Mwanzo 45 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 45 (Swahili) Genesis 45 (English)

Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. Mwanzo 45:1

Then Joseph couldn't control himself before all those who stood before him, and he cried, "Cause every man to go out from me!" There stood no man with him, while Joseph made himself known to his brothers.

Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia. Mwanzo 45:2

He wept aloud. The Egyptians heard, and the house of Pharaoh heard.

Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake. Mwanzo 45:3

Joseph said to his brothers, "I am Joseph! Does my father still live?" His brothers couldn't answer him; for they were terrified at his presence.

Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. Mwanzo 45:4

Joseph said to his brothers, "Come near to me, please." They came near. "He said, I am Joseph, your brother, whom you sold into Egypt.

Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. Mwanzo 45:5

Now don't be grieved, nor angry with yourselves, that you sold me here, for God sent me before you to preserve life.

Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna. Mwanzo 45:6

For these two years the famine has been in the land, and there are yet five years, in which there will be neither plowing nor harvest.

Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu. Mwanzo 45:7

God sent me before you to preserve you a remnant in the earth, and to save you alive by a great deliverance.

Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri. Mwanzo 45:8

So now it wasn't you who sent me here, but God, and he has made me a father to Pharaoh, lord of all his house, and ruler over all the land of Egypt.

Fanyeni haraka, mmwendee baba yangu, mkamwambie, Hivi ndivyo asemavyo mwanao Yusufu, Mungu ameniweka kuwa bwana katika Misri yote, basi unishukie, usikawie. Mwanzo 45:9

Hurry, and go up to my father, and tell him, 'This is what your son Joseph says, "God has made me lord of all Egypt. Come down to me. Don't wait.

Nawe utakaa katika nchi ya Gosheni, utakuwa karibu nami, wewe, na wanao, na wana wa wanao, na wanyama wako, ng'ombe zako, na yote uliyo nayo. Nami nitakulisha huko; Mwanzo 45:10

You shall dwell in the land of Goshen, and you will be near to me, you, your children, your children's children, your flocks, your herds, and all that you have.

maana bado imesalia miaka mitano ya njaa; usije ukaingia katika uhitaji, wewe, na nyumba yako, na yote uliyo nayo. Mwanzo 45:11

There I will nourish you; for there are yet five years of famine; lest you come to poverty, you, and your household, and all that you have."'

Na tazama, macho yenu yanaona, na macho ya ndugu yangu Benyamini, ya kwamba ni kinywa changu mimi kinachosema nanyi. Mwanzo 45:12

Behold, your eyes see, and the eyes of my brother Benjamin, that it is my mouth that speaks to you.

Nanyi mtamwarifu baba yangu habari za fahari yangu yote katika Misri, na za vyote mlivyoviona; mkafanye haraka kumleta huku baba yangu. Mwanzo 45:13

You shall tell my father of all my glory in Egypt, and of all that you have seen. You shall hurry and bring my father down here."

Akaanguka shingoni mwa ndugu yake Benyamini, akalia; Benyamini naye akalia shingoni mwake. Mwanzo 45:14

He fell on his brother Benjamin's neck, and wept, and Benjamin wept on his neck.

Akawabusu ndugu zake wote, akalia nao, baada ya hayo, nduguze wakazungumza naye Mwanzo 45:15

He kissed all his brothers, and wept on them. After that his brothers talked with him.

Habari ikasikika nyumbani mwa Farao kusema, Ndugu zake Yusufu wamekuja. Ikawa vema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake. Mwanzo 45:16

The report of it was heard in Pharaoh's house, saying, "Joseph's brothers have come." It pleased Pharaoh well, and his servants.

Farao akamwambia Yusufu, Uwaambie ndugu zako, Fanyeni hivi; wachukuzeni mizigo wanyama wenu, mwondoke mwende nchi ya Kanaani; Mwanzo 45:17

Pharaoh said to Joseph, "Tell your brothers, 'Do this. Load your animals, and go, travel to the land of Canaan.

kisha mkamtwae baba yenu, na watu wa nyumbani mwenu, mkanijie; nami nitawapa mema ya nchi ya Misri, nanyi mtakula unono wa nchi. Mwanzo 45:18

Take your father and your households, and come to me, and I will give you the good of the land of Egypt, and you will eat the fat of the land.'

Nawe umeamriwa; fanyeni hivi, mjitwalie magari katika nchi ya Misri kwa watoto wenu wadogo na wake zenu, mkamchukue baba yenu mje. Mwanzo 45:19

Now you are commanded: do this. Take wagons out of the land of Egypt for your little ones, and for your wives, and bring your father, and come.

Wala msivisumbukie vyombo vyenu, maana mema ya nchi yote ya Misri ni yenu. Mwanzo 45:20

Also, don't concern yourselves about your belongings, for the good of all of the land of Egypt is yours."

Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli. Yusufu akawapa magari kama Farao alivyoamuru, akawapa na chakula cha njiani. Mwanzo 45:21

The sons of Israel did so. Joseph gave them wagons, according to the commandment of Pharaoh, and gave them provision for the way.

Akawapa kila mtu nguo za kubadili; lakini Benyamini, alimpa fedha mia tatu na mavazi matano ya kubadili. Mwanzo 45:22

To all of them he gave each man changes of clothing, but to Benjamin he gave three hundred pieces of silver and five changes of clothing.

Na babaye akampelekea kama hivi, punda kumi waliochukua mema ya Misri, na punda wake kumi waliochukua nafaka, na mikate, na chakula kwa babaye njiani. Mwanzo 45:23

To his father, he sent after this manner: ten donkeys loaded with the good things of Egypt, and ten female donkeys loaded with grain and bread and provision for his father by the way.

Akaagana na ndugu zake, wakaenda zao; naye akawaambia, Msigombane njiani. Mwanzo 45:24

So he sent his brothers away, and they departed. He said to them, "See that you don't quarrel on the way."

Wakatoka Misri, wakafika nchi ya Kanaani kwa Yakobo, baba yao. Mwanzo 45:25

They went up out of Egypt, and came into the land of Canaan, to Jacob their father.

Wakampasha habari, wakisema, Yusufu angali hai; naye ndiye mtawala katika nchi yote ya Misri. Moyo wake ukazimia, kwa sababu hakuwasadiki. Mwanzo 45:26

They told him, saying, "Joseph is still alive, and he is ruler over all the land of Egypt." His heart fainted, for he didn't believe them.

Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyoyapeleka Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka. Mwanzo 45:27

They told him all the words of Joseph, which he had said to them. When he saw the wagons which Joseph had sent to carry him, the spirit of Jacob, their father, revived.

Israeli akasema, Yatosha! Yusufu mwanangu angali hai; nitakwenda, nionane naye kabla sijafa.

Mwanzo 45:28

Israel said, "It is enough. Joseph my son is still alive. I will go and see him before I die."