Mwanzo 29 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 29 (Swahili) Genesis 29 (English)

Kisha Yakobo akashika njia yake, akafika nchi ya wana wa mashariki. Mwanzo 29:1

Then Jacob went on his journey, and came to the land of the children of the east.

Naye akaangalia, na tazama, kiko kisima kondeni, na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu nacho, kwa sababu katika kisima kile hunywesha makundi; na palikuwa na jiwe kubwa juu ya kinywa cha kisima. Mwanzo 29:2

He looked, and behold, a well in the field, and, behold, three flocks of sheep lying there by it. For out of that well they watered the flocks. The stone on the well's mouth was great.

Makundi yote hukusanyika huko, watu wakafingirisha hilo jiwe katika kinywa cha kisima wakawanywesha kondoo, na kulirudisha jiwe juu ya kinywa cha kisima mahali pake. Mwanzo 29:3

There all the flocks were gathered. They rolled the stone from the well's mouth, and watered the sheep, and put the stone again on the well's mouth in its place.

Yakobo akawauliza, Ndugu zangu, watu wa wapi ninyi? Wakasema, Tu wa Harani sisi. Mwanzo 29:4

Jacob said to them, "My relatives, where are you from?" They said, "We are from Haran."

Akawauliza, Je! Mnamjua Labani, mwana wa Nahori? Wakasema, Tunamjua. Mwanzo 29:5

He said to them, "Do you know Laban, the son of Nahor?" They said, "We know him."

Akawauliza, Je! Hajambo? Wakasema, Hajambo; tazama, Raheli binti yake anakuja na kondoo. Mwanzo 29:6

He said to them, "Is it well with him?" They said, "It is well. See, Rachel, his daughter, is coming with the sheep."

Akasema, Tazama, ukali mchana bado, wala sio wakati wa kukusanya wanyama; wanywesheni kondoo, mwende kuwalisha. Mwanzo 29:7

He said, "Behold, it is still the middle of the day, not time to gather the cattle together. Water the sheep, and go and feed them."

Wakasema, Hatuwezi, hata yakusanyike makundi yote, watu wakafingirishe jiwe katika kinywa cha kisima, ndipo tunapowanywesha kondoo. Mwanzo 29:8

They said, "We can't, until all the flocks are gathered together, and they roll the stone from the well's mouth. Then we water the sheep."

Hata alipokuwa akisema nao, Raheli akaja na kondoo za baba yake, maana aliwachunga. Mwanzo 29:9

While he was yet speaking with them, Rachel came with her father's sheep, for she kept them.

Ikawa Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mamaye, na kondoo za Labani, ndugu wa mamaye, Yakobo akakaribia, na kulifingirisha lile jiwe litoke katika kinywa cha kisima, akawanywesha kondoo za Labani, ndugu wa mamaye. Mwanzo 29:10

It happened, when Jacob saw Rachel the daughter of Laban, his mother's brother, and the sheep of Laban, his mother's brother, that Jacob went near, and rolled the stone from the well's mouth, and watered the flock of Laban his mother's brother.

Yakobo akambusu Raheli, akainua sauti yake akalia. Mwanzo 29:11

Jacob kissed Rachel, and lifted up his voice, and wept.

Yakobo akamwarifu Raheli ya kuwa yeye ni ndugu wa babaye, na ya kuwa ni mwana wa Rebeka. Basi akapiga mbio akampasha babaye habari. Mwanzo 29:12

Jacob told Rachel that he was her father's brother, and that he was Rebekah's son. She ran and told her father.

Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote. Mwanzo 29:13

It happened, when Laban heard the news of Jacob, his sister's son, that he ran to meet Jacob, and embraced him, and kissed him, and brought him to his house. Jacob told Laban all these things.

Labani akamwambia, Ndiwe kweli mfupa wangu na nyama yangu. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja. Mwanzo 29:14

Laban said to him, Surely you are my bone and my flesh. He lived with him for a month.

Labani akamwambia Yakobo, Kwa sababu wewe ni ndugu yangu, basi, je! Unitumikie bure? Niambie mshahara wako utakuwa nini? Mwanzo 29:15

Laban said to Jacob, "Because you are my brother, should you therefore serve me for nothing? Tell me, what will your wages be?"

Labani alikuwa na binti wawili, jina la mkubwa ni Lea, na jina la mdogo ni Raheli. Mwanzo 29:16

Laban had two daughters. The name of the elder was Leah, and the name of the younger was Rachel.

Naye Lea macho yake yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo, na mzuri uso. Mwanzo 29:17

Leah's eyes were weak, but Rachel was beautiful and well favored.

Yakobo akampenda Raheli akasema, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. Mwanzo 29:18

Jacob loved Rachel. He said, "I will serve you seven years for Rachel, your younger daughter."

Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. Mwanzo 29:19

Laban said, "It is better that I give her to you, than that I should give her to another man. Stay with me."

Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli. Ikawa machoni pake kama siku chache tu kwa vile alivyompenda. Mwanzo 29:20

Jacob served seven years for Rachel. They seemed to him but a few days, for the love he had for her.

Yakobo akamwambia Labani, Nipe mke wangu, maana siku zangu zimetimia; niingie kwake. Mwanzo 29:21

Jacob said to Laban, "Give me my wife, for my days are fulfilled, that I may go in to her."

Labani akakusanya watu wote wa mahali pale, akafanya karamu. Mwanzo 29:22

Laban gathered together all the men of the place, and made a feast.

Ikawa wakati wa jioni akamtwaa Lea, binti yake, akamletea Yakobo, naye akaingia kwake. Mwanzo 29:23

It happened in the evening, that he took Leah his daughter, and brought her to him. He went in to her.

Labani akampa Lea mjakazi wake Zilpa, awe mjakazi wake. Mwanzo 29:24

Laban gave Zilpah his handmaid to his daughter Leah for a handmaid.

Ikawa, kulipokuwa asubuhi, kumbe! Ni Lea. Akamwambia Labani, Nini hii uliyonitenda? Mwanzo 29:25

It happened in the morning that, behold, it was Leah. He said to Laban, "What is this you have done to me? Didn't I serve with you for Rachel? Why then have you deceived me?"

Sikukutumikia kwa Raheli? Mbona umenidanganya? Labani akasema, Havitendeki hivi kwetu, kumtoa mdogo kabla ya mkubwa; Mwanzo 29:26

Laban said, "It is not done so in our place, to give the younger before the first born.

timiza siku zake saba, nasi tutakupa huyu naye kwa utumishi utakaonitumikia, miaka saba mingine. Mwanzo 29:27

Fulfill the week of this one, and we will give you the other also for the service which you will serve with me yet seven other years."

Yakobo akafanya hivi, akatimiza siku zake saba. Naye akampa Raheli binti yake kuwa mkewe. Mwanzo 29:28

Jacob did so, and fulfilled her week. He gave him Rachel his daughter as wife.

Labani akampa binti yake Raheli mjakazi wake Bilha, awe mjakazi wake. Mwanzo 29:29

Laban gave to Rachel his daughter Bilhah, his handmaid, to be her handmaid.

Akaingia kwa Raheli naye, akampenda Raheli kuliko Lea, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine. Mwanzo 29:30

He went in also to Rachel, and he loved also Rachel more than Leah, and served with him yet seven other years.

Bwana akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai. Mwanzo 29:31

Yahweh saw that Leah was hated, and he opened her womb, but Rachel was barren.

Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa Bwana ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda. Mwanzo 29:32

Leah conceived, and bore a son, and she named him Reuben. For she said, "Because Yahweh has looked at my affliction. For now my husband will love me."

Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa Bwana amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni. Mwanzo 29:33

She conceived again, and bare a son, and said, "Because Yahweh has heard that I am hated, he has therefore given me this son also." She named him Simeon.

Akapata mimba tena, akazaa mwana, akasema, Basi wakati huu mume wangu ataungana nami, kwa sababu nimemzalia wana watatu. Kwa hiyo akamwita jina lake Lawi. Mwanzo 29:34

She conceived again, and bare a son. Said, "Now this time will my husband be joined to me, because I have borne him three sons." Therefore was his name called Levi.

Akapata mimba tena, akazaa mwana. Akasema, Mara hii nitamsifu Bwana; kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; akaacha kuzaa. Mwanzo 29:35

She conceived again, and bare a son. She said, "This time will I praise Yahweh." Therefore she named him Judah. Then she stopped bearing.