Hesabu 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 16 (Swahili) Numbers 16 (English)

Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni; Hesabu 16:1

Now Korah, the son of Izhar, the son of Kohath, the son of Levi, with Dathan and Abiram, the sons of Eliab, and On, the son of Peleth, sons of Reuben, took [men]:

nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa; Hesabu 16:2

and they rose up before Moses, with certain of the children of Israel, two hundred fifty princes of the congregation, called to the assembly, men of renown;

nao wakakusanyika kinyume cha Musa na Haruni, na kuwaambia, Ninyi inawatosha, kwa kuwa mkutano wote ni mtakatifu, kila mmoja miongoni mwao, Bwana naye yu kati yao; n'nini basi kujitukuza juu ya mkutano wa Bwana? Hesabu 16:3

and they assembled themselves together against Moses and against Aaron, and said to them, You take too much on you, seeing all the congregation are holy, everyone of them, and Yahweh is among them: why then lift yourselves up above the assembly of Yahweh?

Musa aliposikia maneno haya, akapomoka kifudifudi; Hesabu 16:4

When Moses heard it, he fell on his face:

kisha akanena na Kora na mkutano wake wote, akawaambia, Asubuhi Bwana ataonyesha ni kina nani walio wake, kisha ni nani aliye mtakatifu, tena ni nani atakayemkaribisha kwake; maana, yeye atakayemchagua ndiye atakayemsongeza kwake. Hesabu 16:5

and he spoke to Korah and to all his company, saying, In the morning Yahweh will show who are his, and who is holy, and will cause him to come near to him: even him whom he shall choose will he cause to come near to him.

Fanyeni neno hili; twaeni vyetezo, ninyi Kora na mkutano wake wote; Hesabu 16:6

This do: take you censers, Korah, and all his company;

vitieni na moto, mkaweke na uvumba juu yake mbele za Bwana kesho; kisha itakuwa ya kwamba mtu Bwana atakayemchagua, yeye atakuwa mtakatifu; inawatosha ninyi, enyi wana wa Lawi. Hesabu 16:7

and put fire in them, and put incense on them before Yahweh tomorrow: and it shall be that the man whom Yahweh does choose, he [shall be] holy: you take too much on you, you sons of Levi.

Musa akamwambia Kora, Sikizeni basi, enyi Wana wa Lawi; Hesabu 16:8

Moses said to Korah, Hear now, you sons of Levi:

Je! Mwaona kuwa ni jambo dogo kwenu, kuwa Mungu wa Israeli amewatenga ninyi na mkutano wa Israeli, ili apate kuwakaribisha kwake; ili mfanye utumishi wa maskani ya Bwana, na kusimama mbele ya mkutano ili kuwatumikia; Hesabu 16:9

[seems it but] a small thing to you, that the God of Israel has separated you from the congregation of Israel, to bring you near to himself, to do the service of the tent of Yahweh, and to stand before the congregation to minister to them;

tena ya kuwa amekuleta uwe karibu, na ndugu zako wote wana wa Lawi pamoja nawe? Nanyi, je! Mwataka na ukuhani pia? Hesabu 16:10

and that he has brought you near, and all your brothers the sons of Levi with you? and seek you the priesthood also?

Kwa sababu hii wewe na mkutano wako wote mmekusanyika kinyume cha Bwana; na Haruni, je! Yeye ni nani hata mkamnung'unikia? Hesabu 16:11

Therefore you and all your company are gathered together against Yahweh: and Aaron, what is he who you murmur against him?

Kisha Musa akatuma kuwaita Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu; nao wakasema, Hatuji sisi; Hesabu 16:12

Moses sent to call Dathan and Abiram, the sons of Eliab; and they said, We won't come up:

je! Ni jambo dogo, wewe kutuleta kutoka nchi iliyojawa na maziwa na asali, ili kutuua jangwani, lakini pamoja na haya wajikuza mwenyewe uwe mkuu juu yetu kabisa? Hesabu 16:13

is it a small thing that you have brought us up out of a land flowing with milk and honey, to kill us in the wilderness, but you must needs make yourself also a prince over us?

Kisha, hukutuleta katika nchi iliyojawa na maziwa na asali, wala hukutupa urithi wa mashamba, na mashamba ya mizabibu; je! Unataka kuwatoboa macho watu hawa? Hatuji. Hesabu 16:14

Moreover you haven't brought us into a land flowing with milk and honey, nor given us inheritance of fields and vineyards: will you put out the eyes of these men? we won't come up.

Musa akakasirika sana, akamwambia Bwana. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao. Hesabu 16:15

Moses was very angry, and said to Yahweh, "Don't respect their offering: I have not taken one donkey from them, neither have I hurt one of them."

Kisha Musa akamwambia Kora, Wewe na mkutano wako wote iweni hapa mbele ya Bwana kesho, wewe, na wao, na Haruni; Hesabu 16:16

Moses said to Korah, You and all your company go before Yahweh, you, and they, and Aaron, tomorrow:

mkatwae kila mtu chetezo chake, na kutia uvumba juu yake, mkavilete mbele za Bwana, vyetezo mia mbili na hamsini; wewe pia, na Haruni, kila mtu na awe na chetezo chake. Hesabu 16:17

and take every man his censer, and put incense on them, and bring you before Yahweh every man his censer, two hundred fifty censers; you also, and Aaron, each his censer.

Basi wakavitwaa kila mtu chetezo chake, wakatia na moto ndani yake, wakatia na uvumba juu ya moto, na kusimama pale mlangoni pa hema ya kukutania, pamoja na Musa na Haruni. Hesabu 16:18

They took every man his censer, and put fire in them, and laid incense thereon, and stood at the door of the tent of meeting with Moses and Aaron.

Kisha Kora akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa Bwana ukatokea mbele ya mkutano wote. Hesabu 16:19

Korah assembled all the congregation against them to the door of the tent of meeting: and the glory of Yahweh appeared to all the congregation.

Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, Hesabu 16:20

Yahweh spoke to Moses and to Aaron, saying,

Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja. Hesabu 16:21

Separate yourselves from among this congregation, that I may consume them in a moment.

Nao wakapomoka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote? Hesabu 16:22

They fell on their faces, and said, God, the God of the spirits of all flesh, shall one man sin, and will you be angry with all the congregation?

Bwana akasema na Musa, na kumwambia, Hesabu 16:23

Yahweh spoke to Moses, saying,

Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu. Hesabu 16:24

Speak to the congregation, saying, Get away from around the tent of Korah, Dathan, and Abiram.

Basi Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu; na wazee wa Israeli wakaandamana naye. Hesabu 16:25

Moses rose up and went to Dathan and Abiram; and the elders of Israel followed him.

Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao cho chote, msiangamizwe katika dhambi zao zote. Hesabu 16:26

He spoke to the congregation, saying, Depart, I pray you, from the tents of these wicked men, and touch nothing of theirs, lest you be consumed in all their sins.

Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo. Hesabu 16:27

So they got them up from the tent of Korah, Dathan, and Abiram, on every side: and Dathan and Abiram came out, and stood at the door of their tents, and their wives, and their sons, and their little ones.

Musa akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Hesabu 16:28

Moses said, Hereby you shall know that Yahweh has sent me to do all these works; for [I have] not [done them] of my own mind.

Kama watu hawa wakifa kifo cha sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi. Hesabu 16:29

If these men die the common death of all men, or if they be visited after the visitation of all men; then Yahweh hasn't sent me.

Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana Hesabu 16:30

But if Yahweh make a new thing, and the ground open its mouth, and swallow them up, with all that appertain to them, and they go down alive into Sheol; then you shall understand that these men have despised Yahweh.

Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; Hesabu 16:31

It happened, as he made an end of speaking all these words, that the ground split apart that was under them;

nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. Hesabu 16:32

and the earth opened its mouth, and swallowed them up, and their households, and all the men who appertained to Korah, and all their goods.

Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni. Hesabu 16:33

So they, and all that appertained to them, went down alive into Sheol: and the earth closed on them, and they perished from among the assembly.

Nao Israeli wote waliokuwa kando-kando yao wakakimbia kwa ajili ya kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi. Hesabu 16:34

All Israel that were round about them fled at the cry of them; for they said, Lest the earth swallow us up.

Kisha moto ukatoka kwa Bwana, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba. Hesabu 16:35

Fire came forth from Yahweh, and devoured the two hundred fifty men who offered the incense.

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 16:36

Yahweh spoke to Moses, saying,

Mwambie Eleazari mwana wa Haruni kuhani, avitoe vile vyetezo hapo penye moto ukaumwage huo moto kule; kwani ni vitakatifu; Hesabu 16:37

Speak to Eleazar the son of Aaron the priest, that he take up the censers out of the burning, and scatter you the fire yonder; for they are holy,

vile vyetezo vya hao waliofanya dhambi na kuzihasiri nafsi zao wenyewe, na vifanywe mbao za kufuliwa kuwa kifuniko cha madhabahu; kwa kuwa walivisongeza mbele za Bwana, navyo ni vitakatifu; vitakuwa ishara kwa wana wa Israeli. Hesabu 16:38

even the censers of these sinners against their own lives; and let them be made beaten plates for a covering of the altar: for they offered them before Yahweh; therefore they are holy; and they shall be a sign to the children of Israel.

Basi Eleazari kuhani akavitwaa vile vyetezo vya shaba, vilivyosongezwa na hao walioteketezwa; nao wakavifua viwe kifuniko cha madhabahu; Hesabu 16:39

Eleazar the priest took the brazen censers, which those who were burnt had offered; and they beat them out for a covering of the altar,

viwe ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili mgeni awaye yote asiye wa kizazi cha Haruni, asikaribie kufukiza uvumba mbele za Bwana; asiwe mfano wa Kora, na mkutano wake; kama Bwana alivyonena naye, kwa mkono wa Musa. Hesabu 16:40

to be a memorial to the children of Israel, to the end that no stranger, who isn't of the seed of Aaron, comes near to burn incense before Yahweh; that he not be as Korah, and as his company: as Yahweh spoke to him by Moses.

Lakini siku ya pili yake mkutano wote wa wana wa Israeli wakamnung'unikia Musa, na Haruni, wakasema, Ninyi mmewaua watu wa Bwana. Hesabu 16:41

But on the next day all the congregation of the children of Israel murmured against Moses and against Aaron, saying, You have killed the people of Yahweh.

Basi ilikuwa, hapo huo mkutano ulipokuwa umekutanika kinyume cha Musa, na kinyume cha Haruni, wakaangalia upande wa hema ya kukutania; na tazama, hilo wingu likaifunika hema, na utukufu wa Bwana ukaonekana. Hesabu 16:42

It happened, when the congregation was assembled against Moses and against Aaron, that they looked toward the tent of meeting: and, behold, the cloud covered it, and the glory of Yahweh appeared.

Na Musa na Haruni wakaenda hapo mbele ya hema ya kukutania. Hesabu 16:43

Moses and Aaron came to the front of the tent of meeting.

Naye Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 16:44

Yahweh spoke to Moses, saying,

Ondokeni kati ya mkutano, ili niwaangamize mara moja. Wao wakapomoka kifudifudi. Hesabu 16:45

Get away from among this congregation, that I may consume them in a moment. They fell on their faces.

Musa akamwambia Haruni, Haya, shika chetezo chako, ukatie moto ndani yake, moto wa madhabahuni, kisha utie na uvumba juu ya moto, ukakichukue haraka, wende nacho katika huo mkutano, ukawafanyie upatanisho; kwa kuwa ghadhabu zimetoka kwa Bwana; hiyo tauni imeanza. Hesabu 16:46

Moses said to Aaron, Take your censer, and put fire therein from off the altar, and lay incense thereon, and carry it quickly to the congregation, and make atonement for them: for there is wrath gone out from Yahweh; the plague is begun.

Basi Haruni akakishika chetezo kama Musa alivyonena, akapiga mbio akaenda katikati ya mkutano; na tazama, tauni ilikuwa imeanza kati ya watu; akatia uvumba juu ya moto na kufanya upatanisho kwa ajili ya hao watu. Hesabu 16:47

Aaron took as Moses spoke, and ran into the midst of the assembly; and, behold, the plague was begun among the people: and he put on the incense, and made atonement for the people.

Akasimama kati ya hao waliokufa na hao waliokuwa wakali hai; tauni ikazuiwa. Hesabu 16:48

He stood between the dead and the living; and the plague was stayed.

Basi waliokufa kwa tauni walikuwa kumi na nne elfu na mia saba, zaidi ya hao waliokufa katika jambo la Kora. Hesabu 16:49

Now those who died by the plague were fourteen thousand and seven hundred, besides those who died about the matter of Korah.

Haruni akamrudia Musa pale mlangoni pa hema ya kukutania; hiyo tauni ikazuiwa. Hesabu 16:50

Aaron returned to Moses to the door of the tent of meeting: and the plague was stayed.