Hesabu 25 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 25 (Swahili) Numbers 25 (English)

Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; Hesabu 25:1

Israel abode in Shittim; and the people began to play the prostitute with the daughters of Moab:

kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. Hesabu 25:2

for they called the people to the sacrifices of their gods; and the people ate, and bowed down to their gods.

Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli. Hesabu 25:3

Israel joined himself to Baal Peor: and the anger of Yahweh was kindled against Israel.

Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli. Hesabu 25:4

Yahweh said to Moses, Take all the chiefs of the people, and hang them up to Yahweh before the sun, that the fierce anger of Yahweh may turn away from Israel.

Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. Hesabu 25:5

Moses said to the judges of Israel, Kill you everyone his men who have joined themselves to Baal Peor.

Na tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania. Hesabu 25:6

Behold, one of the children of Israel came and brought to his brothers a Midianite woman in the sight of Moses, and in the sight of all the congregation of the children of Israel, while they were weeping at the door of the tent of meeting.

Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake; Hesabu 25:7

When Phinehas, the son of Eleazar, the son of Aaron the priest, saw it, he rose up from the midst of the congregation, and took a spear in his hand;

akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. Hesabu 25:8

and he went after the man of Israel into the pavilion, and thrust both of them through, the man of Israel, and the woman through her body. So the plague was stayed from the children of Israel.

Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao. Hesabu 25:9

Those who died by the plague were twenty-four thousand.

Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, Hesabu 25:10

Yahweh spoke to Moses, saying,

Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu. Hesabu 25:11

Phinehas, the son of Eleazar, the son of Aaron the priest, has turned my wrath away from the children of Israel, in that he was jealous with my jealousy among them, so that I didn't consume the children of Israel in my jealousy.

Basi kwa hiyo, sema, Tazama, nampa yeye agano langu la amani; Hesabu 25:12

Therefore say, Behold, I give to him my covenant of peace:

tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli. Hesabu 25:13

and it shall be to him, and to his seed after him, the covenant of an everlasting priesthood; because he was jealous for his God, and made atonement for the children of Israel.

Basi jina la Mwisraeli huyo aliyeuawa pamoja na yule mwanamke Mmidiani, aliitwa Zimri, mwana wa Salu, mkuu wa nyumba ya baba zake, katika kabila la Simeoni. Hesabu 25:14

Now the name of the man of Israel that was slain, who was slain with the Midianite woman, was Zimri, the son of Salu, a prince of a fathers' house among the Simeonites.

Na jina la huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa, aliitwa Kozbi, binti Suri; naye alikuwa kichwa cha watu wa nyumba ya baba zake huko Midiani Hesabu 25:15

The name of the Midianite woman who was slain was Cozbi, the daughter of Zur; he was head of the people of a fathers' house in Midian.

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 25:16

Yahweh spoke to Moses, saying,

Wasumbue Wamidiani, na kuwapiga; Hesabu 25:17

Vex the Midianites, and strike them;

kwa sababu wao wawasumbua ninyi kwa hila zao, ambazo kwa hizo wamewadanganya ninyi katika jambo la Peori, na katika jambo la huyo Kozbi, binti wa mkuu wa Midiani, umbu lao, huyo aliyeuawa siku hiyo ya pigo katika jambo la Peori. Hesabu 25:18

for they vex you with their wiles, with which they have deceived you in the matter of Peor, and in the matter of Cozbi, the daughter of the prince of Midian, their sister, who was slain on the day of the plague in the matter of Peor.