Hesabu 22 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 22 (Swahili) Numbers 22 (English)

Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu ya Yeriko. Hesabu 22:1

The children of Israel traveled, and encamped in the plains of Moab beyond the Jordan at Jericho.

Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli wamewatendea Waamori. Hesabu 22:2

Balak the son of Zippor saw all that Israel had done to the Amorites.

Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli. Hesabu 22:3

Moab was sore afraid of the people, because they were many: and Moab was distressed because of the children of Israel.

Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile. Hesabu 22:4

Moab said to the elders of Midian, Now will this multitude lick up all that is round about us, as the ox licks up the grass of the field. Balak the son of Zippor was king of Moab at that time.

Basi akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori, hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi. Hesabu 22:5

He sent messengers to Balaam the son of Beor, to Pethor, which is by the River, to the land of the children of his people, to call him, saying, Behold, there is a people come out from Egypt: behold, they cover the surface of the earth, and they abide over against me.

Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa. Hesabu 22:6

Please come now therefore curse me this people; for they are too mighty for me: peradventure I shall prevail, that we may strike them, and that I may drive them out of the land; for I know that he whom you bless is blessed, and he whom you curse is cursed.

Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikilia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki. Hesabu 22:7

The elders of Moab and the elders of Midian departed with the rewards of divination in their hand; and they came to Balaam, and spoke to him the words of Balak.

Akawaambia, Kaeni hapa usiku huu, nami nitawaletea jawabu kama Bwana atakavyoniambia; wakuu wa Moabu wakakaa na Balaamu. Hesabu 22:8

He said to them, Lodge here this night, and I will bring you word again, as Yahweh shall speak to me: and the princes of Moab abode with Balaam.

Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe? Hesabu 22:9

God came to Balaam, and said, What men are these with you?

Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema, Hesabu 22:10

Balaam said to God, Balak the son of Zippor, king of Moab, has sent to me, [saying],

Tazama, kuna watu waliotoka Misri, wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa; labda nitaweza kupigana nao, na kuwafukuza. Hesabu 22:11

Behold, the people that is come out of Egypt, it covers the surface of the earth: now, come curse me them; peradventure I shall be able to fight against them, and shall drive them out.

Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa. Hesabu 22:12

God said to Balaam, You shall not go with them; you shall not curse the people; for they are blessed.

Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Enendeni zenu hata nchi yenu; kwa maana Bwana amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi. Hesabu 22:13

Balaam rose up in the morning, and said to the princes of Balak, Get you into your land; for Yahweh refuses to give me leave to go with you.

Wakuu wakaondoka wakaenda kwa Balaki, wakasema, Balaamu, anakataa kuja pamoja nasi. Hesabu 22:14

The princes of Moab rose up, and they went to Balak, and said, Balaam refuses to come with us.

Basi Balaki akatuma wakuu mara ya pili, wengi zaidi, wenye cheo wakubwa kuliko wale wa kwanza. Hesabu 22:15

Balak sent yet again princes, more, and more honorable than they.

Wakamfikilia Balaamu, wakamwambia, Balaki mwana wa Sipori asema hivi, Nakusihi, neno lo lote lisikuzuie usinijie; Hesabu 22:16

They came to Balaam, and said to him, Thus says Balak the son of Zippor, Please let nothing hinder you from coming to me:

maana nitakufanyizia heshima nyingi sana, na neno lo lote utakaloniomba nitalitenda; basi njoo, nakusihi, unilaanie watu hawa. Hesabu 22:17

for I will promote you to very great honor, and whatever you say to me I will do. Please come therefore, and curse this people for me.

Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la Bwana, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza. Hesabu 22:18

Balaam answered the servants of Balak, If Balak would give me his house full of silver and gold, I can't go beyond the word of Yahweh my God, to do less or more.

Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua Bwana atakaloniambia zaidi. Hesabu 22:19

Now therefore, please wait also here this night, that I may know what Yahweh will speak to me more.

Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, enenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi. Hesabu 22:20

God came to Balaam at night, and said to him, If the men are come to call you, rise up, go with them; but only the word which I speak to you, that shall you do.

Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na wakuu wa Moabu. Hesabu 22:21

Balaam rose up in the morning, and saddled his donkey, and went with the princes of Moab.

Hasira ya Mungu ikawaka kwa sababu alikwenda; malaika wa Bwana akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye. Hesabu 22:22

God's anger was kindled because he went; and the angel of Yahweh placed himself in the way for an adversary against him. Now he was riding on his donkey, and his two servants were with him.

Na yule punda akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, na upanga wake mkononi mwake amekwisha kuufuta; punda akageuka upande ili kuiacha njia, akaingia shambani. Balaamu akampiga punda ili kumrejeza njiani. Hesabu 22:23

The donkey saw the angel of Yahweh standing in the way, with his sword drawn in his hand; and the donkey turned aside out of the way, and went into the field: and Balaam struck the donkey, to turn her into the way.

Kisha malaika wa Bwana akasimama mahali penye bonde, katikati ya mashamba ya mizabibu, tena penye kitalu upande huu na kitalu upande huu. Hesabu 22:24

Then the angel of Yahweh stood in a narrow path between the vineyards, a wall being on this side, and a wall on that side.

Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajisonga ukutani, akamseta Balaamu mguu wake, basi akampiga mara ya pili. Hesabu 22:25

The donkey saw the angel of Yahweh, and she thrust herself to the wall, and crushed Balaam's foot against the wall: and he struck her again.

Malaika wa Bwana akaendelea mbele akasimama mahali pembamba sana, hapakuwa na nafasi ya kugeukia mkono wa kuume, wala mkono wa kushoto. Hesabu 22:26

The angel of Yahweh went further, and stood in a narrow place, where was no way to turn either to the right hand or to the left.

Yule punda akamwona malaika wa Bwana, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake. Hesabu 22:27

The donkey saw the angel of Yahweh, and she lay down under Balaam: and Balaam's anger was kindled, and he struck the donkey with his staff.

Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi? Hesabu 22:28

Yahweh opened the mouth of the donkey, and she said to Balaam, What have I done to you, that you have struck me these three times?

Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi. Hesabu 22:29

Balaam said to the donkey, Because you have mocked me, I would there were a sword in my hand, for now I had killed you.

Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La! Hesabu 22:30

The donkey said to Balaam, Am I not your donkey, on which you have ridden all your life long to this day? was I ever wont to do so to you? and he said, No.

Ndipo Bwana akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa Bwana amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi. Hesabu 22:31

Then Yahweh opened the eyes of Balaam, and he saw the angel of Yahweh standing in the way, with his sword drawn in his hand; and he bowed his head, and fell on his face.

Malaika wa Bwana akamwambia, Mbona umempiga punda wako mara tatu hizi? Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu, Hesabu 22:32

The angel of Yahweh said to him, Why have you struck your donkey these three times? behold, I am come forth for an adversary, because your way is perverse before me:

punda akaniona, akageuka upande mbele zangu mara tatu hizi; kama asingejiepusha nami, bila shaka ningalikuua wewe, nikamwacha yeye hai. Hesabu 22:33

and the donkey saw me, and turned aside before me these three times: unless she had turned aside from me, surely now I had even slain you, and saved her alive.

Balaamu akamwambia malaika wa Bwana, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena. Hesabu 22:34

Balaam said to the angel of Yahweh, I have sinned; for I didn't know that you stood in the way against me: now therefore, if it displease you, I will get me back again.

Malaika wa Bwana akamwambia Balaamu Enenda pamoja na watu hawa, lakini neno lile nitakalokuambia, ndilo utakalosema. Basi Balaamu akaenda pamoja na wakuu wa Balaki. Hesabu 22:35

The angel of Yahweh said to Balaam, Go with the men; but only the word that I shall speak to you, that you shall speak. So Balaam went with the princes of Balak.

Balaki aliposikia ya kuwa Balaamu amefika, akatoka kwenda kumlaki, mpaka Mji wa Moabu, ulioko katika mpaka wa Arnoni, ulioko katika upande wa mwisho wa mpaka huo. Hesabu 22:36

When Balak heard that Balaam was come, he went out to meet him to the City of Moab, which is on the border of the Arnon, which is in the utmost part of the border.

Balaki akamwambia Balaamu, Je! Mimi sikutuma watu kwako kwa bidii ili kukuita? Mbona hukunijia? Je! Siwezi mimi kukufanyizia heshima nyingi? Hesabu 22:37

Balak said to Balaam, Didn't I earnestly send to you to call you? why didn't you come to me? am I not able indeed to promote you to honor?

Balaamu akamwambia Balaki, Tazama, nimekujia. Je! Mimi sasa nina uwezo wo wote kusema neno lo lote? Neno lile Mungu atakalolitia kinywani mwangu, ndilo nitakalolisema. Hesabu 22:38

Balaam said to Balak, Behold, I have come to you: have I now any power at all to speak anything? the word that God puts in my mouth, that shall I speak.

Balaamu akaenda pamoja na Balaki wakafika Kiriath-husothi. Hesabu 22:39

Balaam went with Balak, and they came to Kiriath Huzoth.

Balaki akachinja ng'ombe, na kondoo, akampelekea Balaamu na wale wakuu waliokuwa pamoja naye. Hesabu 22:40

Balak sacrificed oxen and sheep, and sent to Balaam, and to the princes who were with him.

Ikawa asubuhi Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hata mahali pa juu pa Baali; na kutoka huko akawaona watu, hata pande zao za mwisho. Hesabu 22:41

It happened in the morning, that Balak took Balaam, and brought him up into the high places of Baal; and he saw from there the utmost part of the people.