Hesabu 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 21 (Swahili) Numbers 21 (English)

Na Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyeketi upande wa Negebu, alisikia habari ya kuwa Israeli alikuja kwa njia ya Atharimu; basi akapigana na Israeli, na watu kadha wa kadha miongoni mwao akawateka mateka. Hesabu 21:1

The Canaanite, the king of Arad, who lived in the South, heard tell that Israel came by the way of Atharim; and he fought against Israel, and took some of them captive.

Basi Israeli akaweka nadhiri kwa Bwana akasema, Kama wewe utawatia watu hawa mikononi mwangu kweli ndipo mimi nitaiharibu miji yao kabisa. Hesabu 21:2

Israel vowed a vow to Yahweh, and said, If you will indeed deliver this people into my hand, then I will utterly destroy their cities.

Bwana akasikiza sauti ya Israeli, akawatia Wakanaani mikononi mwao; nao wakawaharibu wao na miji yao kabisa; na jina la mahali hapo likaitwa Horma. Hesabu 21:3

Yahweh listened to the voice of Israel, and delivered up the Canaanites; and they utterly destroyed them and their cities: and the name of the place was called Hormah.

Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia. Hesabu 21:4

They traveled from Mount Hor by the way to the Red Sea, to compass the land of Edom: and the soul of the people was much discouraged because of the way.

Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. Hesabu 21:5

The people spoke against God, and against Moses, Why have you brought us up out of Egypt to die in the wilderness? for there is no bread, and there is no water; and our soul loathes this light bread.

Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. Hesabu 21:6

Yahweh sent fiery serpents among the people, and they bit the people; and much people of Israel died.

Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu. Hesabu 21:7

The people came to Moses, and said, We have sinned, because we have spoken against Yahweh, and against you; pray to Yahweh, that he take away the serpents from us. Moses prayed for the people.

Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Hesabu 21:8

Yahweh said to Moses, Make you a fiery serpent, and set it on a standard: and it shall happen, that everyone who is bitten, when he sees it, shall live.

Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi. Hesabu 21:9

Moses made a serpent of brass, and set it on the standard: and it happened, that if a serpent had bitten any man, when he looked to the serpent of brass, he lived.

Kisha wana wa Israeli wakasafiri, wakapanga marago Obothi. Hesabu 21:10

The children of Israel traveled, and encamped in Oboth.

Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika jangwa iliyoelekea Moabu, upande wa maawio ya jua. Hesabu 21:11

They traveled from Oboth, and encamped at Iyeabarim, in the wilderness which is before Moab, toward the sunrise.

Kutoka huko wakasafiri, wakapanga katika bonde la Zeredi. Hesabu 21:12

From there they traveled, and encamped in the valley of Zered.

Kutoka huko wakasafiri, wakapanga upande wa pili wa Arnoni, ulio jangwani, utokao katika mpaka wa Waamori; maana, Arnoni ndio mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori. Hesabu 21:13

From there they traveled, and encamped on the other side of the Arnon, which is in the wilderness, that comes out of the border of the Amorites: for the Arnon is the border of Moab, between Moab and the Amorites.

Kwa hiyo imesemwa katika chuo cha Vita vya Bwana, Wahebu katika Sufa, Na bonde za Arnoni, Hesabu 21:14

Therefore it is said in the book of the Wars of Yahweh, Vaheb in Suphah, The valleys of the Arnon,

Na matelemko ya hizo bonde Kwenye kutelemkia maskani ya Ari, Na kutegemea mpaka wa Moabu. Hesabu 21:15

The slope of the valleys That inclines toward the dwelling of Ar, Leans on the border of Moab.

Kutoka huko wakasafiri kwenda Beeri; ni kisima ambacho Bwana alimwambia Musa, Uwakutanishe watu, nami nitawapa maji. Hesabu 21:16

From there they traveled to Beer: that is the well of which Yahweh said to Moses, Gather the people together, and I will give them water.

Ndipo Israeli wakaimba wimbo huu; Bubujika Ee kisima; kiimbieni; Hesabu 21:17

Then sang Israel this song: Spring up, well; sing you to it:

Kisima walichokichimba wakuu, Ambacho wakuu wa watu wakakifukua, Kwa fimbo za enzi, kwa fimbo zao. Hesabu 21:18

The well, which the princes dug, Which the nobles of the people dug, With the scepter, [and] with their poles. From the wilderness [they traveled] to Mattanah;

na kutoka Matana wakaenda Nahalieli; na kutoka Nahalieli wakaenda Bamothi; Hesabu 21:19

and from Mattanah to Nahaliel; and from Nahaliel to Bamoth;

na kutoka Bamothi wakaenda bondeni kwenye konde la Moabu, hata kilele cha Pisga, kielekeacho chini jangwani. Hesabu 21:20

and from Bamoth to the valley that is in the field of Moab, to the top of Pisgah, which looks down on the desert.

Kisha Israeli akatuma wajumbe kumwendea Sihoni mfalme wa Waamori, na kusema, Hesabu 21:21

Israel sent messengers to Sihon king of the Amorites, saying,

Nipe ruhusa nipite katika nchi yako; hatutageuka kando kwenda mashambani, wala kuingia katika mashamba ya mizabibu hatutakunywa maji ya visimani; tutakwenda kwa njia kuu ya mfalme, hata tutakapokuwa tumepita mpaka wako. Hesabu 21:22

Let me pass through your land: we will not turn aside into field, or into vineyard; we will not drink of the water of the wells: we will go by the king's highway, until we have passed your border.

Lakini Sihoni hakukubali kumwacha Israeli kupita katika mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, akatoka aende kupigana na Israeli jangwani, akafika mpaka Yahasa; akapigana na Israeli. Hesabu 21:23

Sihon would not allow Israel to pass through his border: but Sihon gathered all his people together, and went out against Israel into the wilderness, and came to Jahaz; and he fought against Israel.

Israeli wakampiga kwa makali ya upanga, na kuimiliki nchi yake, tangu mto wa Arnoni hata mto wa Yaboki, mpaka nchi ya wana wa Amoni; kwa kuwa mpaka wa wana wa Amoni ulikuwa una nguvu. Hesabu 21:24

Israel struck him with the edge of the sword, and possessed his land from the Arnon to the Jabbok, even to the children of Ammon; for the border of the children of Ammon was strong.

Basi Israeli wakaitwaa miji hiyo yote; Israeli wakakaa katika miji yote ya Waamori, katika Heshboni, na miji yake yote. Hesabu 21:25

Israel took all these cities: and Israel lived in all the cities of the Amorites, in Heshbon, and in all the towns of it.

Kwa kuwa Heshboni ulikuwa ni mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akipigana na mfalme wa Moabu wa mbele, na kumpokonya nchi yake yote mkononi mwake, mpaka mto wa Arnoni. Hesabu 21:26

For Heshbon was the city of Sihon the king of the Amorites, who had fought against the former king of Moab, and taken all his land out of his hand, even to the Arnon.

Kwa hiyo, hao wanenao kwa mithali wasema, Njoni Heshboni, Mji wa Sihoni na ujengwe na kuthibitishwa; Hesabu 21:27

Therefore those who speak in proverbs say, Come you to Heshbon; Let the city of Sihon be built and established:

Maana, moto umetoka Heshboni, Umekuwa Ari ya Moabu, Mwali wa moto umetoka mji wa Sihoni; Wakuu wa mahali palipoinuka Arnoni Hesabu 21:28

For a fire is gone out of Heshbon, A flame from the city of Sihon: It has devoured Ar of Moab, The lords of the high places of the Arnon.

Ole wako Moabu! Umeangamia, enyi watu wa Kemoshi; Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi, Na binti zake waende utumwani, Wamwendee Sihoni mfalme wa Waamori. Hesabu 21:29

Woe to you, Moab! You are undone, people of Chemosh: He has given his sons as fugitives, His daughters into captivity, To Sihon king of the Amorites.

Tumewapigia mishale; Heshboni umepotea mpaka Diboni, Nasi tumeharibu mpaka Nofa, Ifikiliayo Medeba. Hesabu 21:30

We have shot at them; Heshbon is perished even to Dibon, We have laid waste even to Nophah, Which [reaches] to Medeba.

Basi hivyo Israeli akaketi katika nchi ya Waamori. Hesabu 21:31

Thus Israel lived in the land of the Amorites.

Kisha Musa akapeleka watu ili kupeleleza Yazeri, nao wakaitwaa miji yake, wakawafukuza Waamori waliokuwamo. Hesabu 21:32

Moses sent to spy out Jazer; and they took the towns of it, and drove out the Amorites who were there.

Kisha wakageuka na kukwea kwa njia ya Bashani; na Ogu mfalme wa Bashani akaondoka apigane nao huko Edrei, yeye na watu wake wote. Hesabu 21:33

They turned and went up by the way of Bashan: and Og the king of Bashan went out against them, he and all his people, to battle at Edrei.

Bwana akamwambia Musa, Usimche; kwa kuwa nimekwisha mtia mkononi mwako, na watu wake wote, na nchi yake; nawe utamtenda kama ulivyomtenda Sihoni mfalme wa Waamori, aliyeketi Heshboni. Hesabu 21:34

Yahweh said to Moses, Don't fear him: for I have delivered him into your hand, and all his people, and his land; and you shall do to him as you did to Sihon king of the Amorites, who lived at Heshbon.

Basi wakampiga, na wanawe, na watu wake wote, hata wasisaze kwake mtu ye yote; nao wakaimiliki nchi yake. Hesabu 21:35

So they struck him, and his sons and all his people, until there was none left him remaining: and they possessed his land.