Hesabu 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
Hesabu 11 (Swahili) Numbers 11 (English)

Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa Bwana; Bwana aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa Bwana ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago. Hesabu 11:1

The people were as murmurers, [speaking] evil in the ears of Yahweh: and when Yahweh heard it, his anger was kindled; and the fire of Yahweh burnt among them, and devoured in the uttermost part of the camp.

Ndipo watu wakamlilia Musa; naye Musa akamwomba Bwana, na ule moto ukakoma. Hesabu 11:2

The people cried to Moses; and Moses prayed to Yahweh, and the fire abated.

Jina la mahali hapo likaitwa Tabera; kwa sababu huo moto wa Bwana ukawaka kati yao. Hesabu 11:3

The name of that place was called Taberah, because the fire of Yahweh burnt among them.

Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N'nani atakayetupa nyama tule? Hesabu 11:4

The mixed multitude that was among them lusted exceedingly: and the children of Israel also wept again, and said, Who shall give us flesh to eat?

Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu; Hesabu 11:5

We remember the fish, which we ate in Egypt for nothing; the cucumbers, and the melons, and the leeks, and the onions, and the garlic:

lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu. Hesabu 11:6

but now our soul is dried away; there is nothing at all save this manna to look on.

Na hiyo mana ilikuwa mfano wa chembe za mtama na kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake bedola. Hesabu 11:7

The manna was like coriander seed, and the appearance of it as the appearance of bdellium.

Watu wakazunguka-zunguka na kuikusanya, kisha wakaisaga kwa mawe ya kusagia, au kuitwanga katika vinu, kisha wakaitokosa nyunguni, na kuandaa mikate; na tamu yake ilikuwa kama tamu ya mafuta mapya. Hesabu 11:8

The people went about, and gathered it, and ground it in mills, or beat it in mortars, and boiled it in pots, and made cakes of it: and the taste of it was as the taste of fresh oil.

Umande ulipoyaangukia marago wakati wa usiku, hiyo mana ilianguka pamoja nao. Hesabu 11:9

When the dew fell on the camp in the night, the manna fell on it.

Basi Musa akawasikia watu wakilia katika jamaa zao zote, kila mtu mlangoni pa hema yake; na hasira za Bwana zikawaka sana; Musa naye akakasirika. Hesabu 11:10

Moses heard the people weeping throughout their families, every man at the door of his tent: and the anger of Yahweh was kindled greatly; and Moses was displeased.

Musa akamwambia Bwana, Mbona umenitenda uovu mimi mtumishi wako? Kwa nini sikupata neema machoni pako, hata ukanitwika mzigo wa watu hawa wote juu yangu? Hesabu 11:11

Moses said to Yahweh, Why have you dealt ill with your servant? and why haven't I found favor in your sight, that you lay the burden of all this people on me?

Je! Ni mimi niliyewatungisha mimba watu hawa wote je! Ni mimi niliyewazaa, hata ikawa wewe kuniambia, Haya, wachukue kifuani mwako, mfano wa baba mwenye kulea achukuavyo mtoto anyonyaye, uende nao mpaka nchi uliyowaapia baba zao? Hesabu 11:12

Have I conceived all this people? have I brought them forth, that you should tell me, Carry them in your bosom, as a nursing-father carries the sucking child, to the land which you swore to their fathers?

Nipate wapi nyama ya kuwapa watu hawa wote? Kwani wanililia, wakisema Tupe nyama, tupate kula. Hesabu 11:13

Whence should I have flesh to give to all this people? for they weep to me, saying, Give us flesh, that we may eat.

Mimi siwezi kuwachukua watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni mzigo mzito sana wa kunishinda. Hesabu 11:14

I am not able to bear all this people alone, because it is too heavy for me.

Na kama ukinitenda hivi, nakuomba uniulie mbali, kwamba nimepata fadhili mbele ya macho yako; nami nisiyaone haya mashaka yangu. Hesabu 11:15

If you deal thus with me, please kill me out of hand, if I have found favor in your sight; and let me not see my wretchedness.

Kisha Bwana akamwambia Musa, Nikusanyie watu sabini, miongoni mwa wazee wa israeli, ambao wewe wawajua kuwa ndio wazee wa watu hawa, na maakida juu yao; ukawalete hata hema ya kukutania, wasimame huko pamoja nawe. Hesabu 11:16

Yahweh said to Moses, Gather to me seventy men of the elders of Israel, whom you know to be the elders of the people, and officers over them; and bring them to the tent of meeting, that they may stand there with you.

Nami nitashuka niseme nawe huko, nami nitatwaa sehemu ya roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao; nao watachukua mzigo wa watu hawa pamoja nawe, ili usiuchukue wewe peke yako. Hesabu 11:17

I will come down and talk with you there: and I will take of the Spirit which is on you, and will put it on them; and they shall bear the burden of the people with you, that you not bear it yourself alone.

Kisha uwaambie watu hawa, Jitakaseni nafsi zenu kabla ya kesho, nanyi mtakula nyama; kwa maana mmelia masikioni mwa Bwana, mkisema, Ni nani atakayetupa nyama, tule? Maana huko Misri tulikuwa na uheri. Basi kwa sababu hiyo Bwana atawapa nyama, nanyi mtakula. Hesabu 11:18

Say you to the people, Sanctify yourselves against tomorrow, and you shall eat flesh; for you have wept in the ears of Yahweh, saying, Who shall give us flesh to eat? for it was well with us in Egypt: therefore Yahweh will give you flesh, and you shall eat.

Hamtakula siku moja, wala siku mbili, wala siku tano, wala siku kumi, wala siku ishirini; Hesabu 11:19

You shall not eat one day, nor two days, nor five days, neither ten days, nor twenty days,

lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hata hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa Bwana aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani? Hesabu 11:20

but a whole month, until it come out at your nostrils, and it be loathsome to you; because that you have rejected Yahweh who is among you, and have wept before him, saying, Why came we forth out of Egypt?

Musa akasema, Watu hawa ambao mimi ni kati yao, ni watu sita mia elfu waendao kwa miguu; nawe umesema, Nitawapa nyama, ili wale muda wa mwezi mzima. Hesabu 11:21

Moses said, The people, among whom I am, are six hundred thousand footmen; and you have said, I will give them flesh, that they may eat a whole month.

Je! Makundi ya kondoo na ng'ombe yatachinjwa kwa ajili yao, ili kuwatosha? Au samaki wote wa baharini watakusanywa pamoja kwa ajili yao, ili kuwatosha? Hesabu 11:22

Shall flocks and herds be slain for them, to suffice them? or shall all the fish of the sea be gathered together for them, to suffice them?

Bwana akamwambia Musa, Je! Mkono wa Bwana umepungua urefu wake? Sasa utaona kwamba neno langu litatimizwa kwako, au sivyo. Hesabu 11:23

Yahweh said to Moses, Has Yahweh's hand grown short? now shall you see whether my word shall happen to you or not.

Musa akatoka, akawaambia watu maneno ya Bwana; akawakutanisha watu sabini miongoni mwa wazee wa watu, akawaweka kuizunguka Hema. Hesabu 11:24

Moses went out, and told the people the words of Yahweh: and he gathered seventy men of the elders of the people, and set them round about the Tent.

Ndipo Bwana akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena. Hesabu 11:25

Yahweh came down in the cloud, and spoke to him, and took of the Spirit that was on him, and put it on the seventy elders: and it happened that when the Spirit rested on them, they prophesied, but they did so no more.

Lakini watu wawili walisalia kambini, jina la mmoja aliitwa Eldadi, na jina la wa pili aliitwa Medadi; na roho ile ikawashukia; nao walikuwa miongoni mwao walioandikwa, lakini walikuwa hawakutoka kwenda hemani; nao wakatabiri kambini. Hesabu 11:26

But there remained two men in the camp, the name of the one was Eldad, and the name of the other Medad: and the Spirit rested on them; and they were of those who were written, but had not gone out to the Tent; and they prophesied in the camp.

Mtu mmoja kijana akapiga mbio, akaenda akamwambia Musa, akasema, Eldadi na Medadi wanatoa unabii kambini. Hesabu 11:27

There ran a young man, and told Moses, and said, Eldad and Medad do prophesy in the camp.

Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa tangu ujana wake, akajibu akasema, Ee bwana wangu Musa, uwakataze. Hesabu 11:28

Joshua the son of Nun, the minister of Moses, one of his chosen men, answered, My lord Moses, forbid them.

Musa akamwambia, Je! Umekuwa na wivu kwa ajili yangu; ingekuwa heri kama watu wote wa Bwana wangekuwa manabii na kama Bwana angewatia roho yake. Hesabu 11:29

Moses said to him, Are you jealous for my sake? would that all Yahweh's people were prophets, that Yahweh would put his Spirit on them!

Kisha Musa akaenda akaingia kambini, yeye na wale wazee wa Israeli. Hesabu 11:30

Moses got him into the camp, he and the elders of Israel.

Kisha upepo ukavuma kutoka kwa Bwana, nao ukaleta kware kutoka pande za baharini, nao ukawaacha wakaanguka karibu na kambi, kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, na kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, kuizunguka, nao wakafikilia kiasi cha dhiraa mbili juu ya uso wa nchi. Hesabu 11:31

There went forth a wind from Yahweh, and brought quails from the sea, and let them fall by the camp, about a day's journey on this side, and a day's journey on the other side, round about the camp, and about two cubits above the surface of the earth.

Watu wakaondoka mchana huo wote, na usiku huo wote, na siku ya pili yote, kuwakusanya hao kware; yeye aliyepata ya upungufu kuliko wenziwe alipata kiasi cha homeri kumi; nao wakawaanika wote kando-kando ya kambi kuizunguka pande zote. Hesabu 11:32

The people rose up all that day, and all the night, and all the next day, and gathered the quails: he who gathered least gathered ten homers: and they spread them all abroad for themselves round about the camp.

Kisha hapo hiyo nyama ilipokuwa ikali kati ya meno yao, hawajaitafuna bado, hasira za Bwana ziliwaka juu ya watu, Bwana akawapiga watu kwa pigo kuu mno. Hesabu 11:33

While the flesh was yet between their teeth, before it was chewed, the anger of Yahweh was kindled against the people, and Yahweh struck the people with a very great plague.

Jina la mahali pale likaitwa Kibroth-hataava; maana, ni hapo walipowazika hao watu waliotamani. Hesabu 11:34

The name of that place was called Kibrothhattaavah, because there they buried the people who lusted.

Kutoka hapo Kibroth-hataava watu wakasafiri kwenda Haserothi; wakakaa huko Haserothi.

Hesabu 11:35

From Kibrothhattaavah the people traveled to Hazeroth; and they abode at Hazeroth.