Sifa Lyrics

Magufuli (Safiri Salama) by Bahati cover art

Bahati - Magufuli (Safiri Salama) Lyrics

Artist:
Bahati

Lyrics

Nina imani tutaonana tena
Tena mmmh


Ila yangu swali?
Mbona umeondoka mapema na haukusema
Jua linatua kila pande ni manjozi
Mwongoza njia umetuacha Magufuli
Nani ataitwa mlezi wa wasanii
Na simba amsifie?
Nani ataleta ndege Tanzania uchumi auinue


Aah mbona umetuacha
Aah bado mapema 
Aah..Magufuli safiri salama
Aah mbona umetuacha
Aah bado mapema 
Aah..Magufuli we safiri salama


Bado siamini hatutakuona tena
Kwanini baba yo umeondoka mapema
Msalimie baba Mzee Jomo Kenyatta
Mwambie Kenya imara mwanae anatawala
Aah na mzee Odinga naye mpe salamu
Mwanaye ni gwiji sasa mwambie atabasamu
Umtafute Mzee Moi, umkumbatie
Natamani maziwa ya Nyayo iturudie


Aah mbona umetuacha
Aah bado mapema 
Aah..Magufuli safiri salama
Aah mbona umetuacha
Aah bado mapema 
Aah..Magufuli we safiri salama


I wish ungejua siku barua ungetuandikia
Ila Mungu ndo anapanga pole kwa mama Samia
Rafiki yangu babu Tale chawa wako wanaumia
Swali mbona ni mapema Afrika inakulilia


Magu aah mbona umetuacha?
Aah bado mapema 
Aah..Magufuli we safiri salama
Aah mbona umetuacha?
Aah bado mapema 
Aah..Magufuli we safiri salama


Video