Mwanzo 33 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 33 (Swahili) Genesis 33 (English)

Yakobo akainua macho yake, akaona, na tazama, Esau anakuja na watu mia nne pamoja naye. Akawagawanyia Lea, na Raheli, na wale vijakazi wawili, wana wao. Mwanzo 33:1

Jacob lifted up his eyes, and looked, and, behold, Esau was coming, and with him four hundred men. He divided the children between Leah, Rachel, and to the two handmaids.

Akawaweka hao vijakazi na wana wao mbele, na Lea na wanawe nyuma yao, na Raheli na Yusufu mwisho. Mwanzo 33:2

He put the handmaids and their children in front, Leah and her children after, and Rachel and Joseph at the rear.

Akapita mwenyewe mbele yao, akainama mpaka nchi mara saba, hata alipomkaribia ndugu yake. Mwanzo 33:3

He himself passed over in front of them, and bowed himself to the ground seven times, until he came near to his brother.

Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia. Mwanzo 33:4

Esau ran to meet him, embraced him, fell on his neck, kissed him, and they wept.

Akainua macho yake, akawaona wale wanawake na watoto, akauliza, Ni nani hawa walio pamoja nawe? Akasema, Ni watoto Mungu aliompa mtumwa wako kwa neema yake. Mwanzo 33:5

He lifted up his eyes, and saw the women and the children; and said, "Who are these with you?" He said, "The children whom God has graciously given your servant."

Ndipo wale vijakazi, na wana wao, wakakaribia wakainama. Mwanzo 33:6

Then the handmaids came near with their children, and they bowed themselves.

Lea naye, na wanawe, wakakaribia wakainama. Baadaye Yusufu na Raheli wakakaribia, wakainama. Mwanzo 33:7

Leah also and her children came near, and bowed themselves. After them, Joseph came near with Rachel, and they bowed themselves.

Akasema, Kundi hili lote nililolikuta, maana yake ni nini? Akasema, Kunipatia kibali machoni pa bwana wangu. Mwanzo 33:8

Esau said, "What do you mean by all this company which I met?" Jacob said, "To find favor in the sight of my lord."

Esau akasema, Ninayo tele, ndugu yangu, uliyo nayo na yawe yako. Mwanzo 33:9

Esau said, "I have enough, my brother; let that which you have be yours."

Yakobo akasema, Sivyo; kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, iwapo nimeona uso wako kama kuona uso wa Mungu, ukapendezwa nami. Mwanzo 33:10

Jacob said, "Please, no, if I have now found favor in your sight, then receive my present at my hand, because I have seen your face, as one sees the face of God, and you were pleased with me.

Pokea, tafadhali, mbaraka wangu, ulioletewa, kwa sababu Mungu amenineemesha, na kwa sababu ninavyo hivi vyote Akamshurutisha, naye akapokea. Mwanzo 33:11

Please take the gift that I brought to you; because God has dealt graciously with me, and because I have enough." He urged him, and he took it.

Kisha Esau akamwambia, Twende zetu, tusafiri, nami nitakutangulia. Mwanzo 33:12

Esau said, "Let us take our journey, and let us go, and I will go before you."

Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng'ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote. Mwanzo 33:13

Jacob said to him, "My lord knows that the children are tender, and that the flocks and herds with me have their young, and if they overdrive them one day, all the flocks will die.

Tafadhali bwana wangu na apite mbele ya mtumwa wake; nami nitawaongoza polepole kwa kadiri ya mwendo wa wanyama walio mbele yangu, na kwa kadiri ya mwendo wa watoto, hata nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri. Mwanzo 33:14

Please let my lord pass over before his servant: and I will lead on gently, according to the pace of the cattle that are before me and according to the pace of the children, until I come to my lord to Seir."

Esau akasema, Nikuachie, basi, baadhi ya watu walio pamoja nami. Akasema, Pana haja gani? Na nione kibali tu machoni pa bwana wangu. Mwanzo 33:15

Esau said, "Let me now leave with you some of the folk who are with me." He said, "Why? Let me find favor in the sight of my lord."

Basi Esau akarudi siku ile ile akishika njia yake mpaka Seiri. Mwanzo 33:16

So Esau returned that day on his way to Seir.

Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi. Mwanzo 33:17

Jacob traveled to Succoth, built himself a house, and made shelters for his cattle. Therefore the name of the place is called Succoth.{succoth means shelters or booths.}

Yakobo akaja kwa amani mpaka mji wa Shekemu, ulio katika nchi ya Kanaani, alipokuja kutoka Padan-aramu; akapiga kambi mbele ya huo mji. Mwanzo 33:18

Jacob came in peace to the city of Shechem, which is in the land of Canaan, when he came from Paddan Aram; and encamped before the city.

Akainunua sehemu ya nchi, alipopiga hema yake, kwa mkono wa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia vya fedha. Mwanzo 33:19

He bought the parcel of ground, where he had spread his tent, at the hand of the children of Hamor, Shechem's father, for one hundred pieces of money.

Akajenga huko madhabahu, akaiita, El-elohe-Israeli.

Mwanzo 33:20

He erected an altar there, and called it El Elohe Israel.{El Elohe Israel means "God, the God of Israel" or "The God of Israel is mighty."}