Mwanzo 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 16 (Swahili) Genesis 16 (English)

Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. Mwanzo 16:1

Now Sarai, Abram's wife, bore him no children. She had a handmaid, an Egyptian, whose name was Hagar.

Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. Mwanzo 16:2

Sarai said to Abram," See now, Yahweh has restrained me from bearing. Please go in to my handmaid. It may be that I will obtain children by her." Abram listened to the voice of Sarai.

Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe. Mwanzo 16:3

Sarai, Abram's wife, took Hagar the Egyptian, her handmaid, after Abram had lived ten years in the land of Canaan, and gave her to Abram her husband to be his wife.

Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake. Mwanzo 16:4

He went in to Hagar, and she conceived. When she saw that she had conceived, her mistress was despised in her eyes.

Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe. Mwanzo 16:5

Sarai said to Abram, "This wrong is your fault. I gave my handmaid into your bosom, and when she saw that she had conceived, I was despised in her eyes. Yahweh judge between me and you."

Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake. Mwanzo 16:6

But Abram said to Sarai, "Behold, your maid is in your hand. Do to her whatever is good in your eyes." Sarai dealt harshly with her, and she fled from her face.

Malaika wa Bwana akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri. Mwanzo 16:7

The angel of Yahweh found her by a fountain of water in the wilderness, by the fountain in the way to Shur.

Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai. Mwanzo 16:8

He said, "Hagar, Sarai's handmaid, where did you come from? Where are you going?" She said, "I am fleeing from the face of my mistress Sarai."

Malaika wa Bwana akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake. Mwanzo 16:9

The angel of Yahweh said to her, "Return to your mistress, and submit yourself under her hands."

Malaika wa Bwana akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi. Mwanzo 16:10

The angel of Yahweh said to her, "I will greatly multiply your seed, that they will not be numbered for multitude."

Malaika wa Bwana akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana Bwana amesikia kilio cha mateso yako. Mwanzo 16:11

The angel of Yahweh said to her, "Behold, you are with child, and will bear a son. You shall call his name Ishmael, because Yahweh has heard your affliction.

Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote. Mwanzo 16:12

He will be like a wild donkey among men. His hand will be against every man, and every man's hand against him. He will live opposite all of his brothers."

Akaliita jina la Bwana aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye? Mwanzo 16:13

She called the name of Yahweh who spoke to her, "You are a God who sees," for she said, "Have I even stayed alive after seeing him?"

Kwa hiyo kisima kile kiliitwa Beer-lahai-roi.Tazama,kiko kati ya kadeshi na beredi. Mwanzo 16:14

Therefore the well was called Beer Lahai Roi.{Beer Lahai Roi means "well of the one who lives and sees me."} Behold, it is between Kadesh and Bered.

Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa. Mwanzo 16:15

Hagar bore a son for Abram. Abram called the name of his son, whom Hagar bore, Ishmael.

Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita, hapo Hajiri alipomzalia Abramu Ishmaeli.

Mwanzo 16:16

Abram was eighty-six years old, when Hagar bore Ishmael to Abram.