Mwanzo 36 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 36 (Swahili) Genesis 36 (English)

Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ndiye Edomu. Mwanzo 36:1

Now this is the history of the generations of Esau (the same is Edom).

Esau alitwaa binti za Kanaani, kuwa wakeze; Ada, binti Eloni, Mhiti, na Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, Mhivi; Mwanzo 36:2

Esau took his wives from the daughters of Canaan: Adah the daughter of Elon, the Hittite; and Oholibamah the daughter of Anah, the daughter of Zibeon, the Hivite;

na Basemathi, binti Ishmaeli, nduguye Nebayothi. Mwanzo 36:3

and Basemath, Ishmael's daughter, sister of Nebaioth.

Ada akamzalia Esau Elifazi; na Basemathi alizaa Reueli. Mwanzo 36:4

Adah bore to Esau Eliphaz. Basemath bore Reuel.

Oholibama alizaa Yeushi, na Yalamu, na Kora. Hao ndio wana wa Esau aliozaliwa katika nchi ya Kanaani. Mwanzo 36:5

Oholibamah bore Jeush, Jalam, and Korah. These are the sons of Esau, who were born to him in the land of Canaan.

Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng'ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye. Mwanzo 36:6

Esau took his wives, his sons, his daughters, and all the members of his household, with his cattle, all his animals, and all his possessions, which he had gathered in the land of Canaan, and went into a land away from his brother Jacob.

Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao. Mwanzo 36:7

For their substance was too great for them to dwell together, and the land of their travels couldn't bear them because of their cattle.

Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu. Mwanzo 36:8

Esau lived in the hill country of Seir. Esau is Edom.

Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri. Mwanzo 36:9

This is the history of the generations of Esau the father of the Edomites in the hill country of Seir:

Haya ndiyo majina ya wana wa Esau; Elifazi, mwana wa Ada mkewe Esau. Reuli, mwana wa Basemathi, mkewe Esau. Mwanzo 36:10

these are the names of Esau's sons: Eliphaz, the son of Adah, the wife of Esau; and Reuel, the son of Basemath, the wife of Esau.

Na wana wa Elifazi, ni Temani na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi. Mwanzo 36:11

The sons of Eliphaz were Teman, Omar, Zepho, and Gatam, and Kenaz.

Na Timna alikuwa suria wa Elifazi, mwana wa Esau; naye akamzalia Elifazi Amaleki. Hao ndio wana wa Ada, mkewe Esau. Mwanzo 36:12

Timna was concubine to Eliphaz, Esau's son; and she bore to Eliphaz Amalek. These are the sons of Adah, Esau's wife.

Na hawa ni wana wa Reueli, Nahathi, na Zera, na Shama na Miza. Hao walikuwa wana wa Basemathi, mkewe Esau. Mwanzo 36:13

These are the sons of Reuel: Nahath, Zerah, Shammah, and Mizzah. These were the sons of Basemath, Esau's wife.

Na hawa ni wana wa Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, mkewe Esau; akamzalia Esau, Yeushi, na Yalamu, na Kora. Mwanzo 36:14

These were the sons of Oholibamah, the daughter of Anah, the daughter of Zibeon, Esau's wife: she bore to Esau Jeush, Jalam, and Korah.

Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau; wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau; jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi, Mwanzo 36:15

These are the chiefs of the sons of Esau: the sons of Eliphaz the firstborn of Esau: chief Teman, chief Omar, chief Zepho, chief Kenaz,

jumbe Kora, jumbe Gatamu, jumbe Amaleki. Hao ndio majumbe, waliotoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Ada. Mwanzo 36:16

chief Korah, chief Gatam, chief Amalek: these are the chiefs who came of Eliphaz in the land of Edom; these are the sons of Adah.

Na hawa ni wana wa Reueli, mwanawe Esau; jumbe Nahathi, jumbe Zera, jumbe Shama, jumbe Miza. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Hao ni wana wa Basemathi, mkewe Esau. Mwanzo 36:17

These are the sons of Reuel, Esau's son: chief Nahath, chief Zerah, chief Shammah, chief Mizzah: these are the chiefs who came of Reuel in the land of Edom; these are the sons of Basemath, Esau's wife.

Na hawa ni wana wa Oholibama, mkewe Esau; jumbe Yeushi, jumbe Yalamu, jumbe Kora. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau. Mwanzo 36:18

These are the sons of Oholibamah, Esau's wife: chief Jeush, chief Jalam, chief Korah: these are the chiefs who came of Oholibamah the daughter of Anah, Esau's wife.

Hao ni wana wa Esau, na hao ndio majumbe wao; naye Esau ndiye Edomu. Mwanzo 36:19

These are the sons of Esau, and these are their chiefs. The same is Edom.

Hawa ni wana wa Seiri, Mhori, wenyeji wa nchi ile; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, Mwanzo 36:20

These are the sons of Seir the Horite, the inhabitants of the land: Lotan, Shobal, Zibeon, Anah,

na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, wana wa Seiri, katika nchi ya Edomu. Mwanzo 36:21

Dishon, Ezer, and Dishan. These are the chiefs who came of the Horites, the children of Seir in the land of Edom.

Na wana wa Lotani, ni Hori, na Hemamu; na umbu lake Lotani ni Timna. Mwanzo 36:22

The children of Lotan were Hori and Heman. Lotan's sister was Timna.

Na hawa ni wana wa Shobali, Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Mwanzo 36:23

These are the children of Shobal: Alvan, Manahath, Ebal, Shepho, and Onam.

Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye. Mwanzo 36:24

These are the children of Zibeon: Aiah and Anah. This is Anah who found the hot springs in the wilderness, as he fed the donkeys of Zibeon his father.

Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana. Mwanzo 36:25

These are the children of Anah: Dishon and Oholibamah, the daughter of Anah.

Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. Mwanzo 36:26

These are the children of Dishon: Hemdan, Eshban, Ithran, and Cheran.

Na hawa ni wana wa Eseri, Bilhani, na Zaawani, na Akani. Mwanzo 36:27

These are the children of Ezer: Bilhan, Zaavan, and Akan.

Na hawa ni wana wa Dishani, Usi, na Arani. Mwanzo 36:28

These are the children of Dishan: Uz and Aran.

Hawa ndio majumbe waliotoka katika Wahori; jumbe Lotani, jumbe Shobali, jumbe Sibeoni, jumbe Ana, Mwanzo 36:29

These are the chiefs who came of the Horites: chief Lotan, chief Shobal, chief Zibeon, chief Anah,

jumbe Dishoni, jumbe Eseri jumbe Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, kwa habari za majumbe yao, katika nchi ya Seiri. Mwanzo 36:30

chief Dishon, chief Ezer, and chief Dishan: these are the chiefs who came of the Horites, according to their chiefs in the land of Seir.

Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli. Mwanzo 36:31

These are the kings who reigned in the land of Edom, before any king reigned over the children of Israel.

Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba. Mwanzo 36:32

Bela, the son of Beor, reigned in Edom. The name of his city was Dinhabah.

Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake. Mwanzo 36:33

Bela died, and Jobab, the son of Zerah of Bozrah, reigned in his place.

Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake. Mwanzo 36:34

Jobab died, and Husham of the land of the Temanites reigned in his place.

Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi. Mwanzo 36:35

Husham died, and Hadad, the son of Bedad, who struck Midian in the field of Moab, reigned in his place. The name of his city was Avith.

Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake. Mwanzo 36:36

Hadad died, and Samlah of Masrekah reigned in his place.

Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake. Mwanzo 36:37

Samlah died, and Shaul of Rehoboth by the river, reigned in his place.

Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake. Mwanzo 36:38

Shaul died, and Baal Hanan, the son of Achbor reigned in his place.

Akafa Baal-hanani, mwana wa Akbori, akamiliki Hadadi badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. Mwanzo 36:39

Baal Hanan the son of Achbor died, and Hadar reigned in his place. The name of his city was Pau. His wife's name was Mehetabel, the daughter of Matred, the daughter of Me-zahab.

Na hayo ndiyo majina ya majumbe waliotoka kwa Esau, kufuata jamaa zao, na mahali pao, kwa majina yao. Jumbe Timna, jumbe Alva, jumbe Yethethi, Mwanzo 36:40

These are the names of the chiefs who came from Esau, according to their families, after their places, and by their names: chief Timna, chief Alvah, chief Jetheth,

jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni, Mwanzo 36:41

chief Oholibamah, chief Elah, chief Pinon,

jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibsari, Mwanzo 36:42

chief Kenaz, chief Teman, chief Mibzar,

jumbe Magdieli, jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu, kufuata makao yao, katika nchi ya mamlaka yao. Naye huyo ndiye Esau, baba ya Edomu.

Mwanzo 36:43

chief Magdiel, and chief Iram. These are the chiefs of Edom, according to their habitations in the land of their possession. This is Esau, the father of the Edomites.