Hesabu 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 10 (Swahili) Numbers 10 (English)

Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, Hesabu 10:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Jifanyie tarumbeta mbili za fedha; utazifanya za kazi ya ufuzi; nawe utazitumia kwa kuwaita mkutano wakutane, na kwa kusafiri kwao yale makambi. Hesabu 10:2

Make you two trumpets of silver; of beaten work shall you make them: and you shall use them for the calling of the congregation, and for the journeying of the camps.

Na hapo watakapozipiga hizo tarumbeta, mkutano wote utakukutanikia wewe, hapo mlangoni pa hema ya kukutania. Hesabu 10:3

When they shall blow them, all the congregation shall gather themselves to you at the door of the tent of meeting.

Nao wakipiga tarumbeta moja tu ndipo wakuu, walio vichwa vya maelfu ya Israeli, watakukutanikia wewe Hesabu 10:4

If they blow but one, then the princes, the heads of the thousands of Israel, shall gather themselves to you.

Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha sana, marago yaliyoko upande wa mashariki yatasafiri. Tena hapo mtakapopiga sauti ya kugutusha ya pili, marago yaliyoko upande wa kusini watasafiri; Hesabu 10:5

When you blow an alarm, the camps that lie on the east side shall take their journey.

watapiga sauti ya kugutusha kwa ajili ya safari zao. Hesabu 10:6

When you blow an alarm the second time, the camps that lie on the south side shall take their journey: they shall blow an alarm for their journeys.

Lakini mkutano utakapokutanishwa pamoja mtapiga, lakini hamtapiga sauti ya kugutusha. Hesabu 10:7

But when the assembly is to be gathered together, you shall blow, but you shall not sound an alarm.

Wana wa Haruni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta; nazo zitakuwa kwenu ni amri ya milele katika vizazi vyenu vyote. Hesabu 10:8

The sons of Aaron, the priests, shall blow the trumpets; and they shall be to you for a statute forever throughout your generations.

Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za Bwana, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu. Hesabu 10:9

When you go to war in your land against the adversary who oppresses you, then you shall sound an alarm with the trumpets; and you shall be remembered before Yahweh your God, and you shall be saved from your enemies.

Tena katika siku ya furaha yenu, na katika sikukuu zenu zilizoamriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. Hesabu 10:10

Also in the day of your gladness, and in your set feasts, and in the beginnings of your months, you shall blow the trumpets over your burnt offerings, and over the sacrifices of your peace-offerings; and they shall be to you for a memorial before your God: I am Yahweh your God.

Ikawa mwaka wa pili, mwezi wa pili, siku ya ishirini ya mwezi, hilo wingu liliinuka kutoka pale juu ya maskani ya ushahidi. Hesabu 10:11

It happened in the second year, in the second month, on the twentieth day of the month, that the cloud was taken up from over the tent of the testimony.

Wana wa Israeli wakasafiri kwenda mbele, kwa safari zao kutoka jangwa la Sinai; na hilo wingu likakaa katika jangwa la Parani. Hesabu 10:12

The children of Israel set forward according to their journeys out of the wilderness of Sinai; and the cloud abode in the wilderness of Paran.

Nao wakasafiri kwanza kwa amri ya Bwana kwa mkono wa Musa. Hesabu 10:13

They first took their journey according to the commandment of Yahweh by Moses.

Mahali pa mbele ilisafiri beramu ya marago ya wana wa Yuda, kwa majeshi yao; na Nashoni mwana wa Aminadabu ndiye aliyekuwa juu ya jeshi lake. Hesabu 10:14

In the first [place] the standard of the camp of the children of Judah set forward according to their hosts: and over his host was Nahshon the son of Amminadab.

Na juu ya jeshi la kabila ya wana wa Isakari alikuwa Nethaneli mwana wa Suari. Hesabu 10:15

Over the host of the tribe of the children of Issachar was Nethanel the son of Zuar.

Na juu ya jeshi la kabila ya wana wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni. Hesabu 10:16

Over the host of the tribe of the children of Zebulun was Eliab the son of Helon.

Na maskani ilishushwa; na wana wa Gershoni, na wana wa Merari, walioichukua maskani, wakasafiri kwenda mbele. Hesabu 10:17

The tent was taken down; and the sons of Gershon and the sons of Merari, who bore the tent, set forward.

Kisha beramu ya marago ya Reubeni ikasafiri kwenda mbele kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake alikuwa Elisuri mwana wa Shedeuri. Hesabu 10:18

The standard of the camp of Reuben set forward according to their hosts: and over his host was Elizur the son of Shedeur.

Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Suri-shadai. Hesabu 10:19

Over the host of the tribe of the children of Simeon was Shelumiel the son of Zurishaddai.

Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli. Hesabu 10:20

Over the host of the tribe of the children of Gad was Eliasaph the son of Deuel.

Ndipo wakasafiri Wakohathi wenye kuvichukua vile vitu vitakatifu; na hao wengine wakaisimamisha maskani kabla hawajaja wao. Hesabu 10:21

The Kohathites set forward, bearing the sanctuary: and [the others] did set up the tent against their coming.

Kisha beramu ya marago ya wana wa Efraimu ikasafiri kwenda mbele kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake ni Elishama mwana wa Amihudi. Hesabu 10:22

The standard of the camp of the children of Ephraim set forward according to their hosts: and over his host was Elishama the son of Ammihud.

Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri. Hesabu 10:23

Over the host of the tribe of the children of Manasseh was Gamaliel the son of Pedahzur.

Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni. Hesabu 10:24

Over the host of the tribe of the children of Benjamin was Abidan the son of Gideoni.

Kisha beramu ya marago ya wana wa Dani, ambayo yalikuwa ni nyuma ya marago yote, ikasafiri, kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake ni Ahiezeri mwana wa Amishadai. Hesabu 10:25

The standard of the camp of the children of Dan, which was the rearward of all the camps, set forward according to their hosts: and over his host was Ahiezer the son of Ammishaddai.

Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani; Hesabu 10:26

Over the host of the tribe of the children of Asher was Pagiel the son of Ochran.

Tena juu ya jeshi la kabila ya wana wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani. Hesabu 10:27

Over the host of the tribe of the children of Naphtali was Ahira the son of Enan.

Ndivyo zilivyokuwa safari zao wana wa Israeli kwa majeshi: yao; nao wakasafiri kwenda mbele. Hesabu 10:28

Thus were the travels of the children of Israel according to their hosts; and they set forward.

Kisha Musa akamwambia Hobabu, mwana wa Reueli Mmidiani, mkwewe Musa, Sisi twasafiri kwenenda mahali ambapo Bwana amenena habari zake hivi, Nitawapa ninyi mahali hapo; uje pamoja nasi, nasi tutakufanyia mema; kwa kuwa Bwana ametamka mema juu ya Israeli. Hesabu 10:29

Moses said to Hobab, the son of Reuel the Midianite, Moses' father-in-law, We are journeying to the place of which Yahweh said, I will give it you: come you with us, and we will do you good; for Yahweh has spoken good concerning Israel.

Naye akamwambia, Siendi mimi; ila nitairudia nchi yangu mwenyewe, na kwa jamaa zangu mwenyewe. Hesabu 10:30

He said to him, I will not go; but I will depart to my own land, and to my relatives.

Naye akamwambia, Usituache, tafadhali; kwa kuwa wewe wajua jinsi tutakavyopanga nyikani, nawe utakuwa kwetu badala ya macho. Hesabu 10:31

He said, Don't leave us, please; because you know how we are to encamp in the wilderness, and you shall be to us instead of eyes.

Itakuwa, ukienda pamoja nasi, naam, itakuwa mema yo yote Bwana atakayotutendea sisi, tutakutendea wewe vivyo. Hesabu 10:32

It shall be, if you go with us, yes, it shall be, that whatever good Yahweh shall do to us, the same will we do to you.

Basi wakasafiri kutoka penye mlima wa Bwana safari ya siku tatu; na sanduku la agano la Bwana likatangulia mbele yao mwendo wa siku tatu, ili kuwatafutia mahali pa kupumzika. Hesabu 10:33

They set forward from the Mount of Yahweh three days' journey; and the ark of the covenant of Yahweh went before them three days' journey, to seek out a resting-place for them.

Na wingu la Bwana lilikuwa juu yao mchana hapo waliposafiri kwenda mbele kutoka kambini. Hesabu 10:34

The cloud of Yahweh was over them by day, when they set forward from the camp.

Ilikuwa, hapo sanduku liliposafiri kwenda mbele, ndipo Musa akasema, Inuka, Ee Bwana, adui zako na watawanyike; na wakimbie mbele zako hao wakuchukiao. Hesabu 10:35

It happened, when the ark set forward, that Moses said, Rise up, Yahweh, and let your enemies be scattered; and let those who hate you flee before you.

Tena hapo liliposimama, akasema, Ee Bwana, uwarudie maelfu kumi ya maelfu ya Israeli.

Hesabu 10:36

When it rested, he said, Return, Yahweh, to the ten thousands of the thousands of Israel.