Hesabu 28 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 28 (Swahili) Numbers 28 (English)

Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Hesabu 28:1

Yahweh spoke to Moses, saying,

Waagize hao wana wa Israeli, uwaambie, Matoleo yangu, chakula changu cha sadaka zangu zisongezwazo kwa moto, za harufu ya kupendeza kwangu mimi, mtaangalia kuzisongeza kwangu wakati wake upasao. Hesabu 28:2

Command the children of Israel, and tell them, My offering, my food for my offerings made by fire, of a sweet savor to me, shall you observe to offer to me in their due season.

Nawe utawaambia, Hii ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto mtakayomsongezea Bwana; wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu, wawili kila siku, wawe sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote. Hesabu 28:3

You shall tell them, This is the offering made by fire which you shall offer to Yahweh: he-lambs a year old without blemish, two day by day, for a continual burnt offering.

Mwana-kondoo mmoja utamsongeza asubuhi, na mwana-kondoo wa pili utamsongeza jioni; Hesabu 28:4

The one lamb shall you offer in the morning, and the other lamb shall you offer at even;

pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta ya kupondwa. Hesabu 28:5

and the tenth part of an ephah of fine flour for a meal-offering, mixed with the fourth part of a hin of beaten oil.

Ni sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, iliyoamriwa huko katika mlima wa Sinai iwe harufu ya kupendeza, sadaka ya kusongezwa kwa Bwana kwa moto. Hesabu 28:6

It is a continual burnt offering, which was ordained in Mount Sinai for a sweet savor, an offering made by fire to Yahweh.

Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa robo ya hini kwa mwana-kondoo mmoja; hiyo sadaka ya kinywaji, ya kileo, utammiminia Bwana katika mahali hapo patakatifu. Hesabu 28:7

The drink-offering of it shall be the fourth part of a hin for the one lamb: in the holy place shall you pour out a drink-offering of strong drink to Yahweh.

Na mwana-kondoo wa pili utamsongeza wakati wa jioni; kama ile sadaka ya unga iliyosongezwa asubuhi, na kama sadaka yake ya kinywaji, ndivyo utakavyoisongeza, ni sadaka ya kusongezwa kwa moto, ni harufu ya kupendeza kwa Bwana. Hesabu 28:8

The other lamb shall you offer at even: as the meal-offering of the morning, and as the drink-offering of it, you shall offer it, an offering made by fire, of a sweet savor to Yahweh.

Tena katika siku ya Sabato watasongezwa wana-kondoo wawili, waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, pamoja na sehemu ya kumi mbili za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka yake ya kinywaji; Hesabu 28:9

On the Sabbath day two he-lambs a year old without blemish, and two tenth parts [of an ephah] of fine flour for a meal-offering, mixed with oil, and the drink-offering of it:

hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila Sabato, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. Hesabu 28:10

this is the burnt offering of every Sabbath, besides the continual burnt-offering, and the drink-offering of it.

Tena katika mianzo ya miezi yenu mtamsongezea Bwana sadaka ya kuteketezwa; nayo ni ng'ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza, wakamilifu, saba; Hesabu 28:11

In the beginnings of your months you shall offer a burnt offering to Yahweh: two young bulls, and one ram, seven he-lambs a year old without blemish;

pamoja na sehemu ya kumi tatu za efa za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa kila ng'ombe; na sehemu ya kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, kwa huyo kondoo mume mmoja; Hesabu 28:12

and three tenth parts [of an ephah] of fine flour for a meal-offering, mixed with oil, for each bull; and two tenth parts of fine flour for a meal-offering, mixed with oil, for the one ram;

na sehemu ya kumi moja ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwana-kondoo; kuwa sadaka ya kuteketezwa ya harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto. Hesabu 28:13

and a tenth part of fine flour mixed with oil for a meal-offering to every lamb; for a burnt offering of a sweet savor, an offering made by fire to Yahweh.

Tena sadaka zake za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng'ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo mume, na robo ya hini kwa mwana-kondoo; hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka. Hesabu 28:14

Their drink-offerings shall be half a hin of wine for a bull, and the third part of a hin for the ram, and the fourth part of a hin for a lamb: this is the burnt offering of every month throughout the months of the year.

Tena mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa Bwana itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. Hesabu 28:15

One male goat for a sin-offering to Yahweh; it shall be offered besides the continual burnt offering, and the drink-offering of it.

Tena, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, ni pasaka ya Bwana. Hesabu 28:16

In the first month, on the fourteenth day of the month, is Yahweh's Passover.

Siku ya kumi na tano ya mwezi huo patakuwa na sikukuu; mkate usiotiwa chachu utaliwa muda wa siku saba. Hesabu 28:17

On the fifteenth day of this month shall be a feast: seven days shall unleavened bread be eaten.

Siku ya kwanza patakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; Hesabu 28:18

In the first day shall be a holy convocation: you shall do no servile work;

lakini mtaisongeza sadaka kwa njia ya moto, sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana; ng'ombe waume wadogo wawili, na kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; watakuwa wakamilifu kwenu; Hesabu 28:19

but you shall offer an offering made by fire, a burnt offering to Yahweh: two young bulls, and one ram, and seven he-lambs a year old; they shall be to you without blemish;

pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta; mtasongeza sehemu ya kumi tatu kwa ng'ombe mmoja, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume; Hesabu 28:20

and their meal-offering, fine flour mixed with oil: three tenth parts shall you offer for a bull, and two tenth parts for the ram;

na sehemu ya kumi moja utasongeza kwa kila mwana-kondoo, wale wana-kondoo saba; Hesabu 28:21

a tenth part shall you offer for every lamb of the seven lambs;

tena mtasongeza mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Hesabu 28:22

and one male goat for a sin-offering, to make atonement for you.

Mtasongeza wanyama hao zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, iliyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote. Hesabu 28:23

You shall offer these besides the burnt offering of the morning, which is for a continual burnt offering.

Mtasongeza sadaka kwa mfano huu kila siku muda wa siku saba, chakula cha sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana; itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji. Hesabu 28:24

After this manner you shall offer daily, for seven days, the food of the offering made by fire, of a sweet savor to Yahweh: it shall be offered besides the continual burnt offering, and the drink-offering of it.

Na siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi. Hesabu 28:25

On the seventh day you shall have a holy convocation: you shall do no servile work.

Tena katika siku ya malimbuko, hapo mtakapomsongezea Bwana sadaka ya unga mpya katika sikukuu yenu ya majuma mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yo yote ya utumishi; Hesabu 28:26

Also in the day of the first fruits, when you offer a new meal-offering to Yahweh in your [feast of] weeks, you shall have a holy convocation; you shall do no servile work;

lakini mtasongeza sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana; ng'ombe waume wadogo wawili, kondoo mume mmoja, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza saba; Hesabu 28:27

but you shall offer a burnt offering for a sweet savor to Yahweh: two young bulls, one ram, seven he-lambs a year old;

pamoja na sadaka zake za unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu ya kumi tatu kwa kila ng'ombe, na sehemu ya kumi mbili kwa kondoo mume, Hesabu 28:28

and their meal-offering, fine flour mixed with oil, three tenth parts for each bull, two tenth parts for the one ram,

na sehemu ya kumi moja kwa kila mwana-kondoo, wa wale wana-kondoo saba; Hesabu 28:29

a tenth part for every lamb of the seven lambs;

na mbuzi mume mmoja, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu. Hesabu 28:30

one male goat, to make atonement for you.

Zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, mtasongeza wanyama hao (watakuwa wakamilifu kwenu), pamoja na sadaka zake za vinywaji.

Hesabu 28:31

Besides the continual burnt offering, and the meal-offering of it, you shall offer them (they shall be to you without blemish), and their drink-offerings.