Mwanzo 46 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 46 (Swahili) Genesis 46 (English)

Akasafiri Israeli, pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye. Mwanzo 46:1

Israel traveled with all that he had, and came to Beersheba, and offered sacrifices to the God of his father, Isaac.

Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa. Mwanzo 46:2

God spoke to Israel in the visions of the night, and said, "Jacob, Jacob!" He said, "Here I am."

Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko. Mwanzo 46:3

He said, "I am God, the God of your father. Don't be afraid to go down into Egypt; for there I will make of you a great nation.

Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako. Mwanzo 46:4

I will go down with you into Egypt. I will also surely bring you up again. Joseph will close your eyes."

Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua. Mwanzo 46:5

Jacob rose up from Beersheba, and the sons of Israel carried Jacob, their father, their little ones, and their wives, in the wagons which Pharaoh had sent to carry him.

Wakatwaa na wanyama wao, na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani, wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye. Mwanzo 46:6

They took their cattle, and their goods, which they had gotten in the land of Canaan, and came into Egypt-- Jacob, and all his seed with him,

Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri. Mwanzo 46:7

his sons, and his sons' sons with him, his daughters, and his sons' daughters, and he brought all his seed with him into Egypt.

Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli walioingia Misri, Yakobo na wanawe: Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. Mwanzo 46:8

These are the names of the children of Israel, who came into Egypt, Jacob and his sons: Reuben, Jacob's firstborn.

Na wana wa Reubeni; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi. Mwanzo 46:9

The sons of Reuben: Hanoch, Pallu, Hezron, and Carmi.

Na wana wa Simeoni; Yemueli na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli, mwana wa mwanamke Mkanaani. Mwanzo 46:10

The sons of Simeon: Jemuel, Jamin, Ohad, Jachin, Zohar, and Shaul the son of a Canaanite woman.

Na wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari. Mwanzo 46:11

The sons of Levi: Gershon, Kohath, and Merari.

Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli. Mwanzo 46:12

The sons of Judah: Er, Onan, Shelah, Perez, and Zerah; but Er and Onan died in the land of Canaan. The sons of Perez were Hezron and Hamul.

Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni. Mwanzo 46:13

The sons of Issachar: Tola, Puvah, Iob, and Shimron.

Na wana wa Zabuloni; Seredi, na Eloni, na Yaleeli. Mwanzo 46:14

The sons of Zebulun: Sered, Elon, and Jahleel.

Hao ndio wana wa Lea, aliomzalia Yakobo katika Padan-aramu, na Dina, binti yake. Nafsi zote za wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu. Mwanzo 46:15

These are the sons of Leah, whom she bore to Jacob in Paddan Aram, with his daughter Dinah. All the souls of his sons and his daughters were thirty-three.

Na wana wa Gadi; Sefoni, na Hagi, na Shuni, na Esboni, na Eri, na Arodi, na Areli. Mwanzo 46:16

The sons of Gad: Ziphion, Haggi, Shuni, Ezbon, Eri, Arodi, and Areli.

Na wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na Sera, umbu lao. Na wana wa Beria ni Heberi, na Malkieli. Mwanzo 46:17

The sons of Asher: Imnah, Ishvah, Ishvi, Beriah, and Serah their sister. The sons of Beriah: Heber and Malchiel.

Hao ndio wana wa Zilpa, ambaye Labani alimpa Lea, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao, nafsi kumi na sita. Mwanzo 46:18

These are the sons of Zilpah, whom Laban gave to Leah, his daughter, and these she bore to Jacob, even sixteen souls.

Wana wa Raheli, mkewe Yakobo Yusufu na Benyamini. Mwanzo 46:19

The sons of Rachel, Jacob's wife: Joseph and Benjamin.

Walizaliwa kwake Yusufu katika nchi ya Misri, Manase na Efraimu, aliomzalia Asenathi binti Potifera, kuhani wa Oni. Mwanzo 46:20

To Joseph in the land of Egypt were born Manasseh and Ephraim, whom Asenath, the daughter of Potiphera, priest of On, bore to him.

Na wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Ashbeli, na Gera, na Naamani, na Ehi, na Roshi, na Mupimu, na Hupimu, na Ardi. Mwanzo 46:21

The sons of Benjamin: Bela, Becher, Ashbel, Gera, Naaman, Ehi, Rosh, Muppim, Huppim, and Ard.

Hao ndio wana wa Raheli, aliomzalia Yakobo, nafsi zote walikuwa kumi na wanne. Mwanzo 46:22

These are the sons of Rachel, who were born to Jacob: all the souls were fourteen.

Na wana wa Dani; Hushimu. Mwanzo 46:23

The son of Dan: Hushim.

Na wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yaseri, na Shilemu. Mwanzo 46:24

The sons of Naphtali: Jahzeel, Guni, Jezer, and Shillem.

Hao ndio wana wa Bilha, ambaye Labani alimpa Raheli, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao; nafsi zote walikuwa saba. Mwanzo 46:25

These are the sons of Bilhah, whom Laban gave to Rachel, his daughter, and these she bore to Jacob: all the souls were seven.

Nafsi zote waliokuja pamoja na Yakobo mpaka Misri waliotoka viunoni mwake, bila wake za wanawe Yakobo, nafsi zote walikuwa sitini na sita. Mwanzo 46:26

All the souls who came with Jacob into Egypt, who were his direct descendants, besides Jacob's sons' wives, all the souls were sixty-six.

Na wana wa Yusufu aliozaliwa katika Misri walikuwa nafsi wawili. Nafsi zote za nyumba ya Yakobo walioingia Misri walikuwa sabini. Mwanzo 46:27

The sons of Joseph, who were born to him in Egypt, were two souls. All the souls of the house of Jacob, who came into Egypt, were seventy.

Yakobo akampeleka Yuda mbele yake kwa Yusufu, ili amwongoze njia mpaka Gosheni. Wakaja mpaka nchi ya Gosheni. Mwanzo 46:28

He sent Judah before him to Joseph, to show the way before him to Goshen, and they came into the land of Goshen.

Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionyesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kizima. Mwanzo 46:29

Joseph made ready his chariot, and went up to meet Israel, his father, in Goshen. He presented himself to him, and fell on his neck, and wept on his neck a good while.

Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai. Mwanzo 46:30

Israel said to Joseph, "Now let me die, since I have seen your face, that you are still alive."

Yusufu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, Nitapanda mimi nimpashe Farao habari; nitamwambia, Ndugu zangu, na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa katika nchi ya Kanaani, wamenijia. Mwanzo 46:31

Joseph said to his brothers, and to his father's house, "I will go up, and speak with Pharaoh, and will tell him, 'My brothers, and my father's house, who were in the land of Canaan, have come to me.

Na watu hao ni wachungaji, maana wamekuwa watu wa kuchunga wanyama, nao wameleta kondoo zao, na ng'ombe zao, na yote waliyo nayo. Mwanzo 46:32

These men are shepherds, for they have been keepers of cattle, and they have brought their flocks, and their herds, and all that they have.'

Itakuwa Farao atakapowaita, na kuwauliza, Kazi yenu ni nini? Mwanzo 46:33

It will happen, when Pharaoh summons you, and will say, 'What is your occupation?'

Semeni, Watumwa wako tumekuwa wachunga wanyama tangu ujana wetu, na hata leo, sisi, na baba zetu; mpate kukaa katika nchi ya Gosheni; maana kila mchunga wanyama ni chukizo kwa Wamisri. Mwanzo 46:34

that you shall say, 'Your servants have been keepers of cattle from our youth even until now, both we, and our fathers:' that you may dwell in the land of Goshen; for every shepherd is an abomination to the Egyptians."