Mwanzo 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 19 (Swahili) Genesis 19 (English)

Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. Mwanzo 19:1

The two angels came to Sodom at evening. Lot sat in the gate of Sodom. Lot saw them, and rose up to meet them. He bowed himself with his face to the earth,

Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. Mwanzo 19:2

and he said, "See now, my lords, please turn aside into your servant's house, stay all night, wash your feet, and you will rise up early, and go on your way." They said, "No, but we will stay in the street all night."

Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala. Mwanzo 19:3

He urged them greatly, and they came in with him, and entered into his house. He made them a feast, and baked unleavened bread, and they ate.

Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote. Mwanzo 19:4

But before they lay down, the men of the city, the men of Sodom, surrounded the house, both young and old, all the people from every quarter.

Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua. Mwanzo 19:5

They called to Lot, and said to him, "Where are the men who came in to you this night? Bring them out to us, that we may have sex with them."

Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake. Mwanzo 19:6

Lot went out to them to the door, and shut the door after him.

Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. Mwanzo 19:7

He said, "Please, my brothers, don't act so wickedly.

Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu. Mwanzo 19:8

See now, I have two virgin daughters. Please let me bring them out to you, and do you to them as is good in your eyes. Only don't do anything to these men, because they have come under the shadow of my roof."

Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango. Mwanzo 19:9

They said, "Stand back!" They said, "This one fellow came in to live as a foreigner, and he appoints himself a judge. Now will we deal worse with you, than with them!" They pressed hard on the man, even Lot, and drew near to break the door.

Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango. Mwanzo 19:10

But the men put forth their hand, and brought Lot into the house to them, and shut the door.

Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango. Mwanzo 19:11

They struck the men who were at the door of the house with blindness, both small and great, so that they wearied themselves to find the door.

Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; Mwanzo 19:12

The men said to Lot, "Do you have anybody else here? Sons-in-law, your sons, your daughters, and whoever you have in the city, bring them out of the place:

maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu. Mwanzo 19:13

for we will destroy this place, because the cry of them is grown great before Yahweh. Yahweh has sent us to destroy it."

Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze. Mwanzo 19:14

Lot went out, and spoke to his sons-in-law, who were pledged to marry his daughters, and said, "Get up! Get out of this place, for Yahweh will destroy the city." But he seemed to his sons-in-law to be joking.

Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. Mwanzo 19:15

When the morning arose, then the angels hurried Lot, saying, "Arise, take your wife, and your two daughters who are here, lest you be consumed in the iniquity of the city."

Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. Mwanzo 19:16

But he lingered; and the men laid hold on his hand, and on the hand of his wife, and on the hand of his two daughters, Yahweh being merciful to him; and they took him out, and set him outside of the city.

Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Mwanzo 19:17

It came to pass, when they had taken them out, that he said, "Escape for your life! Don't look behind you, neither stay anywhere in the plain. Escape to the mountain, lest you be consumed!"

Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! Mwanzo 19:18

Lot said to them, "Oh, not so, my lord.

Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa. Mwanzo 19:19

See now, your servant has found favor in your sight, and you have magnified your loving kindness, which you have shown to me in saving my life. I can't escape to the mountain, lest evil overtake me, and I die.

Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi. Mwanzo 19:20

See now, this city is near to flee to, and it is a little one. Oh let me escape there (isn't it a little one?), and my soul will live."

Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. Mwanzo 19:21

He said to him, "Behold, I have granted your request concerning this thing also, that I will not overthrow the city of which you have spoken.

Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari. Mwanzo 19:22

Hurry, escape there, for I can't do anything until you get there." Therefore the name of the city was called Zoar.{Zoar means "little."}

Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. Mwanzo 19:23

The sun was risen on the earth when Lot came to Zoar.

Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana. Mwanzo 19:24

Then Yahweh rained on Sodom and on Gomorrah sulfur and fire from Yahweh out of the sky.

Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile. Mwanzo 19:25

He overthrew those cities, all the plain, all the inhabitants of the cities, and that which grew on the ground.

Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi. Mwanzo 19:26

But his wife looked back from behind him, and she became a pillar of salt.

Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za Bwana, Mwanzo 19:27

Abraham got up early in the morning to the place where he had stood before Yahweh.

naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuru. Mwanzo 19:28

He looked toward Sodom and Gomorrah, and toward all the land of the plain, and looked, and saw that the smoke of the land went up as the smoke of a furnace.

Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu. Mwanzo 19:29

It happened, when God destroyed the cities of the plain, that God remembered Abraham, and sent Lot out of the midst of the overthrow, when he overthrew the cities in which Lot lived.

Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili. Mwanzo 19:30

Lot went up out of Zoar, and lived in the mountain, and his two daughters with him; for he was afraid to live in Zoar. He lived in a cave with his two daughters.

Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. Mwanzo 19:31

The firstborn said to the younger, "Our father is old, and there is not a man in the earth to come in to us after the manner of all the earth.

Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. Mwanzo 19:32

Come, let's make our father drink wine, and we will lie with him, that we may preserve our father's seed."

Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Mwanzo 19:33

They made their father drink wine that night: and the firstborn went in, and lay with her father. He didn't know when she lay down, nor when she arose.

Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye. Mwanzo 19:34

It came to pass on the next day, that the firstborn said to the younger, "Behold, I lay last night with my father. Let us make him drink wine again, tonight. You go in, and lie with him, that we may preserve our father's seed."

Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Mwanzo 19:35

They made their father drink wine that night also. The younger arose, and lay with him. He didn't know when she lay down, nor when she arose.

Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. Mwanzo 19:36

Thus both of Lot's daughters were with child by their father.

Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo. Mwanzo 19:37

The firstborn bore a son, and named him Moab. The same is the father of the Moabites to this day.

Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo. Mwanzo 19:38

The younger also bore a son, and called his name Ben Ammi. The same is the father of the children of Ammon to this day.