Mwanzo 35 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 35 (Swahili) Genesis 35 (English)

Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako. Mwanzo 35:1

God said to Jacob, "Arise, go up to Bethel, and live there. Make there an altar to God, who appeared to you when you fled from the face of Esau your brother."

Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu. Mwanzo 35:2

Then Jacob said to his household, and to all who were with him, "Put away the foreign gods that are among you, purify yourselves, change your garments.

Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea. Mwanzo 35:3

Let us arise, and go up to Bethel. I will make there an altar to God, who answered me in the day of my distress, and was with me in the way which I went."

Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu. Mwanzo 35:4

They gave to Jacob all the foreign gods which were in their hands, and the rings which were in their ears; and Jacob hid them under the oak which was by Shechem.

Wakashika njia, hofu ya Mungu ikaishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana wa Yakobo. Mwanzo 35:5

They traveled: and a terror of God was on the cities that were round about them, and they didn't pursue the sons of Jacob.

Basi Yakobo akafika Luzu, ulio katika nchi ya Kanaani, ndio Betheli, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye. Mwanzo 35:6

So Jacob came to Luz, which is in the land of Canaan (the same is Bethel), he and all the people who were with him.

Akajenga huko madhabahu, akapaita mahali pale, El-Betheli; kwa sababu huko Mungu alimtokea, hapo alipomkimbia ndugu yake. Mwanzo 35:7

He built an altar there, and called the place El Beth El; because there God was revealed to him, when he fled from the face of his brother.

Akafa Debora mlezi wa Rebeka, akazikwa chini ya Betheli, chini ya mwaloni; na jina lake likaitwa Alon-bakuthi. Mwanzo 35:8

Deborah, Rebekah's nurse, died, and she was buried below Bethel under the oak; and the name of it was called Allon Bacuth.

Mungu akamtokea Yakobo tena, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki. Mwanzo 35:9

God appeared to Jacob again, when he came from Paddan Aram, and blessed him.

Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli. Mwanzo 35:10

God said to him, "Your name is Jacob. Your name shall not be Jacob any more, but your name will be Israel." He named him Israel.

Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako. Mwanzo 35:11

God said to him, "I am God Almighty. Be fruitful and multiply. A nation and a company of nations will be from you, and kings will come out of your loins.

Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo. Mwanzo 35:12

The land which I gave to Abraham and Isaac, I will give it to you, and to your seed after you will I give the land."

Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye. Mwanzo 35:13

God went up from him in the place where he spoke with him.

Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake. Mwanzo 35:14

Jacob set up a pillar in the place where he spoke with him, a pillar of stone. He poured out a drink-offering on it, and poured oil on it.

Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli. Mwanzo 35:15

Jacob called the name of the place where God spoke with him "Bethel."

Wakasafiri kutoka Betheli, hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito. Mwanzo 35:16

They traveled from Bethel. There was still some distance to come to Ephrath, and Rachel travailed. She had hard labor.

Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine. Mwanzo 35:17

It happened that, when she was in hard labor, that the midwife said to her, "Don't be afraid, for now you will have another son."

Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini. Mwanzo 35:18

It happened, as her soul was departing (for she died), that she named him Ben-oni,{"Ben-oni" means "son of my trouble."} but his father named him Benjamin.{"Benjamin" means "son of my right hand."}

Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu. Mwanzo 35:19

Rachel died, and was buried in the way to Ephrath (the same is Bethlehem).

Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo. Mwanzo 35:20

Jacob set up a pillar on her grave. The same is the Pillar of Rachel's grave to this day.

Kisha akasafiri Israeli akapiga hema yake upande wa pili wa mnara wa Ederi. Mwanzo 35:21

Israel traveled, and spread his tent beyond the tower of Eder.

Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili. Mwanzo 35:22

It happened, while Israel lived in that land, that Reuben went and lay with Bilhah, his father's concubine, and Israel heard of it. Now the sons of Jacob were twelve.

Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni. Mwanzo 35:23

The sons of Leah: Reuben (Jacob's firstborn), Simeon, Levi, Judah, Issachar, and Zebulun.

Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini. Mwanzo 35:24

The sons of Rachel: Joseph and Benjamin.

Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali. Mwanzo 35:25

The sons of Bilhah (Rachel's handmaid): Dan and Naphtali.

Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu. Mwanzo 35:26

The sons of Zilpah (Leah's handmaid): Gad and Asher. These are the sons of Jacob, who were born to him in Paddan Aram.

Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Ibrahimu na Isaka. Mwanzo 35:27

Jacob came to Isaac his father, to Mamre, to Kiriath Arba (the same is Hebron), where Abraham and Isaac lived as foreigners.

Siku za Isaka zilikuwa miaka mia na themanini. Mwanzo 35:28

The days of Isaac were one hundred eighty years.

Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika Mwanzo 35:29

Isaac gave up the spirit, and died, and was gathered to his people, old and full of days. Esau and Jacob, his sons, buried him.