Mwanzo 37 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 37 (Swahili) Genesis 37 (English)

Yakobo akakaa katika nchi aliyosafiri baba yake, katika nchi ya Kanaani. Mwanzo 37:1

Jacob lived in the land of his father's travels, in the land of Canaan.

Hivi ndivyo vizazi vya Yakobo. Yusufu, aliyekuwa mwenye miaka kumi na saba, alikuwa akichunga kondoo pamoja na ndugu zake; naye alikuwa kijana pamoja na wana wa Bilha, na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya. Mwanzo 37:2

This is the history of the generations of Jacob. Joseph, being seventeen years old, was feeding the flock with his brothers. He was a boy with the sons of Bilhah and Zilpah, his father's wives. Joseph brought an evil report of them to their father.

Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu. Mwanzo 37:3

Now Israel loved Joseph more than all his children, because he was the son of his old age, and he made him a coat of many colors.

Ndugu zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia, wala hawakuweza kusema naye kwa amani. Mwanzo 37:4

His brothers saw that their father loved him more than all his brothers, and they hated him, and couldn't speak peaceably to him.

Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia; Mwanzo 37:5

Joseph dreamed a dream, and he told it to his brothers, and they hated him all the more.

akawaambia, Tafadhalini, sikieni ndoto hii niliyoiota. Mwanzo 37:6

He said to them, "Please hear this dream which I have dreamed:

Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu. Mwanzo 37:7

for, behold, we were binding sheaves in the field, and behold, my sheaf arose and also stood upright; and behold, your sheaves came around, and bowed down to my sheaf."

Ndugu zake wakamwambia, Je! Kweli wewe utatumiliki sisi? Nawe utatutawala sisi? Wakazidi kumchukia kwa ajili ya ndoto yake, na kwa maneno yake. Mwanzo 37:8

His brothers said to him, "Will you indeed reign over us? Or will you indeed have dominion over us?" They hated him all the more for his dreams and for his words.

Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia. Mwanzo 37:9

He dreamed yet another dream, and told it to his brothers, and said, "Behold, I have dreamed yet another dream: and behold, the sun and the moon and eleven stars bowed down to me."

Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi? Mwanzo 37:10

He told it to his father and to his brothers. His father rebuked him, and said to him, "What is this dream that you have dreamed? Will I and your mother and your brothers indeed come to bow ourselves down to you to the earth?"

Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili. Mwanzo 37:11

His brothers envied him; but his father kept this saying in mind.

Ndugu zake wakaenda kuchunga kondoo za baba yao huko Shekemu. Mwanzo 37:12

His brothers went to feed their father's flock in Shechem.

Israeli akamwambia Yusufu, Je! Ndugu zako hawachungi kondoo katika Shekemu? Njoo, nikutume kwao. Akamwambia, Mimi hapa. Mwanzo 37:13

Israel said to Joseph, "Aren't your brothers feeding the flock in Shechem? Come, and I will send you to them." He said to him, "Here I am."

Akamwambia, Enenda, basi, ukaone kama ndugu zako hawajambo, na kundi nalo li salama, ukaniletee habari. Basi akampeleka kutoka bonde la Hebroni, akafika Shekemu. Mwanzo 37:14

He said to him, "Go now, see whether it is well with your brothers, and well with the flock; and bring me word again." So he sent him out of the valley of Hebron, and he came to Shechem.

Mtu mmoja akamkuta, naye alikuwa anazunguka-zunguka katika nyika; yule mtu akamwuliza, akisema, Unatafuta nini? Mwanzo 37:15

A certain man found him, and behold, he was wandering in the field: and the man asked him, saying, "What are you looking for?"

Akasema, Nawatafuta ndugu zangu; tafadhali uniambie mahali wanakochunga. Mwanzo 37:16

He said, "I am looking for my brothers. Tell me, please, where they are feeding the flock."

Yule mtu akasema, Wametoka hapa, maana niliwasikia wakisema, Twendeni Dothani. Basi Yusufu akawafuata ndugu zake akawakuta huko Dothani. Mwanzo 37:17

The man said, "They have left here, for I heard them say, 'Let us go to Dothan.'" Joseph went after his brothers, and found them in Dothan.

Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. Mwanzo 37:18

They saw him afar off, and before he came near to them, they conspired against him to kill him.

Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja. Mwanzo 37:19

They said one to another, "Behold, this dreamer comes.

Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake. Mwanzo 37:20

Come now therefore, and let's kill him, and cast him into one of the pits, and we will say, 'An evil animal has devoured him.' We will see what will become of his dreams."

Reubeni akasikia akamwokoa katika mikono yao, akasema, Tusimwue. Mwanzo 37:21

Reuben heard it, and delivered him out of their hand, and said, "Let's not take his life."

Reubeni akawaambia, Msimwage damu; mtupeni katika birika hii iliyopo nyikani, wala msimguse; ili apate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake. Mwanzo 37:22

Reuben said to them, "Shed no blood. Throw him into this pit that is in the wilderness, but lay no hand on him"-- that he might deliver him out of their hand, to restore him to his father.

Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, Mwanzo 37:23

It happened, when Joseph came to his brothers, that they stripped Joseph of his coat, the coat of many colors that was on him;

wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji. Mwanzo 37:24

and they took him, and threw him into the pit. The pit was empty. There was no water in it.

Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri. Mwanzo 37:25

They sat down to eat bread, and they lifted up their eyes and looked, and saw a caravan of Ishmaelites was coming from Gilead, with their camels bearing spices and balm and myrrh, going to carry it down to Egypt.

Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? Mwanzo 37:26

Judah said to his brothers, "What profit is it if we kill our brother and conceal his blood?

Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. Mwanzo 37:27

Come, and let's sell him to the Ishmaelites, and not let our hand be on him; for he is our brother, our flesh." His brothers listened to him.

Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri. Mwanzo 37:28

Midianites who were merchants passed by, and they drew and lifted up Joseph out of the pit, and sold Joseph to the Ishmaelites for twenty pieces of silver. They brought Joseph into Egypt.

Akarudi Reubeni birikani, kumbe! Yusufu hayumo katika birika, akararua nguo zake. Mwanzo 37:29

Reuben returned to the pit; and saw that Joseph wasn't in the pit; and he tore his clothes.

Akarudi kwa ndugu zake, akasema, Mtoto hayuko, nami niende wapi? Mwanzo 37:30

He returned to his brothers, and said, "The child is no more; and I, where will I go?"

Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika damu. Mwanzo 37:31

They took Joseph's coat, and killed a male goat, and dipped the coat in the blood.

Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo. Mwanzo 37:32

They took the coat of many colors, and they brought it to their father, and said, "We have found this. Examine it, now, whether it is your son's coat or not."

Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa. Mwanzo 37:33

He recognized it, and said, "It is my son's coat. An evil animal has devoured him. Joseph is without doubt torn in pieces."

Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi. Mwanzo 37:34

Jacob tore his clothes, and put sackcloth on his loins, and mourned for his son many days.

Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia. Mwanzo 37:35

All his sons and all his daughters rose up to comfort him; but he refused to be comforted. He said, "For I will go down to Sheol{Sheol is the place of the dead or the grave.} to my son mourning." His father wept for him.

Nao Wamidiani wakamwuza huko Misri, kwa Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari.

Mwanzo 37:36

The Midianites sold him into Egypt to Potiphar, an officer of Pharaoh's, the captain of the guard.