Mwanzo 32 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 32 (Swahili) Genesis 32 (English)

Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye. Mwanzo 32:1

Jacob went on his way, and the angels of God met him.

Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu. Mwanzo 32:2

When he saw them, Jacob said, "This is God's host." He called the name of that place Mahanaim.

Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu. Mwanzo 32:3

Jacob sent messengers in front of him to Esau, his brother, to the land of Seir, the field of Edom.

Akawaagiza akisema, Mwambieni hivi bwana wangu, Esau, Hivi ndivyo asemavyo mtumwa wako, Yakobo; Nimekaa ugenini kwa Labani, na kukawia huko hata sasa, Mwanzo 32:4

He commanded them, saying, "This is what you shall tell my lord, Esau: 'This is what your servant, Jacob, says. I have lived as a foreigner with Laban, and stayed until now.

nami nina ng'ombe, na punda, na kondoo, na watumwa, na vijakazi; nami nimepeleka watu nimpashe bwana wangu habari, nipate neema machoni pako. Mwanzo 32:5

I have oxen, donkeys, flocks, men-servants, and maid-servants. I have sent to tell my lord, that I may find favor in your sight.'"

Wale wajumbe wakarudi kwa Yakobo wakisema, Tulifika kwa ndugu yako, Esau, naye anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye. Mwanzo 32:6

The messengers returned to Jacob, saying, "We came to your brother Esau. Not only that, but he comes to meet you, and four hundred men with him."

Ndipo Yakobo akaogopa sana, na kufadhaika sana, akawagawanya watu waliopo pamoja naye, na kondoo, na ng'ombe, na ngamia, wawe matuo mawili. Mwanzo 32:7

Then Jacob was greatly afraid and was distressed: and he divided the people who were with him, and the flocks, and the herds, and the camels, into two companies;

Akasema, Akija Esau kwa kundi la kwanza, akalipiga, kundi litakalosalia litaokoka. Mwanzo 32:8

and he said, "If Esau comes to the one company, and strikes it, then the company which is left will escape."

Yakobo akasema, Ee Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Bwana, uliyeniambia, Rudi uende mpaka nchi yako, na kwa jamaa zako, nami nitakutendea mema; Mwanzo 32:9

Jacob said, "God of my father Abraham, and God of my father Isaac, Yahweh, who said to me, 'Return to your country, and to your relatives, and I will do you good.'

mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nalivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa matuo mawili. Mwanzo 32:10

I am not worthy of the least of all the loving kindnesses, and of all the truth, which you have shown to your servant; for with just my staff I passed over this Jordan; and now I have become two companies.

Uniokoe sasa na mkono wa ndugu yangu, mkono wa Esau, maana mimi namwogopa, asije akanipiga, na mama pamoja na wana. Mwanzo 32:11

Please deliver me from the hand of my brother, from the hand of Esau: for I fear him, lest he come and strike me, and the mothers with the children.

Nawe ulisema, Hakika nitakutendea mema, nami nitafanya uzao wako uwe kama mchanga wa bahari, usiohesabika kwa kuwa mwingi. Mwanzo 32:12

You said, 'I will surely do you good, and make your seed as the sand of the sea, which can't be numbered because there are so many.'"

Akakaa huko usiku ule. Kisha akatwaa baadhi ya vitu alivyokuwa navyo, kuwa zawadi kwa Esau, nduguye; Mwanzo 32:13

He lodged there that night, and took from that which he had with him, a present for Esau, his brother:

mbuzi wake mia mbili, na mbuzi waume ishirini, kondoo wake mia mbili, na kondoo waume ishirini; Mwanzo 32:14

two hundred female goats and twenty male goats, two hundred ewes and twenty rams,

ngamia wanyonyeshao thelathini pamoja na wana wao, ng'ombe wake arobaini na mafahali kumi; punda wake ishirini na wana wao kumi. Mwanzo 32:15

thirty milk camels and their colts, forty cows, ten bulls, twenty she-donkeys and ten foals.

Akawatia mkononi mwa watumwa wake, kila kundi peke yake. Naye akawaambia watumwa wake, Vukeni mbele yangu, mkaache nafasi kati ya kundi na kundi. Mwanzo 32:16

He delivered them into the hands of his servants, every herd by itself, and said to his servants, "Pass over before me, and put a space between herd and herd."

Akamwagiza yule wa kwanza akasema, Esau, ndugu yangu, akikukuta, na kukuuliza, akisema, Wewe u wa nani? Unakwenda wapi? Tena ni wa nani hawa walio mbele yako? Mwanzo 32:17

He commanded the foremost, saying, "When Esau, my brother, meets you, and asks you, saying, 'Whose are you? Where are you going? Whose are these before you?'

Basi, useme, Ni wa mtumwa wako, Yakobo, ni zawadi, aliyompelekea bwana wangu, Esau. Na tazama, yeye mwenyewe yuko nyuma yetu. Mwanzo 32:18

Then you shall say, 'They are your servant, Jacob's. It is a present sent to my lord, Esau. Behold, he also is behind us.'"

Akamwagiza tena wa pili, na wa tatu, wote waliofuata makundi, akisema, Hivi ndivyo mtakavyomwambia Esau, akiwakuta. Mwanzo 32:19

He commanded also the second, and the third, and all that followed the herds, saying, "This is how you shall speak to Esau, when you find him.

Tena semeni, Tazama, mtumwa wako, Yakobo, yuko nyuma yetu. Maana alisema, Nitamsuluhisha kwa zawadi inayonitangulia, baadaye nitamwona uso wake; huenda atanikubali uso wangu. Mwanzo 32:20

You shall say, 'Not only that, but behold, your servant, Jacob, is behind us.'" For, he said, "I will appease him with the present that goes before me, and afterward I will see his face. Perhaps he will accept me."

Basi ile zawadi ikavuka mbele yake, naye mwenyewe akakaa usiku ule kambini. Mwanzo 32:21

So the present passed over before him: and he himself lodged that night in the camp.

Akaondoka usiku ule akawatwaa wakeze wawili, na vijakazi wake wawili, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki. Mwanzo 32:22

He rose up that night, and took his two wives, and his two handmaids, and his eleven sons, and passed over the ford of the Jabbok.

Akawatwaa, akawavusha mto, akavusha na vyote alivyokuwa navyo. Mwanzo 32:23

He took them, and sent them over the stream, and sent over that which he had.

Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. Mwanzo 32:24

Jacob was left alone, and wrestled with a man there until the breaking of the day.

Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. Mwanzo 32:25

When he saw that he didn't prevail against him, he touched the hollow of his thigh, and the hollow of Jacob's thigh was strained, as he wrestled.

Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki. Mwanzo 32:26

The man said, "Let me go, for the day breaks." Jacob said, "I won't let you go, unless you bless me."

Akamwuliza, Jina lako n'nani? Akasema, Yakobo. Mwanzo 32:27

He said to him, "What is your name?" He said, "Jacob."

Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda. Mwanzo 32:28

He said, "Your name will no longer be called 'Jacob,' but, 'Israel,' for you have fought with God and with men, and have prevailed."

Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko. Mwanzo 32:29

Jacob asked him, "Please tell me your name." He said, "Why is it that you ask what my name is?" He blessed him there.

Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka. Mwanzo 32:30

Jacob called the name of the place Peniel{Peniel means "face of God."}: for, he said, "I have seen God face to face, and my life is preserved."

Jua likamzukia akivuka Penueli, akachechemea kwa sababu ya paja la mguu wake. Mwanzo 32:31

The sun rose on him as he passed over Peniel, and he limped because of his thigh.

Kwa hiyo wana wa Israeli hawali ule mshipa ulio katika uvungu wa paja hata leo; maana alimgusa Yakobo panapo uvungu wa paja katika mshipa wa kiuno.

Mwanzo 32:32

Therefore the children of Israel don't eat the sinew of the hip, which is on the hollow of the thigh, to this day, because he touched the hollow of Jacob's thigh in the sinew of the hip.