Hesabu 31 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 31 (Swahili) Numbers 31 (English)

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 31:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Walipize kisasi wana wa Israeli juu ya Wamidiani; kisha baadaye utakusanywa uwe pamoja na watu wako. Hesabu 31:2

Avenge the children of Israel of the Midianites: afterward you shall be gathered to your people.

Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipiza kisasi Bwana, juu ya Midiani. Hesabu 31:3

Moses spoke to the people, saying, Arm you men from among you for the war, that they may go against Midian, to execute Yahweh's vengeance on Midian.

Katika kila kabila mtatoa watu elfu, katika kabila zote za Israeli, nanyi mtawapeleka waende vitani. Hesabu 31:4

Of every tribe one thousand, throughout all the tribes of Israel, shall you send to the war.

Basi walitolewa katika maelfu ya Israeli, elfu moja ya kila kabila, watu waume kumi na mbili elfu walioandaliwa kwa vita. Hesabu 31:5

So there were delivered, out of the thousands of Israel, a thousand of every tribe, twelve thousand armed for war.

Basi Musa akawapeleka, watu elfu wa kila kabila waende vitani, wao na Finehasi mwana wa Eleazari kuhani, waende vitani, na vile vyombo vya mahali patakatifu, na hizo tarumbeta za kupiga sauti za kugutusha mkononi mwake. Hesabu 31:6

Moses sent them, one thousand of every tribe, to the war, them and Phinehas the son of Eleazar the priest, to the war, with the vessels of the sanctuary and the trumpets for the alarm in his hand.

Nao wakapigana na Midiani kama Bwana alivyomwagiza Musa; nao wakamwua kila mume. Hesabu 31:7

They warred against Midian, as Yahweh commanded Moses; and they killed every male.

Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga. Hesabu 31:8

They killed the kings of Midian with the rest of their slain: Evi, and Rekem, and Zur, and Hur, and Reba, the five kings of Midian: Balaam also the son of Beor they killed with the sword.

Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng'ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara. Hesabu 31:9

The children of Israel took captive the women of Midian and their little ones; and all their cattle, and all their flocks, and all their goods, they took for a prey.

Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na marago yao yote wakayateketeza kwa moto. Hesabu 31:10

All their cities in the places in which they lived, and all their encampments, they burnt with fire.

Nao wakatwaa hizo nyara zote, na mateka yote, ya wanadamu na ya wanyama. Hesabu 31:11

They took all the spoil, and all the prey, both of man and of animal.

Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo maragoni katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko. Hesabu 31:12

They brought the captives, and the prey, and the spoil, to Moses, and to Eleazar the priest, and to the congregation of the children of Israel, to the camp at the plains of Moab, which are by the Jordan at Jericho.

Basi Musa, na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya marago. Hesabu 31:13

Moses, and Eleazar the priest, and all the princes of the congregation, went forth to meet them outside of the camp.

Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao maakida wa elfu elfu, na wakuu wa mia mia, hao waliorudi kutoka katika kupiga vita. Hesabu 31:14

Moses was angry with the officers of the host, the captains of thousands and the captains of hundreds, who came from the service of the war.

Musa akawauliza, Je! Mmewaponya wanawake wote hai? Hesabu 31:15

Moses said to them, Have you saved all the women alive?

Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie Bwana dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa Bwana. Hesabu 31:16

Behold, these caused the children of Israel, through the counsel of Balaam, to commit trespass against Yahweh in the matter of Peor, and so the plague was among the congregation of Yahweh.

Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye. Hesabu 31:17

Now therefore kill every male among the little ones, and kill every woman who has known man by lying with him.

Lakini hao watoto wote wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye, mtawaweka hai kwa ajili yenu. Hesabu 31:18

But all the girls, who have not known man by lying with him, keep alive for yourselves.

Nanyi fanyeni matuo yenu nje ya marago muda wa siku saba; mtu awaye yote aliyemwua mtu, na awaye yote aliyemgusa mtu aliyeuawa, jitakaseni nafsi zenu siku ya tatu, na siku ya saba, ninyi na mateka yenu. Hesabu 31:19

Encamp you outside of the camp seven days: whoever has killed any person, and whoever has touched any slain, purify yourselves on the third day and on the seventh day, you and your captives.

Na katika habari ya kila nguo, na kila kitu kilichofanywa cha ngozi, na kazi yote ya singa za mbuzi, na vyombo vyote vilivyofanywa vya mti, mtajitakasa wenyewe; Hesabu 31:20

As to every garment, and all that is made of skin, and all work of goats' [hair], and all things made of wood, you shall purify yourselves.

Kisha Eleazari kuhani akawaambia waume wa vita wote waliokwenda vitani, Hii ndiyo amri ya sheria Bwana aliyomwagiza Musa; Hesabu 31:21

Eleazar the priest said to the men of war who went to the battle, This is the statute of the law which Yahweh has commanded Moses:

lakini dhahabu, na fedha, na shaba, na chuma, na bati, na risasi, Hesabu 31:22

however the gold, and the silver, the brass, the iron, the tin, and the lead,

kila kitu kiwezacho kuuhimili moto, mtakipitisha katika moto, nacho kitakuwa safi, pamoja na haya kitatakaswa kwa hayo maji ya farakano; na kila kitu kisichouhimili moto mtakipitisha katika hayo maji. Hesabu 31:23

everything that may abide the fire, you shall make to go through the fire, and it shall be clean; nevertheless it shall be purified with the water for impurity: and all that doesn't withstand the fire you shall make to go through the water.

Nanyi mtazifua nguo zenu siku ya saba, nanyi mtakuwa safi, kisha baadaye mtaingia maragoni. Hesabu 31:24

You shall wash your clothes on the seventh day, and you shall be clean; and afterward you shall come into the camp.

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 31:25

Yahweh spoke to Moses, saying,

Fanya jumla ya hayo mateka ya wanadamu, na ya wanyama pia, wewe, na Eleazari kuhani, na wakuu wa nyumba za baba za mkutano; Hesabu 31:26

Take the sum of the prey that was taken, both of man and of animal, you, and Eleazar the priest, and the heads of the fathers' [houses] of the congregation;

ukagawanye nyara mafungu mawili; kati ya watu waliozoea vita, waliotoka nje waende vitani, na huo mkutano wote; Hesabu 31:27

and divide the prey into two parts: between the men skilled in war, who went out to battle, and all the congregation.

kisha uwatoze hao watu wa vita waliotoka kwenda vitani sehemu kwa ajili ya Bwana; mmoja katika mia tano, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo; Hesabu 31:28

Levy a tribute to Yahweh of the men of war who went out to battle: one soul of five hundred, [both] of the persons, and of the oxen, and of the donkeys, and of the flocks:

twaa katika nusu yao, ukampe Eleazari kuhani, kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana. Hesabu 31:29

take it of their half, and give it to Eleazar the priest, for Yahweh's heave-offering.

Na katika hiyo nusu ya wana wa Israeli utatwaa mmoja atakayetolewa katika kila hamsini, katika wanadamu, na katika ng'ombe, na katika punda, na katika kondoo, maana, katika wanyama wote, ukawape Walawi, hao walindao ulinzi wa maskani ya Bwana. Hesabu 31:30

Of the children of Israel's half, you shall take one drawn out of every fifty, of the persons, of the oxen, of the donkeys, and of the flocks, [even] of all the cattle, and give them to the Levites, who keep the charge of the tent of Yahweh.

Musa na Eleazari kuhani wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa. Hesabu 31:31

Moses and Eleazar the priest did as Yahweh commanded Moses.

Basi masazo ya hizo nyara walizotwaa watu wa vita, zilikuwa ni kondoo mia sita na sabini na tano elfu, Hesabu 31:32

Now the prey, over and above the booty which the men of war took, was six hundred seventy-five thousand sheep,

na ng'ombe sabini na mbili elfu, Hesabu 31:33

and seventy-two thousand oxen,

na punda sitini na moja elfu, Hesabu 31:34

and seventy-one thousand donkeys,

tena wanadamu jumla yao ilikuwa thelathini na mbili elfu, katika hao wanawake ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye. Hesabu 31:35

and thirty-two thousand persons in all, of the women who had not known man by lying with him.

Na hiyo nusu ambayo ilikuwa ni sehemu ya hao waliotoka kwenda vitani, hesabu yake ilikuwa kondoo mia tatu na thelathini na saba elfu na mia tano; Hesabu 31:36

The half, which was the portion of those who went out to war, was in number three hundred thirty-seven thousand five hundred sheep:

na kodi ya Bwana katika hao kondoo ilikuwa kondoo mia sita na sabini na watano. Hesabu 31:37

and Yahweh's tribute of the sheep was six hundred seventy-five.

Tena, ng'ombe walikuwa thelathini na sita elfu; na katika hao kodi ya Bwana ilikuwa ng'ombe sabini na wawili. Hesabu 31:38

The oxen were thirty-six thousand; of which Yahweh's tribute was seventy-two.

Na punda walikuwa thelathini elfuna mia tano, katika hao kodi ya Bwana ilikuwa punda sitini na mmoja. Hesabu 31:39

The donkeys were thirty thousand five hundred; of which Yahweh's tribute was sixty-one.

Na wanadamu walikuwa watu kumi na sita elfu; katika hao sehemu ya Bwana ilikuwa ni watu thelathini na wawili. Hesabu 31:40

The persons were sixteen thousand; of whom Yahweh's tribute was thirty-two persons.

Basi Musa akampa Eleazari kuhani hiyo sehemu, iliyokuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Musa. Hesabu 31:41

Moses gave the tribute, which was Yahweh's heave-offering, to Eleazar the priest, as Yahweh commanded Moses.

Tena katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, ambayo Musa aliitenga na watu waliokwenda vitani, Hesabu 31:42

Of the children of Israel's half, which Moses divided off from the men who warred

(basi hiyo nusu ya mkutano ilikuwa ni kondoo mia tatu na thelathini na saba elfu na mia tano, Hesabu 31:43

(now the congregation's half was three hundred thirty-seven thousand five hundred sheep,

na ng'ombe thelathini na sita elfu, Hesabu 31:44

and thirty-six thousand oxen,

na punda thelathini elfu, na mia tano, Hesabu 31:45

and thirty thousand five hundred donkeys,

na wanadamu kumi na sita elfu;) Hesabu 31:46

and sixteen thousand persons),

na katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, Musa akatwaa mmoja aliyetolewa katika kila hamsini, wa binadamu na wa wanyama, akawapa Walawi, waliolinda ulinzi wa maskani ya Bwana; kama Bwana alivyomwagiza Musa. Hesabu 31:47

even of the children of Israel's half, Moses took one drawn out of every fifty, both of man and of animal, and gave them to the Levites, who kept the charge of the tent of Yahweh; as Yahweh commanded Moses.

Na majemadari waliokuwa juu ya elfu elfu za hiyo jeshi, na maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, wakamkaribia Musa; Hesabu 31:48

The officers who were over the thousands of the host, the captains of thousands, and the captains of hundreds, came near to Moses;

wakamwambia Musa wakisema, Sisi watumishi wako tumefanya jumla ya hesabu ya watu wa vita walio chini ya mikono yetu, na hapana hata mmoja aliyetupungukia. Hesabu 31:49

and they said to Moses, Your servants have taken the sum of the men of war who are under our charge, and there lacks not one man of us.

Nasi tumeleta matoleo ya Bwana, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za muhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya Bwana. Hesabu 31:50

We have brought Yahweh's offering, what every man has gotten, of jewels of gold, ankle-chains, and bracelets, signet-rings, ear-rings, and armlets, to make atonement for our souls before Yahweh.

Musa na Eleazari kuhani wakapokea kwao hiyo dhahabu, maana, vile vyombo vyote vilivyofanyizwa. Hesabu 31:51

Moses and Eleazar the priest took the gold of them, even all worked jewels.

Na dhahabu yote ya sadaka ya kuinuliwa waliyosongeza kwa Bwana, ya maakida wa elfu elfu, na maakida wa mia mia, ilikuwa shekeli kumi na sita elfu na mia saba na hamsini. Hesabu 31:52

All the gold of the heave-offering that they offered up to Yahweh, of the captains of thousands, and of the captains of hundreds, was sixteen thousand seven hundred fifty shekels.

(Kwa kuwa hao watu wa vita walikuwa wametwaa nyara, kila mtu nafsi yake.) Hesabu 31:53

([For] the men of war had taken booty, every man for himself.)

Basi Musa na Eleazari kuhani wakapokea hiyo dhahabu mikononi mwa hao maakida wa elfu elfu na wa mia mia, na kuileta ndani ya hema ya kukutania, ili iwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za Bwana.

Hesabu 31:54

Moses and Eleazar the priest took the gold of the captains of thousands and of hundreds, and brought it into the tent of meeting, for a memorial for the children of Israel before Yahweh.