, and maid-servants, and female donkeys, and camels.

Lakini Bwana akampiga Farao na nyumba yake mapigo makuu, kwa ajili ya Sarai, mkewe Abramu. Mwanzo 12:17

Yahweh plagued Pharaoh and his house with great plagues because of Sarai, Abram's wife.

Ndipo Farao akamwita Abramu, akasema, N'nini hili ulilonitendea? Mbona hukuniambia ya kuwa huyo ni mkeo? Mwanzo 12:18

Pharaoh called Abram, and said, "What is this that you have done to me? Why didn't you tell me that she was your wife?

Mbona ulisema, Huyo ni umbu langu, hata nikamtwaa kuwa mke wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako. Mwanzo 12:19

Why did you say, 'She is my sister,' so that I took her to be my wife? Now therefore, see your wife, take her, and go your way."

Farao akawaagiza watu kwa ajili yake, wakampeleka njiani, na mkewe, na kila alichokuwa nacho. Mwanzo 12:20

Pharaoh gave men charge concerning him: and they brought him on the way, and his wife, and all that he had.