Mwanzo 22 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 22 (Swahili) Genesis 22 (English)

Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Mwanzo 22:1

It happened after these things, that God tested Abraham, and said to him, "Abraham!" He said, "Here I am."

Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia. Mwanzo 22:2

He said, "Now take your son, your only son, whom you love, even Isaac, and go into the land of Moriah. Offer him there for a burnt offering on one of the mountains which I will tell you of."

Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu. Mwanzo 22:3

Abraham rose early in the morning, and saddled his donkey, and took two of his young men with him, and Isaac his son. He split the wood for the burnt offering, and rose up, and went to the place of which God had told him.

Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake, akapaona mahali pakali mbali. Mwanzo 22:4

On the third day Abraham lifted up his eyes, and saw the place far off.

Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena. Mwanzo 22:5

Abraham said to his young men, "Stay here with the donkey. The boy and I will go yonder. We will worship, and come back to you.

Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja. Mwanzo 22:6

Abraham took the wood of the burnt offering and laid it on Isaac his son. He took in his hand the fire and the knife. They both went together.

Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? Mwanzo 22:7

Isaac spoke to Abraham his father, and said, "My father?" He said, "Here I am, my son." He said, "Here is the fire and the wood, but where is the lamb for a burnt offering?"

Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja. Mwanzo 22:8

Abraham said, "God will provide himself the lamb for a burnt offering, my son." So they both went together.

Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. Mwanzo 22:9

They came to the place which God had told him of. Abraham built the altar there, and laid the wood in order, bound Isaac his son, and laid him on the altar, on the wood.

Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe. Mwanzo 22:10

Abraham stretched forth his hand, and took the knife to kill his son.

Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Mwanzo 22:11

The angel of Yahweh called to him out of the sky, and said, "Abraham, Abraham!" He said, "Here I am."

Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee. Mwanzo 22:12

He said, "Don't lay your hand on the boy, neither do anything to him. For now I know that you fear God, seeing you have not withheld your son, your only son, from me."

Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. Mwanzo 22:13

Abraham lifted up his eyes, and looked, and saw that behind him was a ram caught in the thicket by his horns. Abraham went and took the ram, and offered him up for a burnt offering instead of his son.

Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,kama watu wasemavyo hata leo,Katika mlima wa BWANA itapatikana. Mwanzo 22:14

Abraham called the name of that place Yahweh-Jireh.{"Yahweh-Jireh" means "Yahweh is my provider."} As it is said to this day, "In Yahweh's mountain it will be provided.

Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni Mwanzo 22:15

The angel of Yahweh called to Abraham a second time out of the sky,

akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, Mwanzo 22:16

and said, "I have sworn by myself, says Yahweh, because you have done this thing, and have not withheld your son, your only son,

katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; Mwanzo 22:17

that in blessing I will bless you, and in multiplying I will multiply your seed as the stars of the heavens, and as the sand which is on the seashore. Your seed will possess the gate of his enemies.

na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu. Mwanzo 22:18

In your seed will all the nations of the earth be blessed, because you have obeyed my voice."

Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba. Mwanzo 22:19

So Abraham returned to his young men, and they rose up and went together to Beersheba. Abraham lived at Beersheba.

Ikawa baada ya mambo hayo, Ibrahimu akaambiwa ya kwamba, Tazama, Milka naye amemzalia Nahori ndugu yako wana; Mwanzo 22:20

It happened after these things, that it was told Abraham, saying, "Behold, Milcah, she also has borne children to your brother Nahor:

Usi, mzaliwa wa kwanza wake, na Buzi nduguye, na Kemueli, baba wa Aramu; Mwanzo 22:21

Uz his firstborn, Buz his brother, Kemuel the father of Aram,

na Kesedi, na Hazo, na Pildashi, na Yidlafu, na Bethueli. Mwanzo 22:22

Chesed, Hazo, Pildash, Jidlaph, and Bethuel."

Bethueli akamzaa Rebeka; hao wanane Milka alimzalia Nahori ndugu wa Ibrahimu. Mwanzo 22:23

Bethuel became the father of Rebekah. These eight Milcah bore to Nahor, Abraham's brother.

Na suria wake Reuma naye alizaa Teba na Gahamu na Tahashi na Maaka. Mwanzo 22:24

His concubine, whose name was Reumah, also bare Tebah, Gaham, Tahash, and Maacah.