Hesabu 36 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 36 (Swahili) Numbers 36 (English)

Kisha wale wakuu wa nyumba za mababa ya jamaa ya wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, katika jamaa za wana wa Yusufu, wakakaribia, na kunena mbele ya Musa, na mbele ya wakuu walio juu ya nyumba za mababa ya wana wa Israeli; Hesabu 36:1

The heads of the fathers' [houses] of the family of the children of Gilead, the son of Machir, the son of Manasseh, of the families of the sons of Joseph, came near, and spoke before Moses, and before the princes, the heads of the fathers' [houses] of the children of Israel:

wakasema, Bwana alimwagiza bwana wangu awape wana wa Israeli nchi kwa kupiga kura iwe urithi wao; tena bwana wangu aliagizwa na Bwana awape binti za Selofehadi ndugu yetu huo urithi wa baba yao. Hesabu 36:2

and they said, Yahweh commanded my lord to give the land for inheritance by lot to the children of Israel: and my lord was commanded by Yahweh to give the inheritance of Zelophehad our brother to his daughters.

Wakiolewa na watu wa wana wa hizo kabila nyingine za wana wa Israeli, ndipo urithi wao utatwaliwa na kuondolewa katika urithi wa baba zetu, na hiyo kabila watakayotiwa ndani yake itaongezewa urithi wao; basi urithi huo utaondolewa katika kura ya urithi wetu. Hesabu 36:3

If they be married to any of the sons of the [other] tribes of the children of Israel, then will their inheritance be taken away from the inheritance of our fathers, and will be added to the inheritance of the tribe whereunto they shall belong: so will it be taken away from the lot of our inheritance.

Tena itakapokuwapo hiyo yubile ya wana wa Israeli, ndipo urithi wa hiyo kabila ambayo wamekuwa ndani yake utaongezewa huo urithi wao; hivyo urithi wao utaondolewa katika urithi wa kabila ya baba zetu. Hesabu 36:4

When the jubilee of the children of Israel shall be, then will their inheritance be added to the inheritance of the tribe whereunto they shall belong: so will their inheritance be taken away from the inheritance of the tribe of our fathers.

Basi Musa akawaagiza wana wa Israeli kama neno la Bwana lilivyokuwa, akasema, Kabila ya wana wa Yusufu imenena yaliyo haki. Hesabu 36:5

Moses commanded the children of Israel according to the word of Yahweh, saying, The tribe of the sons of Joseph speaks right.

Bwana ameagiza neno hili katika habari ya binti za Selofehadi, akasema, Na waolewe na waume wawapendao; lakini na waolewe katika jamaa ya kabila ya baba zao. Hesabu 36:6

This is the thing which Yahweh does command concerning the daughters of Zelophehad, saying, Let them be married to whom they think best; only into the family of the tribe of their father shall they be married.

Hivyo hapana urithi wo wote wa wana wa Israeli utakaotoka kabila hii kwenda kabila hii; kwa kuwa wana wa Israeli watashikamana kila mtu na urithi wa kabila ya baba zake. Hesabu 36:7

So shall no inheritance of the children of Israel remove from tribe to tribe; for the children of Israel shall cleave everyone to the inheritance of the tribe of his fathers.

Na kila binti atakayemiliki urithi katika kabila yo yote katika wana wa Israeli, ataolewa katika jamaa moja ya kabila ya baba yake, ili wana wa Israeli wapate kumiliki kila mtu urithi wa baba zake. Hesabu 36:8

Every daughter, who possesses an inheritance in any tribe of the children of Israel, shall be wife to one of the family of the tribe of her father, that the children of Israel may possess every man the inheritance of his fathers.

Hivyo hapatakuwa na urithi uwao wote utakaotoka kabila hii kwenda kabila hii; kwa kuwa kabila za wana wa Israeli zitashikamana kila mmoja na urithi wake mwenyewe. Hesabu 36:9

So shall no inheritance remove from one tribe to another tribe; for the tribes of the children of Israel shall cleave everyone to his own inheritance.

Basi hao binti za Selofehadi wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa; Hesabu 36:10

Even as Yahweh commanded Moses, so did the daughters of Zelophehad:

kwa kuwa Mala, na Tirsa, na Hogla, na Milka, na Noa, binti za Selofehadi waliolewa na waume, wana wa ndugu za baba yao. Hesabu 36:11

for Mahlah, Tirzah, and Hoglah, and Milcah, and Noah, the daughters of Zelophehad, were married to their father's brothers' sons.

Waliolewa katika jamaa za wana wa Manase, mwana wa Yusufu, na urithi wao ukakaa katika kabila ya jamaa ya baba yao. Hesabu 36:12

They were married into the families of the sons of Manasseh the son of Joseph; and their inheritance remained in the tribe of the family of their father.

Haya ndiyo maagizo na hukumu, ambayo Bwana aliwaagiza wana wa Israeli, kwa mkono wa Musa, hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko Hesabu 36:13

These are the commandments and the ordinances which Yahweh commanded by Moses to the children of Israel in the plains of Moab by the Jordan at Jericho.