Sifa Lyrics

Mapambio by Rose Muhando cover art

Rose Muhando - Mapambio Lyrics

Artist:
Rose Muhando

Lyrics

Ukipata mia mbili shukuru Mungu
Hio ndio riziki yako
Kaa chini utulie imba mapambio
Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa


Wewe tulia mshukuru Mungu
Hio ndio riziki yako
Kaa chini utulie imba mapambio
Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa


Yatakutoa roho
Wacha kwenda mbio mbio
Usishindane na huyo
Wewe nenda pole pole, pole pole
Maisha ni pole pole, pole pole


Mungu ameumba dunia riziki mafungu saba
Wewe imba mapambio
Pengine la kwanza na la pili si lako
La kwako saba we, tulia imba mapambio


Wacha kutamani vitu vya wengine
Vinaumiza moyo
Wewe imba mapambio
Ridhika na ulicho nacho


Wewe tulia mshukuru Mungu
Hio ndio riziki yako
Kaa chini utulie imba mapambio
Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa


Ya watu yatakutoa nyongo
Unataka mapesa kama ya fulani utatoa wapi?
Wewe imba mapambio
Wataka utajiri kama wa fulani hujui alipataje?
Wewe imba mapambio


Fulani ana utajiri na hujui agano lako
Kama itakutoa nyongo
Mumeo kipato chake ni buku
Hafanani na fulani, mwombee imba mapambio
Wewe imba mapambio, shukuru Mungu
Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa


Ukipata mia mbili shukuru Mungu
Hio ndio riziki yako
Kaa chini utulie imba mapambio
Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa
Yatakutoa roho


Wataka mrembo wa gharama kama Wema Sepetu
Kwa kipato cha Harmo Rapa we yatakutoa nyongo
Chunga atakutoa roho


Mrembo ana level ya pizza
Kipato chako miguu ya kuku, chunga atakutoa roho
Wewe imba mapambio, shukuru Mungu
Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa


Dunia ina mambo, ina mambo
Vituko na vijambo na vijambo
Siri nyumba ya mgongo, ya mgongo
Usishindane na huyo


Ukipata mia mbili shukuru Mungu
Hio ndio riziki yako
Kaa chini utulie imba mapambio
Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa


Wewe tulia mshukuru Mungu
Hio ndio riziki yako
Kaa chini utulie imba mapambio
Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa


Video