Hesabu 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 3 (Swahili) Numbers 3 (English)

Basi vizazi vya Haruni na Musa, siku hiyo Bwana aliyosema na Musa katika mlima wa Sinai, ni hivi. Hesabu 3:1

Now this is the history of the generations of Aaron and Moses in the day that Yahweh spoke with Moses in Mount Sinai.

Tena majina ya hao wana wa Haruni ni haya; Nadabu mzaliwa wa kwanza, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. Hesabu 3:2

These are the names of the sons of Aaron: Nadab the firstborn, and Abihu, Eleazar, and Ithamar.

Hayo ndiyo majina ya wana wa Haruni, hao makuhani waliotiwa mafuta, ambao aliwaweka wakfu ili wafanye kazi ya ukuhani. Hesabu 3:3

These are the names of the sons of Aaron, the priests who were anointed, whom he consecrated to minister in the priest's office.

Kisha Nadabu na Abihu walikufa mbele za Bwana, waliposongeza moto wa kigeni mbele za Bwana, katika bara ya Sinai, nao walikuwa hawana wana; na Eleazari na Ithamari wakafanya kazi ya ukuhani mbele ya uso wa Haruni baba yao. Hesabu 3:4

Nadab and Abihu died before Yahweh, when they offered strange fire before Yahweh, in the wilderness of Sinai, and they had no children. Eleazar and Ithamar ministered in the priest's office in the presence of Aaron their father.

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 3:5

Yahweh spoke to Moses, saying,

Ilete karibu kabila ya Lawi, ukawaweke mbele ya Haruni kuhani, ili wapate kumtumikia. Hesabu 3:6

"Bring the tribe of Levi near, and set them before Aaron the priest, that they may minister to him.

Nao wataulinda ulinzi wake, na ulinzi wa mkutano wote mbele ya hema ya kukutania, ili watumike utumishi wa maskani. Hesabu 3:7

They shall keep his charge, and the charge of the whole congregation before the Tent of Meeting, to do the service of the tabernacle.

Nao watavitunza vyombo vyote vya hema ya kukutania, na kulinda ulinzi wa wana wa Israeli, ili watumike utumishi wa maskani. Hesabu 3:8

They shall keep all the furnishings of the Tent of Meeting, and the obligations of the children of Israel, to do the service of the tabernacle.

Nawe utawapa Haruni na wanawe hao Walawi wawe nao; amepewa watu hao kabisa kwa ajili ya wana wa Israeli. Hesabu 3:9

You shall give the Levites to Aaron and to his sons. They are wholly given to him on the behalf of the children of Israel.

Nawe utawaweka Haruni na wanawe, nao wataushika ukuhani wao, na mgeni atakayekaribia atauawa. Hesabu 3:10

You shall appoint Aaron and his sons, and they shall keep their priesthood. The stranger who comes near shall be put to death."

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 3:11

Yahweh spoke to Moses, saying,

Mimi, tazama, nimewatwaa Walawi na kuwatoa kati ya wana wa Israeli badala ya wazaliwa wa kwanza wote wafunguao tumbo katika wana wa Israeli; na hao Walawi watakuwa wangu; Hesabu 3:12

"Behold, I have taken the Levites from among the children of Israel instead of all the firstborn who open the womb among the children of Israel; and the Levites shall be mine:

kwa kuwa hao wazaliwa wa kwanza wote ni wangu; katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri nikajiwekea wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, wa wanadamu na wa wanyama; watakuwa wangu; mimi ndimi Bwana. Hesabu 3:13

for all the firstborn are mine. On the day that I struck down all the firstborn in the land of Egypt I made holy to me all the firstborn in Israel, both man and animal. They shall be mine. I am Yahweh."

Kisha Bwana akanena na Musa huko katika bara ya Sinai, na kumwambia, Hesabu 3:14

Yahweh spoke to Moses in the wilderness of Sinai, saying,

Uwahesabu wana wa Lawi kwa kuandama nyumba za baba zao na jamaa zao; kila mtu mume tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi utawahesabu. Hesabu 3:15

"Number the children of Levi by their fathers' houses, by their families: every male from a month old and upward shall you number."

Basi Musa akawahesabu kama neno la Bwana kama alivyoagizwa. Hesabu 3:16

Moses numbered them according to the word of Yahweh, as he was commanded.

Na wana wa Lawi walikuwa ni hawa kwa majina yao; Gershoni, na Kohathi, na Merari. Hesabu 3:17

These were the sons of Levi by their names: Gershon, and Kohath, and Merari.

Na majina ya wana wa Gershoni kwa jamaa zao ni Libni na Shimei. Hesabu 3:18

These are the names of the sons of Gershon by their families: Libni and Shimei.

Na wana wa Kohathi kwa jamaa zao ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli. Hesabu 3:19

The sons of Kohath by their families: Amram, and Izhar, Hebron, and Uzziel.

Na wana wa Merari kwa jamaa zao ni Mahli, na Mushi. Hizi ndizo jamaa za Walawi kwa nyumba za baba zao. Hesabu 3:20

The sons of Merari by their families: Mahli and Mushi. These are the families of the Levites according to their fathers' houses.

Katika Gershoni walikuwa jamaa ya Walibni, na jamaa ya Washimei, hawa ndio jamaa za Wagershoni. Hesabu 3:21

Of Gershon was the family of the Libnites, and the family of the Shimeites: these are the families of the Gershonites.

Hao waliohesabiwa kwao, kama hesabu ya waume wote, tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, hao waliohesabiwa kwao walikuwa saba elfu na mia tano. Hesabu 3:22

Those who were numbered of them, according to the number of all the males, from a month old and upward, even those who were numbered of them were seven thousand five hundred.

Jamaa za Wagershoni watapanga rago nyuma ya maskani, upande wa magharibi. Hesabu 3:23

The families of the Gershonites shall encamp behind the tabernacle westward.

Na mkuu wa nyumba ya baba zao Wagershoni atakuwa Eliasafu mwana wa Laeli. Hesabu 3:24

The prince of the fathers' house of the Gershonites shall be Eliasaph the son of Lael.

Na ulinzi wa Wagershoni katika hema ya kukutania ni hiyo maskani, na Hema, na kifuniko chake, na pazia la mlango wa hema ya kukutania, Hesabu 3:25

The charge of the sons of Gershon in the Tent of Meeting shall be the tabernacle, and the tent, its covering, and the screen for the door of the Tent of Meeting,

na kuta za nguo za ua, na sitara ya mlango wa ua, iliyo karibu na maskani, na karibu na madhabahu pande zote, na kamba zake zitumiwazo kwa matumizi yake yote. Hesabu 3:26

and the hangings of the court, and the screen for the door of the court, which is by the tabernacle, and around the altar, and its cords for all of its service.

Na katika Kohathi ni jamaa ya Waamrami, na jamaa ya Waishari, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya hao Wauzieli; hizo ni jamaa za Wakohathi. Hesabu 3:27

Of Kohath was the family of the Amramites, and the family of the Izharites, and the family of the Hebronites, and the family of the Uzzielites: these are the families of the Kohathites.

Kama hesabu ya waume wote, tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa elfu nane na mia sita, wenye kuulinda ulinzi wa mahali patakatifu. Hesabu 3:28

According to the number of all the males, from a month old and upward, there were eight thousand six hundred, keeping the charge of the sanctuary.

Jamaa za wana wa Kohathi watapanga rago upande wa kusini wa maskani. Hesabu 3:29

The families of the sons of Kohath shall encamp on the south side of the tabernacle.

Na mkuu wa nyumba ya baba za jamaa za Wakohathi atakuwa Elisafani mwana wa Uzieli. Hesabu 3:30

The prince of the fathers' house of the families of the Kohathites shall be Elizaphan the son of Uzziel.

Na vitu watakavyovitunza ni hilo sanduku, na meza, na kinara cha taa, na madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu wavitumiavyo katika kutumika kwao, na pazia, na utumishi wake wote. Hesabu 3:31

Their charge shall be the ark, the table, the lamp stand, the altars, the vessels of the sanctuary with which they minister, and the screen, and all its service.

Na Eleazari mwana wa Haruni kuhani atakuwa mkuu wa hao wakuu wa Walawi, naye atawasimamia hao walindao ulinzi wa mahali patakatifu. Hesabu 3:32

Eleazar the son of Aaron the priest shall be prince of the princes of the Levites, with the oversight of those who keep the charge of the sanctuary.

Katika Merari ni jamaa ya hao Wamahli, na jamaa ya Wamushi; hizo ni jamaa za Merari. Hesabu 3:33

Of Merari was the family of the Mahlites, and the family of the Mushites. These are the families of Merari.

Na hao waliohesabiwa kwao, kama hesabu ya waume wote, tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa sita elfu na mia mbili. Hesabu 3:34

Those who were numbered of them, according to the number of all the males, from a month old and upward, were six thousand two hundred.

Na mkuu wa nyumba ya baba za jamaa za Merari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hao watapanga rago upande wa maskani, wa kaskazini. Hesabu 3:35

The prince of the fathers' house of the families of Merari was Zuriel the son of Abihail. They shall encamp on the north side of the tabernacle.

Na usimamizi walioamriwa wana wa Merari ulikuwa ni kutunza mbao za maskani, na mataruma yake, na nguzo zake, na matako yake, na vyombo vyake vyote, na utumishi wake wote; Hesabu 3:36

The appointed charge of the sons of Merari shall be the tabernacle's boards, its bars, its pillars, its sockets, all its instruments, all its service,

na nguzo za ua zilizouzunguka, na matako yake, na vigingi vyake, na kamba zake. Hesabu 3:37

the pillars of the court around it, their sockets, their pins, and their cords.

Na hao watakaopanga mbele ya maskani upande wa mashariki, mbele ya hema ya kukutania upande wa kuelekea maawio ya jua, watakuwa hawa, Musa na Haruni na wanawe, wenye kulinda ulinzi wa mahali patakatifu, yaani, huo ulinzi wa wana wa Israeli; na mgeni atakayekaribia atauawa. Hesabu 3:38

Those who encamp before the tabernacle eastward, in front of the Tent of Meeting toward the sunrise, shall be Moses, and Aaron and his sons, keeping the charge of the sanctuary for the charge of the children of Israel. The stranger who comes near shall be put to death.

Hao wote waliohesabiwa katika Walawi, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya Bwana, kwa jamaa zao, waume wote tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, walikuwa ishirini na mbili elfu. Hesabu 3:39

All who were numbered of the Levites, whom Moses and Aaron numbered at the commandment of Yahweh, by their families, all the males from a month old and upward, were twenty-two thousand.

Kisha Bwana akamwambia Musa, Uwahesabu waume wote wazaliwa wa kwanza katika wana wa Israeli tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi uyahesabu majina yao. Hesabu 3:40

Yahweh said to Moses, "Number all the firstborn males of the children of Israel from a month old and upward, and take the number of their names.

Nawe utawatwaa Walawi kwa ajili yangu mimi (Mimi ndimi Bwana) badala ya hao wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli; na wanyama wa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa wanyama wa wana wa Israeli. Hesabu 3:41

You shall take the Levites for me (I am Yahweh) instead of all the firstborn among the children of Israel; and the cattle of the Levites instead of all the firstborn among the cattle of the children of Israel."

Musa akahesabu, kama Bwana alivyomwagiza, wazaliwa wa kwanza wote katika wana wa Israeli. Hesabu 3:42

Moses numbered, as Yahweh commanded him, all the firstborn among the children of Israel.

Wazaliwa wa kwanza wote walio waume kwa hesabu ya majina, tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi, katika hao waliohesabiwa kwao, walikuwa ishirini na mbili elfu na mia mbili na sabini na watatu. Hesabu 3:43

All the firstborn males according to the number of names, from a month old and upward, of those who were numbered of them, were twenty-two thousand two hundred seventy-three.

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 3:44

Yahweh spoke to Moses, saying,

Uwatwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza katika wana wa Israeli, na wanyama wa Walawi badala ya wanyama wao; na hao Walawi watakuwa wangu mimi; mimi ndimi Bwana. Hesabu 3:45

"Take the Levites instead of all the firstborn among the children of Israel, and the cattle of the Levites instead of their cattle; and the Levites shall be mine. I am Yahweh.

Tena kwa kuwakomboa hao watu mia mbili na sabini na watatu, wa hao wazaliwa wa kwanza wa Israeli, ambao wamezidi ile hesabu ya Walawi, Hesabu 3:46

For the redemption of the two hundred seventy-three of the firstborn of the children of Israel, who exceed the number of the Levites,

utatwaa shekeli tano kwa kichwa cha kila mtu kwa hiyo shekeli ya mahali patakatifu (shekeli ni gera ishirini); Hesabu 3:47

you shall take five shekels apiece for each one; after the shekel of the sanctuary you shall take them (the shekel is twenty gerahs):

na hizo fedha ambazo waliosalia wamekombolewa kwazo utampa Haruni na wanawe. Hesabu 3:48

and you shall give the money, with which the remainder of them is redeemed, to Aaron and to his sons."

Basi Musa akawatoza fedha za ukombozi, hao waliozidi hesabu ya wale waliokombolewa na Walawi; Hesabu 3:49

Moses took the redemption money from those who exceeded the number of those who were redeemed by the Levites;

akatwaa hizo fedha kwa wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli; shekeli elfu moja na mia tatu na sitini na tano kwa shekeli ya mahali patakatifu; Hesabu 3:50

from the firstborn of the children of Israel he took the money, one thousand three hundred sixty-five shekels, after the shekel of the sanctuary:

kisha hizo fedha za ukombozi Musa akampa Haruni na wanawe, kama neno la Bwana, kama Bwana alivyomwagiza Musa.

Hesabu 3:51

and Moses gave the redemption money to Aaron and to his sons, according to the word of Yahweh, as Yahweh commanded Moses.