Hesabu 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 7 (Swahili) Numbers 7 (English)

Ilikuwa siku hiyo Musa alipokwisha kuisimamisha maskani, na kuitia mafuta, na kuitakasa, na vyombo vyake vyote, na hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na kuvitia mafuta, na kuvitakasa; Hesabu 7:1

It happened on the day that Moses had finished setting up the tabernacle, and had anointed it and sanctified it, with all its furniture, and the altar with all its vessels, and had anointed and sanctified them;

ndipo wakuu wa Israeli, vichwa vya nyumba za baba zao, wakatoa matoleo; hao ndio wakuu wa kabila, hao ndio waliokuwa juu yao waliohesabiwa; Hesabu 7:2

that the princes of Israel, the heads of their fathers' houses, offered. These were the princes of the tribes. These are they who were over those who were numbered:

nao wakamletea Bwana matoleo yao, magari sita yenye mafuniko juu, na ng'ombe kumi na wawili; gari moja kwa wakuu wawili wawili, na ng'ombe mmoja kwa kila mkuu; nao wakayasongeza hapo mbele ya maskani. Hesabu 7:3

and they brought their offering before Yahweh, six covered wagons, and twelve oxen; a wagon for every two of the princes, and for each one an ox: and they presented them before the tabernacle.

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 7:4

Yahweh spoke to Moses, saying,

Pokea mikononi mwao, ili kwamba viwe vya kutumiwa katika utumishi wa hema ya kukutania; nawe utawapa Walawi vitu hivyo, kila mtu utampa kama utumishi wake ulivyo. Hesabu 7:5

"Accept these from them, that they may be used in doing the service of the Tent of Meeting; and you shall give them to the Levites, to every man according to his service."

Basi Musa akapokea hayo magari, na ng'ombe, akawapa Walawi. Hesabu 7:6

Moses took the wagons and the oxen, and gave them to the Levites.

Wana wa Gershoni akawapa magari mawili na ng'ombe wanne, kama utumishi wao ulivyokuwa; Hesabu 7:7

He gave two wagons and four oxen to the sons of Gershon, according to their service:

na wana wa Merari akawapa magari manne na ng'ombe wanane kama utumishi wao ulivyokuwa, chini ya mkono wa Ithamari, mwana wa Haruni kuhani. Hesabu 7:8

and he gave four wagons and eight oxen to the sons of Merari, according to their service, under the direction of Ithamar the son of Aaron the priest.

Lakini hakuwapa wana wa Kohathi; maana, utumishi wa vile vitu vitakatifu ulikuwa ni wao; nao wakavichukua mabegani mwao. Hesabu 7:9

But to the sons of Kohath he gave none, because the service of the sanctuary belonged to them; they carried it on their shoulders.

Kisha wale wakuu wakatoa matoleo kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, katika siku hiyo iliyotiwa mafuta, wakuu wakayatoa matoleo yao mbele ya madhabahu. Hesabu 7:10

The princes gave offerings for the dedication of the altar in the day that it was anointed, even the princes gave their offerings before the altar.

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Watasongeza matoleo yao, kila mkuu kwa siku yake, kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu. Hesabu 7:11

Yahweh said to Moses, "They shall offer their offering, each prince on his day, for the dedication of the altar."

Basi aliyetoa matoleo yake siku ya kwanza ni Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila ya Yuda; Hesabu 7:12

He who offered his offering the first day was Nahshon the son of Amminadab, of the tribe of Judah,

na matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha uzani wake ni shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:13

and his offering was: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kimejaa uvumba; Hesabu 7:14

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mmoja mume, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:15

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:16

one male goat for a sin offering;

na kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe waume wawili, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Nashoni mwana wa Aminadabu. Hesabu 7:17

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Nahshon the son of Amminadab.

Siku ya pili Nethaneli mwana wa Suari, mkuu wa Isakari, alitoa; Hesabu 7:18

On the second day Nethanel the son of Zuar, prince of Issachar, gave his offering.

yeye akasongeza matoleo yake, sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa ni sadaka ya unga; Hesabu 7:19

He offered for his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilikuwa kimejaa uvumba; Hesabu 7:20

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:21

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:22

one male goat for a sin offering;

na kwa dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Nethaneli mwana wa Suari. Hesabu 7:23

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, five male lambs a year old. This was the offering of Nethanel the son of Zuar.

Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, mkuu wa wana wa Zabuloni; Hesabu 7:24

On the third day Eliab the son of Helon, prince of the children of Zebulun

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:25

gave his offering: one silver platter, the weight of which was a hundred and thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:26

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:27

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:28

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Eliabu mwana wa Heloni. Hesabu 7:29

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Eliab the son of Helon.

Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, mkuu wa wana wa Reubeni; Hesabu 7:30

On the fourth day Elizur the son of Shedeur, prince of the children of Reuben

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:31

gave his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:32

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:33

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:34

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Elisuri mwana wa Shedeuri. Hesabu 7:35

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Elizur the son of Shedeur.

Siku ya tano Shelumieli mwana wa Suri-shadai, mkuu wa wana Simeoni; Hesabu 7:36

On the fifth day Shelumiel the son of Zurishaddai, prince of the children of Simeon

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:37

gave his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:38

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:39

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:40

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Shelumieli mwana wa Suri-shadai Hesabu 7:41

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old: this was the offering of Shelumiel the son of Zurishaddai.

Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, mkuu wa wana wa Gadi Hesabu 7:42

On the sixth day, Eliasaph the son of Deuel, prince of the children of Gad

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:43

gave his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:44

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:45

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:46

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Eliasafu mwana wa Deueli. Hesabu 7:47

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Eliasaph the son of Deuel.

Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, mkuu wa wana wa Efraimu; Hesabu 7:48

On the seventh day Elishama the son of Ammihud, prince of the children of Ephraim

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:49

gave his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:50

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:51

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:52

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Elishama mwana wa Amihudi. Hesabu 7:53

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Elishama the son of Ammihud.

Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, mkuu wa wana wa Manase; Hesabu 7:54

On the eighth day Gamaliel the son of Pedahzur, prince of the children of Manasseh

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:55

gave his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:56

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:57

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:58

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Gamalieli mwana wa Pedasuri. Hesabu 7:59

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Gamaliel the son of Pedahzur.

Siku ya kenda Abidani mwana wa Gideoni, mkuu wa wana wa Benyamini; Hesabu 7:60

On the ninth day Abidan the son of Gideoni, prince of the children of Benjamin

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:61

gave his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:62

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:63

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:64

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Abidani mwana wa Gideoni. Hesabu 7:65

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Abidan the son of Gideoni.

Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, mkuu wa wana wa Dani; Hesabu 7:66

On the tenth day Ahiezer the son of Ammishaddai, prince of the children of Dan

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:67

gave his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:68

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:69

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:70

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Ahiezeri mwana wa Amishadai. Hesabu 7:71

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Ahiezer the son of Ammishaddai.

Na siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, mkuu wa wana wa Asheri; Hesabu 7:72

On the eleventh day Pagiel the son of Ochran, prince of the children of Asher

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:73

gave his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:74

one golden ladle of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:75

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:76

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Pagieli mwana wa Okrani. Hesabu 7:77

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Pagiel the son of Ochran.

Na siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, mkuu wa wana wa Naftali; Hesabu 7:78

On the twelfth day Ahira the son of Enan, prince of the children of Naphtali

matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; Hesabu 7:79

gave his offering: one silver platter, the weight of which was one hundred thirty shekels, one silver bowl of seventy shekels, after the shekel of the sanctuary; both of them full of fine flour mixed with oil for a meal offering;

na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; Hesabu 7:80

one golden spoon of ten shekels, full of incense;

na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; Hesabu 7:81

one young bull, one ram, one male lamb a year old, for a burnt offering;

na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; Hesabu 7:82

one male goat for a sin offering;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Ahira mwana wa Enani. Hesabu 7:83

and for the sacrifice of peace offerings, two oxen, five rams, five male goats, and five male lambs a year old. This was the offering of Ahira the son of Enan.

Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa na wakuu wa Israeli kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, siku hiyo ilipotiwa mafuta; sahani za fedha kumi na mbili, na bakuli za fedha kumi na mbili, na vijiko vya dhahabu kumi na viwili; Hesabu 7:84

This was the dedication of the altar, on the day when it was anointed, by the princes of Israel: twelve silver platters, twelve silver bowls, twelve golden ladles;

kila sahani ya fedha uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na kila bakuli uzani wake ni shekeli sabini; fedha yote ya vile vyombo ilikuwa shekeli elfu mbili na mia nne, kwa shekeli ya mahali patakatifu; Hesabu 7:85

each silver platter weighing one hundred thirty shekels, and each bowl seventy; all the silver of the vessels two thousand four hundred shekels, after the shekel of the sanctuary;

na vijiko vya dhahabu vilivyojaa uvumba kumi na viwili, uzani wake kila kijiko shekeli kumi, kwa shekeli ya mahali patakatifu; dhahabu yote ya vile vijiko ilikuwa shekeli mia na ishirini; Hesabu 7:86

the twelve golden ladles, full of incense, weighing ten shekels apiece, after the shekel of the sanctuary; all the gold of the ladles weighed one hundred twenty shekels;

ng'ombe wote waliokuwa wa sadaka ya kuteketezwa walikuwa ng'ombe waume kumi na wawili, na hao kondoo waume walikuwa kumi na wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza walikuwa kumi na wawili, pamoja na sadaka yao ya unga; na mbuzi waume wa sadaka ya dhambi ni kumi na wawili; Hesabu 7:87

all the oxen for the burnt offering twelve bulls, the rams twelve, the male lambs a year old twelve, and their meal offering; and the male goats for a sin offering twelve;

na ng'ombe wote waliokuwa wa dhabihu ya sadaka za amani ni ng'ombe waume ishirini na wanne, na hao kondoo waume walikuwa ni sitini, na hao mbuzi waume walikuwa ni sitini, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza walikuwa sitini. Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, baada ya hiyo madhabahu kutiwa mafuta. Hesabu 7:88

and all the oxen for the sacrifice of peace offerings twenty-four bulls, the rams sixty, the male goats sixty, the male lambs a year old sixty. This was the dedication of the altar, after it was anointed.

Kisha, Musa alipoingia ndani ya hema ya kukutania ili kunena na Mungu ndipo alipoisikia Sauti ikinena naye kutoka hapo juu ya kiti cha rehema, kilichokuwa juu ya sanduku la ushahidi, ikitoka kati ya yale makerubi mawili; naye akanena naye. Hesabu 7:89

When Moses went into the Tent of Meeting to speak with Yahweh, he heard his voice speaking to him from above the mercy seat that was on the ark of the Testimony, from between the two cherubim: and he spoke to him.