Mwanzo 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 9 (Swahili) Genesis 9 (English)

Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi. Mwanzo 9:1

God blessed Noah and his sons, and said to them, "Be fruitful, and multiply, and replenish the earth.

Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu. Mwanzo 9:2

The fear of you and the dread of you will be on every animal of the earth, and on every bird of the sky. Everything that the ground teems with, and all the fish of the sea are delivered into your hand.

Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. Mwanzo 9:3

Every moving thing that lives will be food for you. As the green herb, I have given everything to you.

Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile. Mwanzo 9:4

But flesh with the life of it, the blood of it, you shall not eat.

Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu. Mwanzo 9:5

I will surely require your blood of your lives. At the hand of every animal I will require it. At the hand of man, even at the hand of every man's brother, I will require the life of man.

Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu. Mwanzo 9:6

Whoever sheds man's blood, by man will his blood be shed, for in the image of God made he man.

Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake. Mwanzo 9:7

Be fruitful, and multiply. Bring forth abundantly in the earth, and multiply in it."

Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema, Mwanzo 9:8

God spoke to Noah, and to his sons with him, saying,

Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu; Mwanzo 9:9

"As for me, behold, I establish my covenant with you, and with your offspring after you,

tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi. Mwanzo 9:10

and with every living creature that is with you: the birds, the cattle, and every animal of the earth with you. Of all that go out of the ark, even every animal of the earth.

Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi. Mwanzo 9:11

I will establish my covenant with you; neither will all flesh be cut off any more by the waters of the flood; neither will there any more be a flood to destroy the earth."

Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mwanzo 9:12

God said, "This is the token of the covenant which I make between me and you and every living creature that is with you, for perpetual generations:

Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Mwanzo 9:13

I set my rainbow in the cloud, and it will be for a sign of a covenant between me and the earth.

Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni, Mwanzo 9:14

It will happen, when I bring a cloud over the earth, that the rainbow will be seen in the cloud,

nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. Mwanzo 9:15

and I will remember my covenant, which is between me and you and every living creature of all flesh, and the waters will no more become a flood to destroy all flesh.

Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi. Mwanzo 9:16

The rainbow will be in the cloud. I will look at it, that I may remember the everlasting covenant between God and every living creature of all flesh that is on the earth."

Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi. Mwanzo 9:17

God said to Noah, "This is the token of the covenant which I have established between me and all flesh that is on the earth."

Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani. Mwanzo 9:18

The sons of Noah who went forth from the ark were Shem, Ham, and Japheth. Ham is the father of Canaan.

Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu. Mwanzo 9:19

These three were the sons of Noah, and from these, the whole earth was populated.

Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; Mwanzo 9:20

Noah began to be a farmer, and planted a vineyard.

akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Mwanzo 9:21

He drank of the wine, and got drunk. He was uncovered within his tent.

Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Mwanzo 9:22

Ham, the father of Canaan, saw the nakedness of his father, and told his two brothers outside.

Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Mwanzo 9:23

Shem and Japheth took a garment, and laid it on both their shoulders, went in backwards, and covered the nakedness of their father. Their faces were backwards, and they didn't see their father's nakedness.

Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea. Mwanzo 9:24

Noah awoke from his wine, and knew what his youngest son had done to him.

Akasema,Na alaaniwe Kaanani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake. Mwanzo 9:25

He said, "Cursed be Canaan; A servant of servants will he be to his brothers."

Akasema,Na atukuzwe Bwana,Mungu wa Shemu;Na kaanani awe mtumwa wake. Mwanzo 9:26

He said, "Blessed be Yahweh, the God of Shem; Let Canaan be his servant.

Mungu akamnafisishe Yafethi,Na akae katika hema za Shemu; Na kaanani awe mtumwa wake. Mwanzo 9:27

God enlarge Japheth, Let him dwell in the tents of Shem; Let Canaan be his servant."

Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini. Mwanzo 9:28

Noah lived three hundred fifty years after the flood.

Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.

Mwanzo 9:29

All the days of Noah were nine hundred fifty years, then he died.